Nakukunda
JF-Expert Member
- Jul 10, 2017
- 875
- 1,647
Very TrueSiku zote mnashauriwa mkapime hospital ili kuepuka mambo kama haya, kwa maelezo na picha uliyoweka umefanya makosa mengi sana, nitaeleza kwa kifupi ;
1. Hukutumia micro pipette ili kupata kiasi cha damu kinachohitajika, ndio maana eneo la kuweka sample limetapakaa damu
2. Nina wasiwasi kama ulitumia special buffer solution au maji ya kawaida, batch number ya test kit ni lazima ifanane na iliyopo kwenye buffer solution, kinyume na hapo kunayafanya majibu yawe invalid
3. Hukujali kabisa muda unaostahili kusubiri kabla ya kusoma majibu
4. Ufahamu wako kuhusu hiki kipimo ni Mdogo ndio maana umeshindwa kutafsiri majibu
Makosa niliyo ainisha hapo juu yanafanya majibu hayo yawe batili
Tujitahidi kuheshimu taratibu zilizowekwa kwenye mambo ya msingi.
sent from my Sony Xperia using jamii forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app