Hili ni jaribio jingine kwa System/state au Kitengo!

Hili ni jaribio jingine kwa System/state au Kitengo!

Eti system ndio inaleta amani,tena system ndio juu ya kila kitu,MAWAZO MADOGO KABISA


ukiona nchi yeyote duniani hakuna amani , kwa maana kuna machafuko, vita, na vurugu za kila aina ujue system iko nyoronyoro sie waafrika wenzetu wanatushangaa kwanini wakati wa uchaguzi hata hatudundani hapo ujue system iko kazini kutwa kucha, heko kwa system iendelee hivyo hivyo
 
Man at work

Heko kwao ila watende Haki sio kukandamiza wengine sana angalau kidogo.

Waneteleza hapa Gwajima vs Ponda

Wabane na kuachia.
 
Amen and amen!

Niliwahi kuandika.... Watanzania wazalendo watajikuta wamejikusanya pamoja bila kujua nani kawakusanya na kwa jinsi gani..... Once again fisadi yeyote hata kaa akatize miguu yake kwenda kwenye jumba letu takatifu.... Its done just wait and see!

Not by power or mighty but through the holly spirit.

Kila roho yenye dhambi itakufa, asemama Bwana wa majeshi; Ambaye Ame aona fahari kuitwa mtumishi wake.

Glory, honor, power and majesty belong to my Lord and saviour Jesus!

Hii nchi inalindwa na matambiko aliyofanya Nyerere, hakuna cha Yesu wala mfano wake... Tunalindwa na Mizimu yetu iliyo hai!
 
System inabadilika. JPM ni sehemu ya system mpya iliyo penyezwa na sasa inawashughulikia. Nyinyi mnasema system, chezea watu nyie. Hili nililiona na nikajua laja.
 
ukiona nchi yeyote duniani hakuna amani , kwa maana kuna machafuko, vita, na vurugu za kila aina ujue system iko nyoronyoro sie waafrika wenzetu wanatushangaa kwanini wakati wa uchaguzi hata hatudundani hapo ujue system iko kazini kutwa kucha, heko kwa system iendelee hivyo hivyo

Ingekua iko vizuri tusingefika hapa tulipo after fifty years of independence. Labda kulinda chama iko vzuri.
 
System ni muunganiko wa organs mbalimbali zinazofanya kazi moja hili ni somo la darasa la saba au form one!

System/Mfumo hufanya jukumu moja na hulifanya vizuri kwa saabu za ubobezi. Mfumo hatumii nguvu mambo huenda kiulaini na kwa ubora wa hali ya juu. Muunganiko wa sehemu/parts mbali mbali huitwa mifumo/sstems ambayo kila sehemu imebobea kaika eneo lake.
 
System inahitaji kupangwa mkuu, iliyopo imepalaganyishwa na nyie wenyewe kwa siasa za kishetani na za kitoto, mbaya zaidi kwa maslahi yenu. Sasa utusaidie ipangwe vizuri na i-serve interest za Taifa, ili twiga wasikwee Boeing 777, tembo wasionje dhahma ya AK 47, vijana wasijidunge heroine, makontena yasigeuke sisimizi, HSC isifirisike mwisho mwa term ya uongozi, TANESCO wasilipe matajiri kwa maagizo ya system, mengine unayajua. Mwacheni atengeneze yake yenye maslahi kwa nchi.
 
Hii nchi inalindwa na matambiko aliyofanya Nyerere, hakuna cha Yesu wala mfano wake... Tunalindwa na Mizimu yetu iliyo hai!

Ndio maana tunafail sehemu nyingine but ninaamini kunawatu wanapambana kubafilisha hiyo mzimu coz hivi vizazi hakuna anayejua hayo matambiko na yanazidi kuitesa nchi kuna haja ya kuyakataa kila mtu kwa dini yake.
 
Ingekua iko vizuri tusingefika hapa tulipo after fifty years of independence. Labda kulinda chama iko vzuri.

Wakati mmemiliki system hatukujua kuwa mlikubaliana kutawanyika nchini ili kutuibia.

Hatukujua kuwa mlikubaliana kuwa mbadilishe Sir names zenu ili mchukue nafasi zetu za ajira.

Hatukujua kuwa mliwatuma dada zenu ili waolewe na kaka zetu waliisoma kwa lengo la kutuibia.

Hatukujua kuwa ninyi ndo mlikubaliana kupandisha bei za bidhaa ili mtuibie.
 
Mimi ni muunini wa kinachoitwa SYSTEM AU STATE AU KITENGO.

Ninaamini nchi hii kama zilivyo nyingine nyingi zina MFUMO AU SYSTEM na kazi yake ni moja tu kulinda maslahi ya nchi dhidi ya majaribio ovu kutoka ndani na nje ya mipaka yetu.

Ni 'system' pekee ndio inatufanya tuishi kwa amani hata kama ni kidogo!


System hailali wala kusinzia!

System inaachia uhuru wa kutosha sana mpaka pale ulevi wa uhuru unapoanza ndipo system inaingilia kati !

Sitaki kuongelea mengi pengine siyajui sana!

Naamini ni kazi ya kawaida kabisa ya System kuendelea kujilinda na kulinda values za kitanzania ili kuifanya Tanzania iendelee kuitwa Tanzania!

Hakuna aliye juu ya system awe masikini,kilema au tajiri au gaidi.ni system pekee ndio Alpha na Omega!

Mwaka 1992,1995,2010,2013 na labda miaka ya nyuma zaidi nikiwa mdogo SYSTEM ilipitia majaribio makubwa kadhaa na ikayashinda na sasa ni jaribio jingine tena ndani ya mwaka huu 2015.

Kwa hekima ya kipekee naamini system itashinda kiurahisi kuliko kila mmoja wetu anavyotarajia kwa kuwa ili-anticipate na hivyo imejipanga vilivyo.

KILA LA KHERI KWA SYSTEM KATIKA KUENDELEZA MAJUKUMU YAKE!

#Heshimakwakitengo

nchi inamifumo mingi isiyoweza kufanya kazi pamoja kwa ufanisi, tra na bandari ni mfano.
mifumo mibovu kila sehemu mpaka ndani ya vyama, serikalini huko ndio usiseme ni Zaidi ya hatari kitu kidogo kama dawa kinashindwa kuthibitika.

mifumo hii kwa ujumla inabidi kurekebishwa kabla haijadondoka kwa hasara ya nchi
 
ingekua iko vizuri tusingefika hapa tulipo after fifty years of independence. Labda kulinda chama iko vzuri.

dada yangu ulishawahi fika jamhuri ya afrika ya kati hivi karibuni? Ulishawahi fika burma ya kipindi cha leave for nothing or die with something? Ulishawahi fika sarajevo miaka ya 1998?

Ukishanijibu haya majibu nitakuuliza kwanini nimekuuliza hivyo unless hoja yangu hujaielewa
 
Ingekua aibu kama mafisadi wangeachwa kujipenyeza ikulu, kwa bahati nzuri, halikutokea janga kwa taifa letu.
 
dada yangu ulishawahi fika jamhuri ya afrika ya kati hivi karibuni? Ulishawahi fika burma ya kipindi cha leave for nothing or die with something? Ulishawahi fika sarajevo miaka ya 1998?

Ukishanijibu haya majibu nitakuuliza kwanini nimekuuliza hivyo unless hoja yangu hujaielewa

Poti! Kuna watu wana dalili za shibe, Watanzania wameshiba maisha mazuri, wanasingizia Serikali as if walifanya biashara wakakatazwa, watu wanalalamika shida wakati kila wikiendi wanabeua na kigodoro mara nne kwa mwaka, najiuliza hawaoni hata wageni wanavyokimbilia kwetu na wakakaa bila kokoro?
Naamini system imeshinda jaribu kubwa kabisa, kwa hisani ya tambiko la Nyerere ambako bado tunasafiri nalo.
Ukiona wazee kama Salim na Sinde wameacha yao wakaja kwenye kampeni ujue ni mpango wa miungu!
 
Back
Top Bottom