Hisabati/mathematics nightmare | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hisabati/mathematics nightmare

Discussion in 'Great Thinkers' started by Sangarara, Oct 23, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Somo la hisabati ni somo ambalo naweza kusema limekuwa ni daraja la mafanikio ya binaadamu kitaaluma (ambayo mpaka sasa duniani kote ndio kitu kinachochukuliwa kama mlango wa mafanikio ya kimaisha hasa uhakika wa maisha mazuri kwa binadamu wote ikibebeshwa na vijimisemo kama EDUCATION IS KEY..., EDUCATION IS POWER n.k

  Nasema ni daraja kwa sababu ya umuhimu linalopewa katika mchakato mzima wa kielemu, tokea shule za msingi (sasa chekechea) mpaka vyuo vikuu, wale wanaofanikio/bahatika kuwa na uwezo mkubwa wa hisabati ndio uheshimika na kuonekana kama watu wenye uwezo wa hali ya juu wakati wale wanaoonyesha udhaifu kwenye somo hili huchukuliwa kama wajinga na si watu wanaotegemewa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

  Ukichukulia mitihani ya darasa la saba, wale wanaofaulu vizuri sana kwenye somo la hisabati ndio upewa kipaumbele katika nasafi sa special schools kama tabora boys, mzumbe, na ilboru.

  na pia ikifika secondary, ni vipanga wa hisabati ndio wanopewa kipaumbele kuchukua mchepuo wa sayansi, ambako ndiko hata wanaofaulu sana masomo ya arts hutokea.

  kuingia chuo kikuu, ufaulu wa somo la hisabati a-level na o-level inapewa kipaumbele ili kupata nafasi hiyo.ambako pia somo la hisabati linafundishiswa karibia katika programs zote isipokuwa sheria kama sikosei.

  haiishii hapo, hata makazini, kupata first job inategemea na ulivyofaulu hisabati o-level na a-level, kuna kampuni nimefanyia kazi, ili uitwe kwenye first interview ni lazima uwe una at least D ya hisabati o-level ama sivyo unapigwa chini.

  Kwa kifupi, hisabati katika mchakato wa elimu ni kama pumzi kwenye maisha ya viumbe hai, swali nalojiuliza ni kama kuna ulazima wa hii kitu kupewa kipaumbele kikubwa namna hii kwenye maisha yetu. tukifanya utafikiti wa kina tunaweza kukuta kwamba watu wengi sana tena mamilioni walikatishwa na wanaendelea kukatishwa tamaa ya kujiendeleza kielimu na hata kimaisha kwa sababu tu at one point katika maisha yao hawakumaster somo la hesabu.

  nahoji umuhimu huu kwa sababu, si kweli kwamba tunahitaji uelewa mkubwa sana wa hesabu katika kuendesha maisha yetu ya kila siku, angalia tanzania, asilia 80% yetu ni wakulima, ambayo ni sawa na watanzania Milioni 40, tukiangalia mchakato wao wa kimaisha wa kila siku hakuna sehemu utakuta wanahitaji application ya hesabu, lakini pia utakuta hao wote at one point katika maisha yao walikutana na mchakato wa kujifunza hisabati ambao uliwadisappoint vibaya sana.

  nani hapa anaweza akanithibishia kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kuna wakati wowote ule logarithm au calculus, au propability theories ilimsaidia katika kujipatia kipato chake au kuboresha maisha yake katika namna yoyote ile?
  kama hakuna, ya nini kuwashurutisha watu kupitia kwenye mchakato ambao hautakuwa sehemu ya maisha yao mara tu baada ya kutoka kwenye mchakato wa elimu.

  Hivi sasa kila baada matokeo ya mitihani ya darasa la saba na form four yanapotoka, kila gazeti na vyombo vingine vya habari linaibuka na takwimu kuonyesha ni namna gani hesabu ni janga la kitaifa utadhani wale waliofeli watakufa kesho wakati ukweli ni kwamba vijana hawa wanachokihitaji kwenye maisha yao ni MAYAMAZIJUTO tu. sijui kama tumewahi kutafakari ni damage kiasi gani imbayo inatokea kwenye maisha ya vijana hawa kwa sababu tu wamekuwa labeled kama wajinga wa hisabati? ama, ni wanaadamu wangapi leo wanataabika na maisha kwa sababu at one point kwenye maisha yao walikuwa disappointed na hisabati

  Naomba kuwasilisha hoja.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Consider Computer science program pale chuo kikuu cha Dar es Salaam, kuna kipindi program hii ilikuwa inadahili wanafunzi 25 tu mwaka na hawa ni wale walioscore A kwenye mitihani ya kidato cha sita, hili lilikuwa linafanyika huku ikieleweka wazi kwamba gulu wa computer Mr. Bill Gates ni college drop out, sina hakika kama alifail hisabati au la, lakini at least ingeweza kutuma ujumbe kwamba it is not mathematics which matters.

  Then angalia kama kweli computer applications tunazotumia zinahitaji hisabati ki vile, angalia computer programs kama ni kweli wanasctrach heads kuapplie zile mahesabu, hakuna. Kisha angalia ni watanzania wangapi walinyimwa fursa ya kujiendeleza katika fani hii adhimu at their tender ages kwa kitu ambacho in fact hawakukihitaji. Who is going to pay for this?

  Kwanini hesabu isiachwe kwa wanahesabu kama philosophy ilivyoachwa kwa wanaphilososy as long as vyote viwili havina msaada wowote kwa maisha ya wengi wetu.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Somo la Hisababti umuhimu wake hauko kwenye kukukotoa namba tu kama ambavyo wengi wetu wanavyodhani. Umuhimu mkubwa wa hisabati uko kwenye ile misingi yake ya kutoa ufumbuzi wa nadharia (proof of theorems).

  Mtu anapojijengea uwezo kuweka nadharia na kuzifumbua anakuwa anapanua sana uwezo wake wa kuona mambo kwa kina. Ndiyo maana wavumbuzi wakuu wa kisayansi kama akina Newton na akina Einstein (siyo wafanya biashara watumiaji wa sayansi kama akina Bill Gates na akina Steve Jobs) huwa wana uwezo mkubwa sana wa hisabati.

  Digrii nyingi za udaktari wa falsafa katika sayansi huko Marekani zinahitaji mtu awe amepasi hisabati kwa kiwango cha juu sana.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bill Gates ni mathematical genius
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Huyo ni mtumiaji wa sayansi ya namba, siyo mathematical genius hata siku moja. Angalau wale jamaa wa Google walikuwa ni mathematical geniuses kwa kuvumbua algorithm ya page rank number.

  Bill gates hakutoa algorithm yoyote; products zake nyingi zinatumia algorithm za kizamani sana, na alivyojingiza wahindi wengi kwenye kampuni yake akajilazimisha kuwa na product hafifu sana.

  Kuna Code moja ya mwanafunzi wetu iliingizwa kwenye product moja ya microsoft bila ridhaa yake na kusababisha mtafaruku, MS wakaamua kusawazisha mambo nje ya mahakama.

  Ndiyo maana product za Microsoft zimekuwa ni nzito sana siku hizi. Kampuni yako ikitumia server ya Outlook kwenye email basi ujue utakuwa unasoma email zako baada ya nusu saa. Packages zote za Microsofot office ni inefficient kiasi kuwa unahitaji memory kubwa sana ili kuzitumia. Watu wengi wanahamia kwenye cloud computing kwa sababu personal computing imeshindwa, na microsoft haikuhimiri kuistabilize.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kama kuna hoja ambayo natamani nije kuiandika kabisa ni ile ya "Hisabati msingi wa maendeleo". Mataifa yote ambayo yamepiga hatua ya haraka ya maendeleo ni yale yaliyopiga hatua katika hisabati. Ilipokuwa inasemwa kuwa "hisabati ni mama ya sayansi" ni kweli.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mathematics is very important in all sciences. Especially in developing models. N models ndo solution ya mambo yote!
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hisabati ni muhimu sana umeona wewe mwenyewe ulioleta huu mjadala huku Great Thinkers unasema Watanzania 80% ni wakulima hii hesabu umeipata wapi...Mataifa makubwa ambayo yamewekeza kwenye kilimo wananchi wake ambao ni wakulima hawafiki hata 20%. Tungekuwa hivyo afrika nzima wangeitegemea Tanzania kwa chakula.
   
 10. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Naamini katika ukweli wa aina mbili chini ya jua.
  Kuna FACTS na LOGIC. Facts ni katika "science-studies of life" wakati Logic ni katika Socialogy-studies of life. Mama wa FACTS ni HESABU wakati mama wa LOGIC ni REASONING!
  Hivyo si rahisi kuipuuza HESABU, mother of FACTS!
  Mungu wetu anaita sasa!
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kichuguu

  Kwani kuwa mathematical genius ni mpaka uwe na sifa zipi? Manake somo la hisabati Bill alikuwa analimudu vizuri sana enzi za uanafunzi wake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,696
  Likes Received: 8,232
  Trophy Points: 280
  Hesabu ni nzuri sana we X2
  Mwalimu nifundishe nipate kuelewa
  ee mwalimu eem mwalimu nifundishe!

  Maths is just but a game of numbers!

  Nadhani kama tungetumia nguvu zaidi ku-sensitize wanetu juu ya umuhimu wa somo hili wala tusingelalamika kama mtoa mada.
  Wazazi tunabeba lawama zaidi linapokuja suala hilo kwani utakuta mzazi anamwambia mwanaye, "Aah hesabu! huo ugonjwa wa taifa bana!" "Hata mimi nlikua hivyohivyo wala usijali mwanangu"

  Akienda shule anakutana na wengine wa madarasa ya juu nao wanasema vivyo hivyo. Ina kuwa matatizo matupu.
  Tunatakiwa kuwatia moyo na kuwafanya wapende somo hilo (like wise Biology - sio tu ili aje kuwa doctor- na masomo mengine ambayo tumeyapa unfitting names).

  I commend my dad kwa kutufanya tuipende hesabu na kusoma vitabu.
  Just kama ushuhuda: Kwenye familia yetu ya watoto SITA wote tulipata A za hesabu regardless ya shule tofauti tulizosoma (Old Moshi Sec., Mawenzi Sec., Olduvai Sec., St. Mary Goreti, na Agape seminary).
  So its up to us to provide the solution na kuacha kulalama so what..unataka sote tuwe Bill Gates. Kwanini hutolei mifano ya Newton na wengine!??
   
 13. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Am not a mathematician but katika pitapita zangu hasa kwenye falsafa nimejifunza kwamba maths ndio kilele cha mang'amuzi ya fikara za mwanadamu.
  Ukamilifu wa mahesabu unajengwa katika abstract thinking, wanafalsafa na wanasayansi wakubwa waliofanya mang'amuzi makubwa katika historia ya binadamu kutoka kwa kina Plato, Aristotle, Pythagoras, Galileo, Newton, Einstein mpaka wanasosholojia na wanapsychology kama Karl Marx na Mead, hawa wote walikua mathematicians wazuri au walijengwa vizuri katika mfumo wa kimahesabu.

  Kwa hiyo kama tuna nia ya dhati katika kuendeleza kizazi chetu na vizazi vijavyo kifikara, maths ni lazima na ni muhimu, kwani maendeleo mazuri ya fikara ndio yatatuletea maendeleo halisi katika material things kama social service, miji, uchumi n.k
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Vizuri, hisabati inatumika kutoa proof of theorem, ni maamuzi gani ya kimaisha (basici decision) ambayo tunalazimika kuapply theory yoyote ile. Kwa mfano, asilimia karibia 98 ya members hapa JF wanajadiri siasa na hasa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kama kweli maamuzi ya kisiasa (uchaguzi) ni kitu ambacho ni sahihi kufikirika kwamba yanaimpact katika maisha yetu ni hisabati gani inatumika katika kuyafikia au theorem ipi? na kama hamna why bother everyone with it?
   
 15. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Sisi tupo bize na mutiple choice , tena A,B,C tu angalau ingekuwa A,B,C,D,E,F,J
   
 16. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  hivi kweli mwanakijiji kama hisabati ni kitu muhimu namna hivyo kwa nini ihitajike mpaka iandikiwe ndio watu waone umuhimu wake? any way ukiandika usisahau kutukumbusha namna tunavyotumia calculus kwenye kilimo cha umwagiliaji huku mfindi.
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hata hiyo falsafa tu ni questionable kama kweli ima impact kwenye maisha ya wengi wetu, ukisoma vizuri maandiko yako utagundua karibia hayo yote uliyoandika sio kweli kwamba bila hayo maisha yangekuwa magumu hapa duniani.
   
 18. Mourinho

  Mourinho JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,622
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo unataka kusema vitu kama vyombo vya usafiri, madawa and medical procedures, communication systems n. k vingekuja/vimekuja kuwepo bila ya manguli wa mahesabu?
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Ile misingi inayotumika katika kujenga hoja wakati wa kuprove theorem ndiyo msingi inayotumika pia katika kujenga hoja ya kutatua matatizo mengine ya kijamii. Usichukulia reproduction ya material bali angalia application ya methods. Mathematician mzuri siyo mkurupukaji katika mambo yake; kila jambo analiangalia kwa makini na kina sana. Huo utamadunbi wa kuangalia mambo kwa kina ndio unawafanya wawe na mtazamo mpana sana wa kila jambo na hata katika mambo ya jamii. Utashangaa kuwa mathematician aliyeiva hawezi kukubali kuwa 3+1.0=4, ingawa watu wa kawaida wanaojua hesabu za kukokotoa tu watamshangaa.
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Sisemi hesabu is nothing, nacholalamika ni kwa nini kila mtu alazimishwe kuisoma na ifanywe kizingiti kwenye michakato ya kielimu wakati application yake sio ya muhimu kiivyo, Ni ya muhimu sana tena sana lakini does every one need to master it? kwani kila mtu anatengeneza ndege au meli? au kila mtu ni medical technician?

  hata kama, madaktari na mafamasia kwenye mahospitali yetu wanatumia hisabati gani wakati wanatuhudimia, watakupima uzito na ulefu labda basi, why calculus? hata numerical presentation ya vipimo vyao haitusaidii wagonjwa chochote kile ni vague technical and medical industry centered jargons, hata leo wakina newton wakija ukawaambia wanamalaria 3 watabaki kushangaa,

  naendelea kuuliza, kwa nini? watoto wetu wanafeli darasa la saba sababu wameshindwa kutafuta kigawe kidogo cha shirika, au eneo la nusu mlinganyo, hata wale waliofaulu, ufahamu wa kubadirisha desimali kuwa sehemu unawasaidia nini immedietly baada ya masomo yao au lately wakati wa uzee wao?
   
Loading...