Hisabati/mathematics nightmare

hata mwal nyerere siku moja alishawahi kusema ktk moa ya speech zake alishasema tuwe na elimu ya kujenga uelewa na sio kukariri na kujibu mitihani tunakuwa tumepoteza muda wetu for nothing.
 
namshukuru sana mungu kwa kuwa nimekuwa tofauti sana, yale yote niliyoyasoma yote yamekuwa msaada kwangu na kunifanya nielewe mambo mengi ya dunia inayonizunguka sijuti kusoma chochote nilichosoma kwa namna moja ama nyingine nimeweza kuyatumia katika day to day life. na nimeweza kuyaleta katika uhalisia wa mambo yanayoendelea kila siku. najipa hongera mwenyewe kwa jitihada zangu binafsi za kuyaconnect na kuyatumia na kuona manufaa yake. elimu ni nzuri sana na ni jambo jema kama wenzangu watanzania watakuwa na uelewa ama wawe kama mimi nilivyoweza kuyaleta mambo niliyoyasoma katika maisha ya kila siku.
 
Sisemi hesabu is nothing, nacholalamika ni kwa nini kila mtu alazimishwe kuisoma na ifanywe kizingiti kwenye michakato ya kielimu wakati application yake sio ya muhimu kiivyo, Ni ya muhimu sana tena sana lakini does every one need to master it? kwani kila mtu anatengeneza ndege au meli? au kila mtu ni medical technician?

hata kama, madaktari na mafamasia kwenye mahospitali yetu wanatumia hisabati gani wakati wanatuhudimia, watakupima uzito na ulefu labda basi, why calculus? hata numerical presentation ya vipimo vyao haitusaidii wagonjwa chochote kile ni vague technical and medical industry centered jargons, hata leo wakina newton wakija ukawaambia wanamalaria 3 watabaki kushangaa,

naendelea kuuliza, kwa nini? watoto wetu wanafeli darasa la saba sababu wameshindwa kutafuta kigawe kidogo cha shirika, au eneo la nusu mlinganyo, hata wale waliofaulu, ufahamu wa kubadirisha desimali kuwa sehemu unawasaidia nini immedietly baada ya masomo yao au lately wakati wa uzee wao?

Ndo maana kuna post yako moja umesema waajiri watahitaji angalau mtu aliyepata D kwenye hesabu katika mtihani wake wa O-level, katika hali halisi mtu aliyepata D O-level hawezi kuwa anajua Calculus na mahesabu mengine magumu magumu kama vector space, na majometri ya ajabu ajabu sana sana atakuwa anajua tu hesabu basic na milinganyo rahisi rahisi yenye single variable pamoja na hesabu zingine za Magazijuto na vijometri ya kutafuta maeneo pamoja na mizingo kitu ambacho utaweza kukitumia kujua hata ukitaka kujenga tank lako la maji lenye ujazo wa lita elfu ishirini basi liwe na vipimo gani, sasa mkuu wangu unataka tuwe na kizazi ambacho hata ukimwambia akufanyie tathmini ya tofali utakazotumia kujenga kibanda cha bati 30 anaanza kushangaa hata hajui aanzie wapi.

Tafadhali mkuu tunataka angalau basi watu waliopata D sio lazima wenye kujua mahesabu magumu ambayo mengi yanatumika kwenye engineering design.
 
Nadhani hapo ndipo kwenye mzizi wa tatizo hili. Walimu wengi hawafundishi kwa kuelezea nadharia zenyewe na namna unavyoweza kuzitumia katika maisha ya kila siku, badala yake wanafundisha namna ya kujibu maswali ya kwenye mtihani.

Hata mifano inayotumiwa kuelezea nadharia hizo wakati mwengine inakosa uhalisia wa mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi. Walimu wanakosa ubunifu wakati wa kutumia vitabu vya kufundishia na kukosa kuvijenga kuendana na mazingira yaliyomzunguka mwanafunzi.

Naamini tatizo lipo kwenye aina ya walimu wanaopelekwa huko mashuleni. Mwalimu wa shule ya msingi ni yule aliyefeli (almost) Form four. Anafundishwa kidogo, anakabidhiwa darasa. Hatuwezi kutarajia maajabu kutoka kwa walimu hawa hususan wanapotakiwa kufundisha wanafunzi 80 kwenye darasa moja.

Mimi nilikuwa home-schooled (almost kwa primary school) na nadharia zote za hisabati zilikuwa customized wakati wa kuzieleza kuendana na interests zangu na vitu ninavyovijua vyema, hivyo ilikuwa rahisi sana ku-relate na maisha ya kila siku. Na kuweza ku-relate na maisha ya kila siku, kulinifanya niwe na interest na hisabati.

Ninachotaka kusema ni kuwa, interest na uelewa wa mtoto kwa somo la hisabati unachangiwa na mambo mengi, ikiwemo walimu, vitabu na mazingira ambayo kimsingi kwa Tanzania katika yote hayo tumepwaya sana.

Gaijin:

Now we converge. Nyumbani ulikuwa unafundishwa kwa kutumia mifano ya dunia yako ya ufahamu, so your home instructor was cultivating your ability to think critically naturally.

We, on the other hand, who attended public schools didn't have that luxury and we are punished for that. I am punished because I failed to answer a simultaneous equation. However, in book keeping, counting money, construction of simple building etc and in our daily lives we don't use simultaneous equations or her cousin quadratic. So why is that a big deal?

Please refer the dialog below between the great philosopher Socrates and a slave boy.
Halving a square
 
mkuu zakumi,
ni kweli nimepata mafanikio mazuri kutokana na hayo mambo, na imenisaidia si tu kujenga hoja vizuri, bali imenipa busara, hekima, heshima, na kuwa na mipango mizuri katika maisha yangu ya kila siku, si hayo tu imenijenga kuwa mdadisi mfuatiliaji na mtekelezaji mzuri na wa umakini wa mipango yangu. imenijenga kuwasoma watu kuwaelewa watu na kuishi na watu kwa namna ya busara. and never to take things for granted.

si lazima watanzania wapitie njia kama yangu ila ni muhimu kama inawezekana,( na inawezekana) mafanikio sio jambo nilitakalo mimi tu ni kitu watu wote wanatamani kukipata.

IL,

Cha muhimu tusiwaangalie watanzania wenzetu kuwa wanaelimu ndogo au hawawezi kujenga hoja. Wanajenga hoja kutokana na dunia yao which by the way isn't western.

Please click the link below and read the dialog between Socrates and uneducated slave boy.

Halving a square
 
nafikiri zaidi ya yote tuliyoyaonge masomo mengi yanavyofundishwa hapa kwetu ni kukopi na komeza na kutapika kwa ajili ya mitihani. hili ni kosa kubwa sana. ndio maana waajiri wanalalamika kuwa watu wanatoka chuoni hawana kitu si kweli hawana ila wameshasahau kutokana na usomaji wa kukariri akimaliza pepa usiku muulize chochote hana kashatema katika mtihani na kamalizana nalo. hapa mtu huyu hawezi kuwa mbinifu wala mtu wa kutafakari na kutumia ujuzi na uelewa wake katika maisha yake ya kila siku.
sasa tukibadili mfumo huu na kuwa na mfumo wa kuelewa na sio kuangalia A's basi taifa litabadilika.

Hiyo ndio point muhimu hapa. Kuna kipindi nirudi Tanzania na nikamuuliza ndugu yangu aliye form II anipe past paper zake za form II. Kwenye Jiografia alikuwa ameboronga kwelikweli. Nikatafsiri maswali aliyokosa kwa kiswahili na aliweza kuyajibu kwa hoja nzuri.

Kwa kutumia kigezo cha mitihani, huyu jamaa alikuwa ni mbumbumbu. Lakini kwa kutumia lugha yake sio mbumbumbu hata kidogo.
 
Ndo maana kuna post yako moja umesema waajiri watahitaji angalau mtu aliyepata D kwenye hesabu katika mtihani wake wa O-level, katika hali halisi mtu aliyepata D O-level hawezi kuwa anajua Calculus na mahesabu mengine magumu magumu kama vector space, na majometri ya ajabu ajabu sana sana atakuwa anajua tu hesabu basic na milinganyo rahisi rahisi yenye single variable pamoja na hesabu zingine za Magazijuto na vijometri ya kutafuta maeneo pamoja na mizingo kitu ambacho utaweza kukitumia kujua hata ukitaka kujenga tank lako la maji lenye ujazo wa lita elfu ishirini basi liwe na vipimo gani, sasa mkuu wangu unataka tuwe na kizazi ambacho hata ukimwambia akufanyie tathmini ya tofali utakazotumia kujenga kibanda cha bati 30 anaanza kushangaa hata hajui aanzie wapi.

Tafadhali mkuu tunataka angalau basi watu waliopata D sio lazima wenye kujua mahesabu magumu ambayo mengi yanatumika kwenye engineering design.

Kuna sababu nyingi kwanini mtu anapata D. Kwanza waalimu wabovu. Pili upatikanaji wa material. Tatu mazingira. Nne jinsi ya utungaji wa mitihani. Mitihani ya Tanzania ina-cover elimu yote ya miaka minne. Kuna watu hawana memory za kukumbuka.
 
Gaijin:

Now we converge. Nyumbani ulikuwa unafundishwa kwa kutumia mifano ya dunia yako ya ufahamu, so your home instructor was cultivating your ability to think critically naturally.

We, on the other hand, who attended public schools didn't have that luxury and we are punished for that. I am punished because I failed to answer a simultaneous equation. However, in book keeping, counting money, construction of simple building etc and in our daily lives we don't use simultaneous equations or her cousin quadratic. So why is that a big deal?

Please refer the dialog below between the great philosopher Socrates and a slave boy.
Halving a square

Kwanza unakuwa punished kwa kuwa Mtanzania. Hiyo suluba lazima kila mmoja wetu imshukie.

Kimsingi ni kuwa mfumo wetu wa elimu haukidhi haja hata kidogo. Tunasomeshwa darasani ili tusogee vidato tu, lakini sio kuwa elimu ile ituongezee maarifa. Na hii sio kwenye somo la hisabati peke yake.

Mtu anafikia kumaliza form 6, hajui hata karatasi inaweza kutengenezwa vipi kwa kutumia materials zilizomzunguka kwa sababu haipo kwenye mtaala, walimu si wabunifu, na hakuna hata vitabu ambavyo mtu anaweza kujisomea mwenyewe ili kuongeza maarifa yake yeye mwenyewe.

Tunatengeneza jamii ya watu wanaotegemea natural instincts pekee katika maamuzi yao hata kwa waliosoma na kumaliza vidato vyote. Ni hatari sana.
 
Ni kwamba ukisoma na kufaulu somo la Siasa inakuwa ni vyema sana maana utawadanganya na kuwanyonya wana sayansi, wana mahesabu, wanasheria madakitari na hata wachumi!.

Mie nashauri watoto wetu wawe wanasiasa. Siasa is everything.
 
Naomba kusahihishwa kama nakosea, nimejaribu kuupitia tena huu uzi na nachokiona katika hoja za wengi ni majadiliano katika "mfumo mbovu" wa elimu katika Taifa letu, mfumo usiomsaidia au kumjenga mwanafunzi katika kufikiri, mfumo usioshabihiana na mazingira yetu na labla jingine ambalo halijajadiliwa sana ni nafasi ya lugha katika kutoa hiyo elimu.

Kama hayo ni sahihi then ndio sababu ya hesabu kuwa "nightmare" kwa watanzania wengi.
 
Nchi zote za ulaya zilikuwa zinajifunza kwa kutumia kilatini. Na kama wangeendelea kutumia lugha sijuhi kama wangeweza kufika walipo sasa.

Tatizo hatujahamua kuwa tunaweza kuwa na maarifa katika lugha zetu.
 
Pamoja na ugumu wa hisabati, kuijua kuna raha zake. Kuna masomo mawili ya msingi; hisabati na kiingereza. Masomo mengine huchipuka na kumea kutokana na hayo mawili
 
Ndo maana kuna post yako moja umesema waajiri watahitaji angalau mtu aliyepata D kwenye hesabu katika mtihani wake wa O-level, katika hali halisi mtu aliyepata D O-level hawezi kuwa anajua Calculus na mahesabu mengine magumu magumu kama vector space, na majometri ya ajabu ajabu sana sana atakuwa anajua tu hesabu basic na milinganyo rahisi rahisi yenye single variable pamoja na hesabu zingine za Magazijuto na vijometri ya kutafuta maeneo pamoja na mizingo kitu ambacho utaweza kukitumia kujua hata ukitaka kujenga tank lako la maji lenye ujazo wa lita elfu ishirini basi liwe na vipimo gani, sasa mkuu wangu unataka tuwe na kizazi ambacho hata ukimwambia akufanyie tathmini ya tofali utakazotumia kujenga kibanda cha bati 30 anaanza kushangaa hata hajui aanzie wapi.

Tafadhali mkuu tunataka angalau basi watu waliopata D sio lazima wenye kujua mahesabu magumu ambayo mengi yanatumika kwenye engineering design.

Masuke. Hiki unachokisema ndio ninachokililia, kwa syslabus ya hisabati ambayo tunapitishwa at the end of the day tunashindwa hata kufocus kwenye key mathematics ambazo in fact tunazihitaji kwenye maisha yetu kama ulivyozitaja kwa ufupi. ukiwauliza watoto wa form two ni hesabu gani zinawapa changamoto watakuambia Logarithm, wa form three watakuambia cycle na function etc. hizi zinawakeep so busy kiasi kwamba wanashindwa hata kupata concentration ya kuwawezesha kumaster hesabu kama magazijuto na milinganyo.

Better kama zingepewa weight basi, kwamba Mtu anatakiwa apate zaidi ya asilimia 60 ya hesabu za magazitujo,milinganyo,metrics na zingine ambazo zinahitajika kwenye maisha ya kawaida ya binaadamu alafu hizo zingine zifundishwe katika misingi ya introduction pending for detailed training in professional educations.

Ukifuatilia hao wanaopata D kwenye mathematics za o-level hata ukiwapa hesabu za mayagazito utazimia kuujua ukweli, kama unataka tafuta mwanasheria mmoja tu pale mahakama ku umpe hesabu ya mayagazito kama hautajuta kumfahamu.
 
Nchi zote za ulaya zilikuwa zinajifunza kwa kutumia kilatini. Na kama wangeendelea kutumia lugha sijuhi kama wangeweza kufika walipo sasa.

Tatizo hatujahamua kuwa tunaweza kuwa na maarifa katika lugha zetu.

Zakumi
Hizi mambo za kufikiria kwamba tunaweza tukafanya any break through kwa kutumia lugha yetu huwa sielewi misingi yake ni nini? kwamba tufundishe Physics au Biliogia au chemistry kwa Kiswahili? Haiwezekani, kama tunataka kufanya hivyo basi tuhakikishe kwamba tumejiandaa na tuwe na dhamira ya dhati ya kufanya utafiti, ama sivyo hauwezi kufundisha kwa lugha yako mambo ambayo haujayagundua wewe.
 
bado nasisitiza ni kutokujua ndio kunasababisha hatuipi kipaumbele falsafa katika maisha yetu ya kila siku. angalia mfn ufuatao,
matatizo ya kijamii - yanapelekea critical thinking - inapelekea application of different solns mojawapo ni hesabu halafu suluhu ya matatizo.

hapa unafikiri kipi ni muhimu kusisitizwa kufundishwa, critical thinking ndyo inayoleta hesabu kutumika if necessary.
haya ni mawazo yangu.

Iron Lady
Unaweza ukashare na mimi critical thinking process inayotumiwa na any of our government organ katika kukabiliana na mpasuko wa kijamii katika misingi ya kidini unaoendelea nchini mwetu hivi sasa? unaweza ukaanzia pale Kikwete alipotamka Bungeni kwamba uchaguzi mkuu wa 2010 uligubikwa na udini.

ukiweza ukanionyesha na some mathematics involved nitashukuru zaidi.

Ukishindwa tafuta tatizo lolote linalotukabili la kijamii alafu ulitumie kama mfano. karibu.
 
Zakumi
Hizi mambo za kufikiria kwamba tunaweza tukafanya any break through kwa kutumia lugha yetu huwa sielewi misingi yake ni nini? kwamba tufundishe Physics au Biliogia au chemistry kwa Kiswahili? Haiwezekani, kama tunataka kufanya hivyo basi tuhakikishe kwamba tumejiandaa na tuwe na dhamira ya dhati ya kufanya utafiti, ama sivyo hauwezi kufundisha kwa lugha yako mambo ambayo haujayagundua wewe.

Nani kasema haiwezekani? Mbona wengine wanaweza? Wachina,wajapan, wajeruman, waspain na wengine wengi tu, infact haya tunayofundishwa kwa kiingereza who told u that they were invented by britons? Hesabu, sayansi, philosophy, literature, n.k yalianzia kwa ancient Egyptians na yakapata mwendelezo mzuri na wagiriki, mbona lugha za ancient egyptian au hellenic hatuzioni zikitumika kufundishia vitu walivyogundua wao?
Your argument is fallacious Mkuu!
 
Sielewi focus yetu ni nini? sababu kama unakubali kwamba wajerumani, waegypt,wagiriki nk wamefanya inventions na lugha zao hazitumiki kufundishia ntakuuliza why would you want to use your own language then?

why exactly do we want to use swahili in teaching? what do we want to achieve? want to do it for fun?, then, were the egyptian invention made in briton or american? au wagiriki did they use english?

Ndio maana nasema vitu ambavyo haujavindua wewe unalazimika kutumia lugha za wagunduzi kufundishia, unaweza ukasema kama ni hivyo kwa nini hatutumii lugha za kigiriki kufundishia mambo yaliyogunduliwa na wagiriki, the answer is simple. who has put our education system in place? ama sivyo pia zipo evidence nyingi tu kwamba kwa yaliyogunduliwa na wagiriki hata waingereza wanafundisha kwa kigiriki.

au tujadiri why english is a world language?
 
Si lazima uwe na mwalimu mzuri katika kila stage. Kwa nchi kama Tanzania or for that matter, any other African country, itabidi uchukuwe wajanja wote wakafundishe.

Katika makuzi ya mtoto kuna critical period ambacho mtoto au mwanafunzi anatakiwa awe na watu makini wa kumfundisha. Katika kipindi hicho, wanafunzi wengi wa Tanzania wanakuwa wanasahauliwa.
what stages are those? for a man to develop into his full potential he has to go through proper guidance throughout his life.
 
Sielewi focus yetu ni nini? sababu kama unakubali kwamba wajerumani, waegypt,wagiriki nk wamefanya inventions na lugha zao hazitumiki kufundishia ntakuuliza why would you want to use your own language then?

why exactly do we want to use swahili in teaching? what do we want to achieve? want to do it for fun?, then, were the egyptian invention made in briton or american? au wagiriki did they use english?

Ndio maana nasema vitu ambavyo haujavindua wewe unalazimika kutumia lugha za wagunduzi kufundishia, unaweza ukasema kama ni hivyo kwa nini hatutumii lugha za kigiriki kufundishia mambo yaliyogunduliwa na wagiriki, the answer is simple. who has put our education system in place? ama sivyo pia zipo evidence nyingi tu kwamba kwa yaliyogunduliwa na wagiriki hata waingereza wanafundisha kwa kigiriki.

au tujadiri why english is a world language?

Mkuu Sangarara.
Its possible kutumia lugha yoyote ile kufundishia as long as hiyo lugha inakamata kisawasawa mawazo ya hao watu. Nimekupe mfano rahisi tu, mtu akiwa kazama ndani ya mawazo,labla kapata matatizo makubwa, au yuko in deep thinking akitafuta solution au uvumbuzi wa kitu fulani, lugha inayoweza kukamata mawazo yake ndio lugha inayofaa kutumika kumpa elimu mtu huyo.

Sasa kwenye jamii yetu ni lugha gani inayoweza to serve that purpose? Is it english? Ni wangapi wanakijua vizuri kiingereza? Kinafundishwaje huko mashuleni kwetu? Waalimu wanaokifundisha wanakijua vizuri? Wangapi can access and afford english medium schools? Chukua mfano wa "elites" kama wabunge wetu,wanakijua vizuri kiingereza? Kama kwao nacho ni "nightmare" kwa wananchi wa kawaida na walalahoi inakuaje?

Am not against english whatsoever, ila nna wasiwasi na uelewa wa watu(majority) juu ya hii lugha na matumizi yake katika elimu. Ndio maana unachoita "nightmare" hakipo kwenye hesabu tu, english ni "nightmare", masomo ya sayansi ni "nightmare" na tutaendelea kuzalisha a lot of "nightmares" in the near future!
 
Back
Top Bottom