SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,244
- 4,258
Kuna hili neno watu wanalitumia sana. Hata kuna kampuni moja ya vinywaji baridi walilitumia sana hili neno, mimi nikabaki na mshangao. Hata hapa JF linatumika sana.Neno hilo ni 'kuboa' na 'kuboreka'.
Mtu akichoshwa na kitu anasema: Hiki kitu kimeniboa sana au anasema: Nimeboreka ile mbaya.
Kwa muda mrefu nimewaza kwamba neno hili ni la kiingereza 'to bore' na hatuna haja ya kulitumia kwa sababu tunalo la kiswahili: kuchosha'.
Kwa nini tuombe maji kwa jirani aliye mbaaaali ilhali bomba letu linatoa maji?