Hiki ni Kiswahili cha wapi? Binafsi Sikikubali!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,257
Kuna hili neno watu wanalitumia sana. Hata kuna kampuni moja ya vinywaji baridi walilitumia sana hili neno, mimi nikabaki na mshangao. Hata hapa JF linatumika sana.Neno hilo ni 'kuboa' na 'kuboreka'.

Mtu akichoshwa na kitu anasema: Hiki kitu kimeniboa sana au anasema: Nimeboreka ile mbaya.
Kwa muda mrefu nimewaza kwamba neno hili ni la kiingereza 'to bore' na hatuna haja ya kulitumia kwa sababu tunalo la kiswahili: kuchosha'.

Kwa nini tuombe maji kwa jirani aliye mbaaaali ilhali bomba letu linatoa maji?
 
Kwa nini tuombe maji kwa jirani aliye mbaaaali ilhali bomba letu linatoa maji?

is the water clean and pure?[/QUOTE]
Don't take the water analogy literally Fasouls! What I meant was:If we have our own word, why don't we use it?
 
Last edited by a moderator:
who cares its just a small staff dude ,kuanzishia thread
 
Ni kweli neno chosha linaweza kutumika lakini halikidhi maana inayotakiwa hapa. Kitu kikikuchosha maana yake mwanzo kilikuwa sawa na hakina shida ila baada ya muda kikakuchosha. Likini mfano mechi inaweza kuanza tu na ikawa haivutii hivyo ikawa "inaboa". Neno "bore" linahusisha kukinai, kutobrudisha na kutokuwa na kitu kipya ndani yake. Kwa hiyo bado nini halikidhi.
 
Kwanza tuondoe mitazamo ya kwamba heti lugha ya Kiswahili haikidhi haja kutokana na kuwa na misamiati michache. Halafu 'kuchocha' ni neno linaloweza kutumika kuwa mbadala wa hilo neno la kiingereza,kwa maana kinachoangaliwa katika mazungumzo ni dhana gani inalengwa wakati huo,. Lakin sisi wenye lugha yetu kwanza tumekuwa wavivu wa kutafuta miamiati mipya kutokana na kujenga mitazamo mibovu katika lugha yetu. Pia tukumbuke katika kuunda misamiati ya lugha kuchukua misamiati kutoka katika lugha nyingine kunaruhusiwa ilimradi tu dhana lengwa iwe sahihi. Hata hicho kiingereza kinachoonekana kuwa ni lugha bora,mbona kina misamiati mingi inayotoka katika lugha zingine.?
KISWAHILI NDIO LUGHA TAMU NA ADHIMU DUNIANI KOTE.
 
Mkataa kwao ni mtumwa; Mtanzania hata azungumze Kiingereza kwa ufundi kiasi gani atabaki kuwa mtanzania/mswahili. Ni vizuri kutunza ulicho nacho; "Usiteme jojo kwa karanga za kuonjeshwa" Usiache mbachao kwa msala upitao.
Kwanza tuondoe mitazamo ya kwamba heti lugha ya Kiswahili haikidhi haja kutokana na kuwa na misamiati michache. Halafu 'kuchocha' ni neno linaloweza kutumika kuwa mbadala wa hilo neno la kiingereza,kwa maana kinachoangaliwa katika mazungumzo ni dhana gani inalengwa wakati huo,. Lakin sisi wenye lugha yetu kwanza tumekuwa wavivu wa kutafuta miamiati mipya kutokana na kujenga mitazamo mibovu katika lugha yetu. Pia tukumbuke katika kuunda misamiati ya lugha kuchukua misamiati kutoka katika lugha nyingine kunaruhusiwa ilimradi tu dhana lengwa iwe sahihi. Hata hicho kiingereza kinachoonekana kuwa ni lugha bora,mbona kina misamiati mingi inayotoka katika lugha zingine.?
KISWAHILI NDIO LUGHA TAMU NA ADHIMU DUNIANI KOTE.
 
Swaga ndiyo maana hadi leo tumeshindwa kusema "BILAURI"Tukaishia kusema "GLASS"
 
hiyo ni athari ya kuchanganya lugha na zaidi ni ukoloni uliomo vichwani mwetu hasa pale tunapodhani kuwa kuongea kiingereza ni kuwa maarufu na muelewa...la hasha! kumbe ni upofu! ila neno 'kuboreka' ni la kiswahili liki nyambulishawa au kuambishwa kutoka 'bora'- kitu imara na kizuri chenye kukidhi haja na mahitaji ya matumizi, na kipendezacho
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom