Hii ya Wakuu wa Wilaya Kupewa Ilani ya CCM imekaaje?

Naona makonda anawaapisha kisha anawa ilani ya chama cha mapinduzi

Ivi hawa ni watumishi wa chama au serikali? Me navyojua watumishi wa serikali wangepewa katiba ya nchi na waape kuilinda sasa mbona wanapewa ilani ya chama?

Attach
37409f08d6ea617f661c268bdceacc7e.jpg
Apewe ya act AMA?
 
Wanakwensa kutimiza ilaniyachama sio yanchi
 
Mkuu wa wilaya ni mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya hivyo lazima apewe ilani ili aisimamie. Mkuu wa mkoa ni mjumbe wa kamati ya siasa ccm mkoa anakuwepo ktk vikao vya ccm
 
Naona makonda anawaapisha kisha anawa ilani ya chama cha mapinduzi

Ivi hawa ni watumishi wa chama au serikali? Me navyojua watumishi wa serikali wangepewa katiba ya nchi na waape kuilinda sasa mbona wanapewa ilani ya chama?

Attach
37409f08d6ea617f661c268bdceacc7e.jpg

Endelea kujitoa akili tu......
 
Kwani ilani za vyama madhumuni yake ni nini hasa? Kwenye hizo ilani iwe za CCM, CHADEMA, CUF etc yaliyoandikwa yanahusu malengo ya vyama kwa ajili ya kazi za ustawi wa vyama ama yanahusu kazi zitakazofanywa na vyama hivyo endapo wananchi watachagua kimojawapo na kukipa ushindi ktk uchaguzi? Zinaitwa ILANI ZA UCHAGUZI na vyama vyote vinavyogombea uongozi huwa na ilani zao za uchaguzi ambazo hutumika kama silaha ya kupatia ushindi. Chama kikishinda uchaguzi ushindi ule hutokana na wananchi kushawishika na kuvutiwa na yale yaliyonadiwa kwao kutoka kwenye ilani za uchaguzi. Kwa maana hiyo basi Chama kinachoshinda kinawajibika kutekeleza yaliyomo kwenye ilani ya chama hicho. Kwa msingi huo hakuna kosa lolote kwa CCM kuwapa watendaji wa Serkali (ya CCM) ilani ya chama hicho iwe mwongozo wa utekelezaji wa yaliyomo humo ambayo ndiyo CCM ilijinadi kwayo na kuahidi kuyafanya endapo wagombea wake watachaguliwa. Tatizo letu tumezoea kuchukulia chaguzi za uongozi wa nchi kishabiki zaidi kama ushabiki wa vilabu vya mipira bila kuelewa uzito wa uchaguzi na mambo muhimu yanayoendana na uchaguzi wa nchi kama ilani za uchaguzi za vyama vinavyogombea kuchaguliwa kuongoza nchi.
 
Kama walivyo mawaziri, wakuu wa wilaya na mikoa ni makada wazeefu. Tatizo sio lingine bali CCM
 
Inayoongoza sasa hv n ilani ya chama cha mapinduzi na kwenye ilan ndo kunaahadi alizosema kiongozi wa nchi wakati wa kampen kwahyo mwenye akili timamu awezi shangaa kwann wamepewa ilan ya ccm
 
Someni katiba serikali uunɗwa na chama kilichoshinɗa uchaguzi na hiyo serikali inaunɗwa kutekeleza ilani ya chama hicho. DCs ni watawala wa serikali ni kazi yao kuilinɗa katiba na kutekeleza ilani ya chama. Nawashauri elekezeni nguvu kushughulikia katiba mpya.
 
Kazi kubwa ya mtumishi yeyote wa serikali ni kutekeleza ilani. Hata mkuu wa majeshi ana nakala ya ilani na anatekeleza ilichosema CCM juu ya ulinzi na usalama.
 
halafu ilitekekezwaje hapo wizarani kwao? Kwa 100% ? Iliwasaidiaje watanzania kwa kipindi cha 2010- 2015? Ni aibu kulisemea siyo? Siku nyingine ukiwa na bunch of theories na ukaziapply kwa miaka kumi then ukajievaluate na kujikuta efficiency is below average unazitupilia mbali na kuja na idea mpya. Hiyo ilani yenu ilishafeli for almost 50+ years why mnaendelea kuja nazo zilezile?
Wale wakuu wa wilaya ni watendaji wa chama au umma? Kama ni wa umma, jiulize umma huo ni wa ccm pekee yao? Na kama wanakwenda na ilani ya ccm ni kwanini walipwe na serikali badala ya ccm iliyowaajiri? Usizungumzie ilani inayotekelezwa bali jadili ni nani mwajiri wao.

Kila chama wakati wa kampeni kilikua na ilani yake. Chama kilichoshinda kinaongoza kwa mujibu wa ilani yake hata wangeshinda ukawa wangeongoza kiwa mujibu wa ilani yao. Mkuu wa wilaya lazima ajue kilichomo kwenye ilani ili aitekeleze vizuri.
 
ELIMU, ELIMU,ELIMU. Watanzania wengi hasa pro CCM wapo brain-washed. Elimu yetu ni ya kukariri na sio ku-integrate mambo. Tunajiuliza what na sio how. Hakuna anayepinga kwamba watumishi wa umma (kama mimi) tunatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama cha siasa kilichoshinda (kwa bao la mkono au la). Lakini wengi pro-CCM hamjawahi kujiuliza ilani hii inatekelezwa vipi. Wengi wenu pro-CCM (around 95%) hamjui mstari unaotenganisha chama na serikali katika utumishi wa umma. Ilani ya chama tawala hutafsiriwa ndani ya mipango ya kisekta ya serikali (miundombinu, elimu, mifugo, afya, madini, kilimo, utalii nk). Namaanisha bajeti, sera na mipango ya maendeleo zinapoandaliwa huangalia ilani ya chama tawala inasema nini. Hakuna haja ya mtumishi mwandamizi wa umma kumkabidhi Hard Copy ya ilani ya chama tena hadharani. Ni umaamuma, kutokujiamini, ulevi wa madaraka, umburura na ukilaza tu. Sote tunajua DCs hawana kazi ya maana zaidi ya kuwa political post lakini bado haifai kutuelezea hilo hadharani. DCs hawana fungu la fedha la shughuli za maendeleo na huwa wanaishi kwa kudandia pesa za DEDs so kama kuwapa ilani ya chama ili watekeleze yaliyomo basi mngewapa wenye kasma (mafungu ya pesa) yaani makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa halmashauri.
 
Watu wengine bhana kila mtanzania wa vyama vyote tunaishi kwa kutumia ilani ya ccm, upende usipende unatumia ilani ya ccm na ndiyo maana wakuu wa wilaya lazima wapewe ilani inayowaongoza.
 
cha kushangaza hakuna, hata viongozi wa taasisi na wizara ambao ni wataalamu huwa wanapewa kama rejea wakati wa kuandaa mipango na utekelezaji wa majukumu ya taasisi wanazo ziongoza
 
Kila chama wakati wa kampeni kilikua na ilani yake. Chama kilichoshinda kinaongoza kwa mujibu wa ilani yake hata wangeshinda ukawa wangeongoza kiwa mujibu wa ilani yao. Mkuu wa wilaya lazima ajue kilichomo kwenye ilani ili aitekeleze vizuri.
sijui unakielewa tunachokijadili hapa? Ule wakati wa chama kwanza nchi baadae ulishapitwa. Mkuu wa wilaya au mkoa uchama wake sio wa muhimu na ndio maana uteuzi wao haukuzingatia ukada kama ulivyozooleka hapo nyuma. Isitoshe huyu makonda mara nyingi anakwenda against na mkulu. Vitu anavyofikiri vitamwiinua vitamtagaragaza siku siyo nyingi. Mbona wakuu wengine hawakuwapa ilani za chama? Hata pale ikulu mbona hatukuona yeyote akipewa ilani ya chama? Maendeleo ya nchi hayaletwi kwa itikadi za ccm.
 
Wa serikali. Na nenda ofisi zote za serikali wanazo, maana ndo zenye dira ya taifa kwa nchi zetu. Kipindi cha kampeni waaliahidi kilichopo kwenye Ilan yao na ndo wanatekeleza.

Kwa ujumla huwezi kutekeleza ahadi zilizotolewa na CCM bila kuijua. Na ndo msingi wa utekelezaji kwa miaka hii mpaka 2020.

Tusione wivu, hata UKAWA ungeshinda tungekuwa tunatumia ile ya UKAWA ingawa jamaa alikuwa anatuangusha nayo.
swali la msingi ni je mkuu wa wilaya ni mtumishi wa uma au wa chama?
 
sijui unakielewa tunachokijadili hapa? Ule wakati wa chama kwanza nchi baadae ulishapitwa. Mkuu wa wilaya au mkoa uchama wake sio wa muhimu na ndio maana uteuzi wao haukuzingatia ukada kama ulivyozooleka hapo nyuma. Isitoshe huyu makonda mara nyingi anakwenda against na mkulu. Vitu anavyofikiri vitamwiinua vitamtagaragaza siku siyo nyingi. Mbona wakuu wengine hawakuwapa ilani za chama? Hata pale ikulu mbona hatukuona yeyote akipewa ilani ya chama? Maendeleo ya nchi hayaletwi kwa itikadi za ccm.

Aliyewateua mwenyewe aliwaambia kua wakatekeleze ilani ya chama(rejea hotuba ya raisi ikulu baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa watatu). Utasemaje kua uchama wake sio muhimu wakati ni mlezi wa chama katika ngazi ya mkoa/wilaya. Huwezi kumtenhanisha mkuu wa mkoa/wilaya na chama kama usivyoweza kumtenganisha raisi na chama.
 
Back
Top Bottom