Hilo la leo limeniuma sana

Hilo la leo limeniuma sana

Joined
Oct 27, 2024
Posts
33
Reaction score
277
Leo asubuhi nilipeleka maombi ya kazi katika moja ya shule hapa mjini. Lakini uzoefu niliokutana nao leo ulikuwa mbaya sana.

Picha inaanza nilipofika getini, nikamsalimia mlinzi, mwanaume mwenye umri unaokadiriwa kuwa zaidi ya miaka 44. Nikamwambia naomba anielekeze ofisi ya mkuu wa shule. Mlinzi yule akaniambia kuwa bosi anaongea kwa simu, hivyo anipe CV zangu ili atampatie akimaliza. Nikamuomba kuwa nipo tayari kumsubiri mkuu hadi atakapomaliza kuongea kwa simu, lakini mlinzi akakataa.

Nilimsihi sana mlinzi yule angalau anipe dakika tano, lakini bado alikataa. Nikamuomba basi aniruhusu nipeleke bahasha hiyo kwa sekretari wa mkuu wa shule, naye akakataa. Nikaona sina jinsi, hivyo nikampa mlinzi bahasha yangu.

Cha kushangaza, mlinzi yule akaifungua bahasha na kuanza kusoma barua ya maombi na CV zangu. Nilihisi huzuni sana kiasi cha machozi kunilengalenga. Nikaona labda haikuwa bahati yangu kufanya kazi katika taasisi hiyo.
 
Leo majira ya asubuhi nilipeleka maombi ya kazi katika moja ya shule hapa mjini.
Lakini experience nimeyokutana nayo Leo it's was too bad.
Picha inaanza Nimefika getini, nikamsalimia mlinzi jinsia yake me anaonekana kama ana miaka 44+ . Nikamwambia naomba unielekeze ofisi ya mkuu wa shule.
Mlinzi yule akanambia boss anaongea na simu, kwa hiyo nipe CV zako akimaliza tampa. Nikamuomba kuwa nipo Tayari kumsubilia mkuu hadi atakao maliza kuongea na simu jamaa akagoma.
Ndipo nikamsihi sana yule mlinzi kuwa anape hata dakika tano tu, lakini jamaa yule alikataa.
Nikamuomba kaka Tafadhali naomba basi bahasha hii nimpelekee sekretari wa mkuu wa shule jamaa akagoma.
Nikaona sina jinsi, nikachukua bahasha nikampa mlinzi, jambo la ajabu jamaa akafungua bahasha akaanza kusoma application letter na CV zangu, aisse I was to excited kiasi kwamba machozi yalinilenga.
Nikaona maybe labda sio neema yangu kufanya Kazi kwenye tasisi hiyo.
Siku nyingine ukifika kwa mlinzi mwambie ninahitaji kuonana na mkuu pasipo kumwambia kwa shida gani. Akikomaa sana kutaka kujua unakwenda kufanya nini, mwambie nakwenda kutafuta nafasi ya kumhamisha mwanangu asome katika shule hiyo.
 
Leo majira ya asubuhi nilipeleka maombi ya kazi katika moja ya shule hapa mjini.
Lakini experience nimeyokutana nayo Leo it's was too bad.
Picha inaanza Nimefika getini, nikamsalimia mlinzi jinsia yake me anaonekana kama ana miaka 44+ . Nikamwambia naomba unielekeze ofisi ya mkuu wa shule.
Mlinzi yule akanambia boss anaongea na simu, kwa hiyo nipe CV zako akimaliza tampa. Nikamuomba kuwa nipo Tayari kumsubilia mkuu hadi atakao maliza kuongea na simu jamaa akagoma.
Ndipo nikamsihi sana yule mlinzi kuwa anape hata dakika tano tu, lakini jamaa yule alikataa.
Nikamuomba kaka Tafadhali naomba basi bahasha hii nimpelekee sekretari wa mkuu wa shule jamaa akagoma.
Nikaona sina jinsi, nikachukua bahasha nikampa mlinzi, jambo la ajabu jamaa akafungua bahasha akaanza kusoma application letter na CV zangu, aisse I was to excited kiasi kwamba machozi yalinilenga.
Nikaona maybe labda sio neema yangu kufanya Kazi kwenye tasisi hiyo.
Pole sana mkuu, kuna walinzi ni ovyo sana.
 
walikujaribu tu na kupima kiwango chako cha hekima, busara, ustaarabu, ustahimilivu na subra..

kiukweli hiyo kazi utapata au utakosa kwa namna ulivyokua unareact hapo ofisini pa watu.

na kupitia CCTV camera 📷 mkuu wa shule alikua anakucheki ulivyokua ukizungumza na mlinzi ambae na ni mwalimu na mfanyakazi wa shule hiyo.

Next time, be careful and take note 🐒
 
Kwani kuna shida gani kumpa mlinzi akupelekee hiyo.barua.

Au akiisoma kuna tatizo gani? Unahisi wanaofanya kazi za kulinda wote hawajasoma?

Huyo sasa ndiyo alikuwa mtu wa kuyajenga naye vizuri.

Kwenye maeneo ya private wengi wanapata nafasi kwa connections.

Na hapo ukipata nafasi mshahara utakuja kuambiwa laki 3.

Jikaze mtoto wa kiume.

Tatizo kizazi cha sasa mmelelewa kinyanya nyanya sana.

BTW karibu sana mtaani, huo ndiyo mtaa sasa, ya darasani yaache hukohukoo..
 
Kaka mimi nishaachaga kabisa huu upuuzi wakusambaza Cv. Niko kitaa najikaBili mdo mdo kuajiriwa no way
 
Back
Top Bottom