Historia Mpya ya Zanzibar yaandikwa "kwa heri ukoloni kwaheri Uhuru" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia Mpya ya Zanzibar yaandikwa "kwa heri ukoloni kwaheri Uhuru"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Nov 23, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naam nimekisoma hiki kitabu kilichoandikwa na Dr Ghassan kwa kweli kina mengi ya kustaajabisha na ambayo yalikua hayajulikani na pia kuna migongano ya historia tuijuayo na hii


  tukisomeni na kuchangia juu ya historia hii mpya kama ilivyoandikwa na mzanzibari huyu
   
 2. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Kinapatikana wapi??? tupe source
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  ...soma kwanza hii makala ...

  ZANZIBAR UTATA MTUPU
  Kwa wanafiki na wenye uchu wa madaraka hili linaweza kuchukuliwa kama swali la uchochezi, swali la kutaka kuvuruga amani na utulivu wa watanzania. Wenye upeo wa kuangalia Tanzania ya miaka ijayo, hili ni swali la msingi.

  Tusiangalie amani na utulivu wa leo na kesho na kusahau kwamba Tanzania itaendelea kuwepo miaka mingi inayokuja. Tunaweza kuweka pembeni maswali muhimu kwa lengo la kutaka leo hii tuishi kwa amani na utulivu huku tukijua kwamba kila lifunikwalo kwa nguvu hufumuka na kusababisha maangamizi.

  Historia haiwezi kutusamehe kwa kosa letu la makusudi la kuviandalia vizazi vijavyo maangamizi ya kuchinjana na kuikimbia nchi yao kuishi uhamishoni.

  Ushindi wa CCM wa pointi moja unaacha maswali mengi zaidi ya majibu. Yako matukio mengi yanayowasukuma baadhi ya watu ndani na nje ya nchi kutilia mashaka ushindi huu. Siku moja kabla ya kutangaza ushindi;

  wafuasi wa CUF kwa kujua wameshinda walizunguka kituo cha kutangaza matokeo ya kutangazia kura kwenye Hoteli ya Bwawani kwa lengo la kuishinikiza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) , iwatangaze washindi.

  Hali ya hewa ilibadilika; Jeshi likaanza kujiandaa, baadhi ya sehemu zikawa zinalindwa na wanajeshi. Marais wastaafu wa Muungano Mzee Mwinyi aliingia Zanzibar kimya kimya ili kuhakikisha kosa halifanyiki la CCM kuachia madaraka. Vigogo wengine wa CCM nao
  walifika Zanzibar kwa lengo lile lile.

  Kilichokuwa wazi ni kwamba ushindi wa kura haukuwa na maana tena.

  Muhimu ilikuwa ni kuyalinda mapinduzi matukufu ya mwaka 1964. Wazanzibari wenyewe wanasema ushindi wa kura si neno; la msingi nikupewa. Maana yake unaweza kushinda usipewe!
  Pamoja na ukweli kwamba hata mimi wakati huo nilikuwa Zanzibar nikifuatilia matukio yote haya kwa karibu, sitajadili yote haya kwenye makala haya.

  Siku za mbeleni baada ya vumbi kutulia na shughuli za kawaida kuendelea, baada ya kushuhudia baraza jipya la mawaziri na uteuzi mwingine nitajitosa kujadili Zanzibar, Muungano na hatima ya vyama viwili vikubwa vya CCM na CUF.

  Wiki iliyopita Mheshimiwa Rais Ali Mohamed Shein, alifanya uteuzi wa baraza la wawakilishi kwa kuwachagua sita wa CCM na wawili wa CUF, kwa vyama vinavyozidiana pointi moja tu, uchaguzi huo haukuwa na uwiano hata kidogo.

  Bado ni mapema; subira yavuta heri! Leo nijadili jambo la wazi kabisa ambalo hata wachambuzi na vyombo vya habari makini vimekataa kulijadili.

  Nalo ni kwa nini Profesa Lipumba amepata kura nyingi kule Zanzibar zaidi ya Seif Sharif Hamad? Wakati Lipumba ana zaidi ya asilimia 60, Seif Sharif Hamad ana asilimia 49.1.

  Hili ni muhimu sana kujadili maana mwishowe linaweza kutujibia swali letu la nani alishinda Zanzibar. Tunaweza kufahamu wazi ni nani alishinda na hakupewa na ni nani alishindwa akapewa.

  Inawezekana kabisa kwamba watu waliompigia kura Lipumba, ambao wazi ni wale wa CUF, hawakumpigia kura Seif.

  Hili linawezekana maana kura ni siri ya mtu na inafuata mapenzi yake kwa yule anayemtaka, lakini si kwa Zanzibar ambako kura ya rais wa Zanzibar ni muhimu zaidi ya kura ya Rais wa Muungano.

  Inawezekana kabisa mtu akampigia Seif na asimpigie Lipumba na si kinyume chake. Kwa Wazanzibari, Zanzibar inakuja kwanza na muungano ni baadaye.

  Hata hivyo, kama CUF, walimpigia kura Shein na kumtosa Seif, basi CCM ingeweza kuchukua walao kiti kimoja kule Pemba.

  CUF, ilifanikiwa kujinyakulia viti zaidi ya vitatu Unguja, lakini CCM ikaambulia patupu hata kule anakozaliwa Shein mwenyewe. Hata kama mtu hukusomea sayansi ya siasa, anaweza kuona ukinzani unaojitokeza wazi wazi katika hoja hii ninaojaribu kuileta hapa.

  Hoja ninayotaka kuijenga hapa ni kwamba kama kilichofanyika kule Zanzibar ni uchakachuaji, basi waliofanya hivyo ni wanafunzi wa kuchakachua na si watu makini, maana wangehakikisha wanaondoa utata huu ambao kama si leo hata kesho wenye akili timamu watasimama na kuhoji, kwanini Seif apate asilimia 49.1 na Lipumba apate zaidi ya 60 wakati wapiga kura ni wale wale wa chama cha CUF?

  Haiwezekani watu wale wale wamchague mbunge wa CUF, mwakilishi wa CUF na Diwani wa CUF na kukataa kumchagua rais wa nchi wakati shauku yao kubwa ilikuwa ni kuiongoza kwa mara ya kwanza serikali ya Umoja wa kitaifa. Katika akili ya kawaida hili haliwezekani.

  CUF wanajua wameshinda, lakini hawakupewa. CCM wanajua wazi kabisa kwamba CUF wameshinda lakini hawako tayari kuwapa; na si kweli kwamba CUF wameamua kunyamaza kwa vile wana imani ya kuingizwa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.

  Na si kweli kabisa kwamba Maalim Seif, amekuwa msaliti wa CUF kwa kujua kwamba ataingizwa serikalini kuwa Makamu wa kwanza wa Rais. Kuwafikiria hivyo Maalim Seif na viongozi wenzake wa CUF ni kuwavunjia heshima na kuwakosea haki.

  Hawa wameonyesha uzalendo, busara na hekima. Wameitanguliza Zanzibar badala ya kutanguliza masilahi yao binafsi. Kama CUF, wangesimama kidete kudai ushindi wao kwa nguvu; Zanzibar ingeshuhudia machafuko makubwa zaidi ya yale ya 2002.

  Swali langu ni je uvumilivu huu wa Seif Sharif Hamad wa kushinda akakubali kushindwa ili kuepusha shari utaendelea hadi lini? Vizazi vijavyo vitakuwa na uvumilivu huu? Na je

  kwa nini uvumilivu huu uwe wa upande mmoja kana kwamba kule Zanzibar kuna watu ambao wana haki zaidi ya wengine? Kwanini CCM isijifunze kukubali kushindwa? Kwa nini dhana nzima ya Mapinduzi Daima isiwe na maana mpya ya mapinduzi katika maisha ya kila siku ya Mzanzibari;

  kufukuza umasikini, kufukuza ujinga kwa kuhakikisha kila Mzanzibari anapata elimu bora; kujenga uchumi bora na imara. Mapinduzi ya 1964 pamoja na umuhimu wake ambao unajenga historia isiyofutika umepitwa na wakati.

  Kuyalazimisha mapinduzi haya katika nyakati hizi tulizomo ni kutaka kuzalisha maasi ya leo na ya vizazi vijavyo.
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Ng'wanangwa!! Kweli umefikiri mbali mkuu, umeandika pasina shaka. Nilipata kudokeza lakini wanamageuzi wa Jamvini hawakutaka kuliona hilo, wengi wetu hapa tunaiangalia leo, lakini si miaka 5 ijayo, si miaka 50 ijayo. Ndio maana vuguvugu la mageuzi TZ liko kama homa ya vipindi. mara inapanda hivi au inashuka... :teeth:
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwa upande wangu serikali a umoja zanzibar sielewi na mwisho wake ni lini na nini!? Naona imekaa kama boom hivi litakuja kulipuka siku moja, ni sawa na muungano nao umekaa kulipukalipuka tuu!
  Siombei hilo, ila ni kitu ninachokiona kuwa huu muungano na serikali ya zanzibar hazijakaa vyema!
  Huu ni mtazamo wangu tu!
   
 6. r

  roby m Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Kaka Ng'wanangwa no comment katika hilo:redfaces:
  i real support you
   
 7. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Bila shaka huo ndio ukweli. CUF ilishinda Zanzibar tena pasipo shaka. Nilifuatilia sana kila matokeo ya wawakilishi, wabunge na urais yakitangazwa na kila mara kwa wastani wawakilishi na wabunge wa CUF Pemba walipata zaidi ya 80% ya kula katika kila jimbo, kwa Unguja walipata karibu zaidi ya 35% ya kura za majimbo. Pia CUF wameshinda majimbo manne upande wa Unguja, ukiachia mbali majimbo karibu 4 waliokabana koo kwa Unguja.

  Na niliamini pasipo shaka kuwa muafaka wa Zanzibar ilikuwa ni ticketi ya CUF kushinda kwa idadi ya ya kura kirahisi kwa Wapemba wengi walipewa chance ya kupiga kura lakini kumbe CCM wana jua mbinu zao kwamba hoja sio kushinda kwa uwingi wa kura bali ni kutangazwa na tume, ZEC.

  Ni ajabu na kweli Shein kutangazwa kushinda na Hamad kwa haraka na upole usio wa kawaida kuwa wa kwanza kuwatuliza wafuasi wake.

  Hapo nikaamini kuwa lazima hamad ameambiwa na kuukubali ukweli kuwa bora CUF washirikishwe kwenye serikali kuliko kuporwa ushindi na kutoshirikishwa kabisa, kwani CCM Zanzibar hawapo tayari kuwatangaza CUF washindi hadi mbingu ishuke.

  Na napata hisia kwamba Hamad ameujua ukweli kuwa CCM Zanzibar hawapo tayari kumuona hamad akiwa rais wa Zanzibar mpaka afe, labda watoto au wajuu wake.

  Naamini hivi ndivyo itakavyo kuwa

  Lakini nikashanga
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  2005 Sikumpa Kura Yangu JK; 2010 Sikumpa Kura Yangu JK. Kwa Sababu JK Ni Chekibobu. Siwezi Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Bora Nife Tu, Kuliko Kutoa Kura Yangu Kwa Chekibobu. Chekibobu Hastahili Kuwa Rais wa TZ. Ndiyo Maana Tuna Matatizo Mengi Kwa Sababu ya Huyu Chekibobu JK.

  Waonyeshwa mchana jua, wewe wasema hii ni mbalamwezi. Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii
   
 9. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
 10. MMDAU

  MMDAU Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mada ya zanzibar hata mtoto Mdogo anajuwa wazi kuwa CUF walishinda licha ya ushahidi ulio elezwa. dhambi ile iliyotumika kuwadhulumu ushindi CUF ndio itakayo pelekea zanzibar kujitenga na muungano kwani wanzanzibar wameona kuwa hawasikilizwi na serikali ya muungano kwa sera ya chama tawala. Chama tawala kimekuwa kikiwadhulumu wanachi wake maendeleo na wamefanya hivyo mpaka huko zanzibar hivyo zanzibar ikiangalia historia ya dola yake inagundua kuwa hadhi yake imeshuka na kuwa kama mkoa.
  nawashauri wasikate tamaa na kupigania nchi yao kwa maendeleo yao na vizazi vyao
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2017
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!

  Harith Ghassany

  info@kwaherikwaheri.com

  Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani.

  Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:

  • Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi binafsi ya kitabu
  • Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo wa kitabu
  • Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi
  Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/

  Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi.

  Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu.

  Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao. Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, http://kwaherikwaheri.com au moja kwa moja kutoka http://lulu.com na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu http://kwaherikwaheri.comikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao.

  Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao.

  Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake.

  Mnakaribishwa nyote—walio karibu na walioko mbali.


  Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!

  Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia

  Copyright 1431 Anno Hegirae / 2010 Anno Domini by Harith Ghassany

  Library of Congress Cataloging-in-Publication Data

  Mapinduzi ya Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ukweli na Mapatano, Zanzibar na Oman, Afrabia, Masomo ya Afrabia.

  English translation of title:

  Goodbye Colonialism, Goodbye Freedom! Zanzibar and the Afrabia Revolution

  Keywords:

  Zanzibar Revolution, Union of the Republic of Tanzania, Truth and Reconciliation, Zanzibar and Oman, Afrabia Studies.

  Printed in the United States of America
   
 12. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2017
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Kulikoni bi Faiza leo unafukua MAKABURI?
  Mbuzi wa Bwana Kheri, Mahindi ya Bwana Kheri hata shamba nalo la Bwana Kheri aaah yote kheri tu!!
   
Loading...