Hiki chama ni cha kidini?

Hiki chama ni cha kidini?

Ndugu, lazima utakuwa na tatizo la akili. Kama ungekuwa na akili timamu lazima ungekujua kuwa hapa Tanzania hakuna chama kinachoungwa mkono au kukataliwa na dini moja.

Kuna wachungaji, manabii, maaskofu na kuna mashekhe pia wanaoimba wimbo wa CCM, 'tulinde amani' (ie hata kama hakuna haki). Kwa uchache, umesikia tamko la Malasusa na shekhe mkuu wa BAKWATA, wakiimba huo wimbo.

Lakini wapo viongozi wa dini, maaskofu, wachungaji, manabii, mashekhe, wanaungana na watanzania walio wengi kuwa huwezi kuongelea Amani, bila kuongrlea HAKI. Hawa wanaungana na wananchi wengi wenye akili timamu, wasio wanafiki, wanaoipenda nchi yao, wanaoona wazi kuwa mifumo yetu ya udhulumaji haki iliyotamalaki kwenye nchi hii, ni tishio kwa amani yetu, tukitaka amani ya kweli ni lazima tufanyie maboresho ya sheria na mifumo inayotengeneza mazingira ya kuwadhumuru wananchi. SHURA YA MAIMAMU, TEC, Maaskofu, wachungaji, manabii na mashekhe, mmoja mmoja wamesimama kwenye msingi huu.

Na hakika, yeyote ambaye hataki kurekebisha na kubora mifumo yetu ambayo ni ya kuwadhulumu wananchi mamalaka yao, ni mashetani na maibilisi wakubwa.

Nchi inataka haki, haitaki kuendelea na ushetani unaofurahiwa na tale maibilisi ya CCM.
Yaani nisiwe na akili ajili ya kuuliza tu kama chadema ni chama cha kidini?
Mbona mnaweweseka hivyo? Jibuni swali ni chama cha kidini?
 
Hao waislam wako wapi! Mbona kwenye huu uzi wako, hata CHAWA tu wasiojua kutofautisha kati kizuri na kibaya; wameshindwa kukuunga mkono.

Kwa hiyo wewe endelea tu kufurahisha genge. Nikiendelea kubishana na mjinga, nitaonekana na mimi ni mjinga kama wewe tu.
Zimekuwa mbili
 
Palikuwa na tume pale ya uchaguzi?
Walishindana na chama gani?
CHADEMA bado haijachukua Dola lakini Uchaguzi pekee ambao CHADEMA imefanya na kuusimamia ni ule wa ndani ya Chama na na ooh.. bwooy ulikuwa ni Uchaguzi HURU na HAKI na UWAZI sasa CHADEMA na sisi wananchi tunataka Tume ya Uchaguzi iwe Taasisi HURU ili iweze kusimamia Chaguzi zote bila ya kuingiliwa.
 
CHADEMA bado haijachukua Dola lakini Uchaguzi pekee ambao CHADEMA imefanya na kuusimamia ni ule wa ndani ya Chama na na ooh.. bwooy ulikuwa ni Uchaguzi HURU na HAKI na UWAZI sasa CHADEMA na sisi wananchi tunataka Tume ya Uchaguzi iwe Taasisi HURU ili iweze kusimamia Chaguzi zote bila ya kuingiliwa.
Ndio tunaenda huko step by step

Ccm ni chama makini
 
Tujikumbushe tumefikaje hapa mpaka tafadhali angalia hii clip fupi sana halafu tafakari👇
 
Kwanini matamko yao yanaungwa mkono na viongozi wa dini?

Ni either wanaanza wao kusema au kutoa tamko na halafu viongozi wa dini flani wanaunga mkono na kusisitiza au wananza viongozi wa dini flani kisha wao wanaunga mkono na kusisitiza,

Tena hao viongozi wa hicho chama wanatoa matamko ya kuamrisha serikali na wala sio kushauri au kupendekeza
Yaani ni amri tu kwanini lakin

Waungwana msifute hii, acheni tujadili tupeane faida
Naunga mkono hoja
 
Nitajibu baadhi ya hoja hapa japo upo inje ya mada yangu

Mada yangu ni swali je chama ni cha kidini au si cha kidini, ok turudi kwenye hoja yako

Ni kweli mabadiliko yanahitajika na ccm na serikali yake wanafanya hayo mabafiliko kila yanapohitajika kwa kadri ya haja ila ni hatua kwa hatua na mabadiliko ni mchakato, hayawezi kufanyika ghafka ni kdogo kidpgo na yanafanyika na tunaona,

Kuhusu vyama vingi ni likikuwa hitajio la lazima kwa kipindi kile so hata hata kama watanzania wote wangekataa au hata kama rais angekuwa ni shetani ilikua lazima mabadiliko yaje

Na hata sasa mabadiliko yatakuja tu ni suala la mdabtu

na ccm ni chama kimejichimbia sana so wapinzani wakiona njia ni kuingiza viongozi wa dini mwishowe ni kusababisha fujo kwani kila mmoja ana dini yake

Kuhusu mwalimu kusifu ushindani ule ni kwamba hata rais aliyewepo kipindi kile alikuwa muungwana na mwema akaridhika na kuendekea mbele na kushirikia na wapinzani

Taizo hili lilianzishwa na mwendazake kiasi cha kufungia hata siasa zisifanyike wakati wa uongizi wake na hakuna hata aliyeoaza sauti si vyama wala viongozi wa dini na maisha yaliendelea na harakati zilifanyika chini kwa chini na mpaka hapa tulipofika ni cvm imebadilisha mengi katika mabaya ya mwenzao aliyepita vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi

NB
Chama kile ni cha kidini au sio cha kidini?

..chama sio cha kidini.

..hoja zake zinaungwa mkono, na kupingwa, na viongozi wa dini zote kuu Tanzania.

..wakati wa Jpm wako viongozi wa vyama, na wa dini kuu za hapa Tanzania, ambao walipinga ukandamizaji uliokuwa ukiendelea. Sio kweli kwamba watu wote waliufyata, wako waliopambana.
 
..chama sio cha kidini.

..hoja zake zinaungwa mkono, na kupingwa, na viongozi wa dini zote kuu Tanzania.

..wakati wa Jpm wako viongozi wa vyama, na wa dini kuu za hapa Tanzania, ambao walipinga ukandamizaji uliokuwa ukiendelea. Sio kweli kwamba watu wote waliufyata, wako waliopambana.
Asante kwa jibu zuri, bado nakusanya maoni
 
Ukiwa na akili huru na ukaitumia vizuri utaelewa kabisa kwamba mimi nina faida kwa hicho chama kuliko mnavyodhani coz nawatahadharisha na hiyo njia mnayopitia pengine kwa makusudi au bila kujua

Kweli umesema sawa hata cuf walipitishwa humo sasa kwanini nanyi mkubali kupitishwa humo?

Ni moja katika mawili either chama ni pandikizi au viongozi ni mapandikizi
Naunga mkono hoja yako
 
Na ndio maana wakatoliki wanaunga mkono chadema?

..hata baadhi ya viongozi wa Bakwata wanaunga mkono hoja za Chadema.

..Ndio maana Katibu Mtendaji wa Bakwata, Alhaj Mruma, alisoma risala na kuiasa serikali kurekebisha kasoro zilizojitokeza ktk uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024.
 
Hivi kweli utapata haki pasipo na amani? Mimi nadhani amani kwanza kisha haki labda tukubaliane kwamba amani ipo,

Na amani kama ipo basi na haki ipo
Sema siasa ni kama mpira, kila anaefungwa hakubali na atatoa kila sababu za kweli na za uongo

Kuhusu bakwata nijuavyo ni taasisi iliyoanzishwa na serika pamoja na kanisa na ndio sio waislam wote wanaikubali

Sio kwasababu nimewasema wakristo na hicho chama mkafikiri natetea kwasababu ya uisla, no mie natetea uadilifu na amani,
Haki ije na wajibu coz hakuna haki bila wajibu na wengi wanataka haki lakini hawafanyi wajibu wao,
Mfano kila mtu anadai matibabu buee, shule bure na barabara nzuri huduma nzuri ila hakuna anaetimiza wajibu wake kwa mfani wa kulipa kodi stahiki kwa wafanyabiashara, wachuuzi pia na hakuna anaetimiza wajibu wake kwa kulinda miundo mbinu na kufichua wezi wa miundo mbinu, basi ilimradi watu wanasema na wao wanasema
Yaani oye oye wengi ni oye oye
Kinachozaa haki ni amani au kinachozaa amani ni haki

Kinachoondoa amani ni haki au kinachoondoa haki ni amani ?

Nchi gani ilipata Aman bila haki kuwepo katika nchi hiyo?

Familia gani ilipata amani bila haki kuwepo katika familia hiyo?

Ukweli unaijua Ila unaleta siasa!!!
 
Back
Top Bottom