Makonda anatukumbusha kuwa CCM ni kubwa kuliko Serikali

Tao

Member
Nov 10, 2018
95
157
PAUL MAKONDA ANATUKUMBUSHA KUWA CCM NI KUBWA KULIKO SERIKALI

Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Christian Makonda anafanya kazi nzuri sana ambayo kila mwana CCM na Mtanzania yeyote ambaye ni mpenda maendeleo anapaswa kuikubali.

Makonda anatukumbusha kuwa Chama Cha Mapinduzi ndiyo Chama tawala na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeundwa na CCM ili kusimamia sera za CCM.

KATIKA mfumo wa kidemokrasia Chama Cha siasa ndicho kinachounda serikali baada ya kushinda uchaguzi hivyo Chama Cha Mapinduzi kina wajibu mkubwa wa kuisimamia serikali yake.

Wananchi wanapopiga kura hawaichagui serikali isipokuwa Chama Cha Siasa.

Tokea Makonda alipoteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM na hasa baada ya hotuba yake ya jana pale jinini Dodoma Kumekuwepo na minong'ono ya chini kwa chini kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuwa Makonda anaingilia kazi na majukumu ya wakubwa zake katika Chama na serikali-Hii si kweli, ukweli wenyewe ni kuwa Makonda anakijenga na kukiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi na hili ni jambo muhimu kwani Chama Cha Mapinduzi ni moja ya urithi muhimu tulioachiwa na waasisi wa taifa hili na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba"

Waziri au waziri mkuu hawezi kamwe kuwa mkubwa kuliko CCM

Rais wa Tanzania hawezi kuwa mkubwa kuliko CCM iliyompa dhamana.

Makonda anapotoa maelekezo kwa viongozi wa serikali hafanyi kosa lolote.

Makonda anapowataka mawaziri kutoa taarifa kwenye Chama Cha Mapinduzi kila baada ya miezi mitatu yuko sahihi na katika hili kusitokee timbwilitimbwili zisizo na maana na sasa ifike mahali kauli hiyo izingatiwe na huo uwe mfumo wa CCM kuisimamia serikali yake.

Kama CCM itashindwa kuisimamia serikali yake ipasavyo basi kitambue kuwa kimechoka kutawala.

Naunga mkono hotuba yote aliyoitoa Makonda huko jijini Dodoma na kwa kauli moja nasema "Kazi imempata Mwenyewe.
 
I don't like this guy, but ameongea ukweli, ccm ni kubwa kuliko serekali maana ndiyo inayopigiwa kura nayo inawapanga watendaji wake watakaoisaidia kutimiza ahadi ambazo CHAMA kimewahahidi wapiga kura wake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom