Hili la uhaba wa Vyumba vya Madarasa linaonesha namna Serikali yetu ilivyojaa Uzembe na Ubabaishaji

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,332
2,000
Leo Waziri wa TAMISEMI ametangaza matokeo ya vijana waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza, ambapo zaidi ya wanafunzi 74,000 wamekosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Jambo hili linasikitisha na kuhuzunisha sana maana sasa limekuwa wimbo wa taifa, kila wamalizapo wanafunzi ni lazima wengine wabaki kutokana na uhaba wa Vyumba vya Madarasa, hii inadhihirisha namna serikali ilivyojaa ubabaishaji na uzembe.

Hivi serikali inashindwa kuandaa vyumba vya kutosha mapema ili wanafunzi hawa wajiunge kwa pamoja pasipo kuwasubirisha, hivi kama tatizo dogo kama hili limewashinda wataweza yale makubwa kweli?

Hili linatia aibu na kuonesha namna tusivyokuwa makini na elimu ya watoto wetu.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Serikali utopolo huwa ina mipango utopolo. Hao wanafunzi wanao kwa miaka 7 kwann haikujipanga?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom