Hii ya Wakuu wa Wilaya Kupewa Ilani ya CCM imekaaje?

Wateule wa Rais huteuliwa na Rais kumsaidia kutekeleza Ahadi za Rais.unapewa Ilani ili kujua Mahitaji yanayotegemewa kutokana na kazi yako.
 
Hili jambo halijawahi kufanywa na mkuu yeyote wa mkoa katika kuapisha MaDc. Huyu Makonda huku kusifiwa sifiwa kusiko na tija na mkuu kuna mfanya afanye mambo ya ajabu ajabu ambayo hayana mwelekeo mzuri.
Kama Magufuli anaona mwenendo wa Makonda ni sawa basi shauri yake, lakini kiongozi mzuri ni yule anaye kwepa migogoro ya kikatiba
 
Nadhan ungesikiliza hotuba ya raisi siku wakuu wa wilaya walipokua ikulu usingepata shida. Moja ya majukumu aliyowapa ni kuhakikisha yaliyomo kwenye ilani yanasimamiwa na kutekelezwa. Ilan inayotekelezwa ni ya chama kilichoshinda, kwa hiyo hapo hakuna jipya. Kwa kuweka kumbukumbu sawa mwaka 2010 Mh Magufuli(alipoteuliwa kua waziri wa ujenzi) na Mh. Mwakyembe(alipoteuliwa kua Naibu waziri) wakati wanaenda wizarani kwako mda mfupi baada ya kuapishwa walienda na ilani ya ccm na Mh. Magufuli mwenyewe aliwambia watendaji wakuu waliokuwepo kuipitia vizuri ilani hiyo na kuhakikisha inatekelezwa ndani ya miaka mitano.
halafu ilitekekezwaje hapo wizarani kwao? Kwa 100% ? Iliwasaidiaje watanzania kwa kipindi cha 2010- 2015? Ni aibu kulisemea siyo? Siku nyingine ukiwa na bunch of theories na ukaziapply kwa miaka kumi then ukajievaluate na kujikuta efficiency is below average unazitupilia mbali na kuja na idea mpya. Hiyo ilani yenu ilishafeli for almost 50+ years why mnaendelea kuja nazo zilezile?
Wale wakuu wa wilaya ni watendaji wa chama au umma? Kama ni wa umma, jiulize umma huo ni wa ccm pekee yao? Na kama wanakwenda na ilani ya ccm ni kwanini walipwe na serikali badala ya ccm iliyowaajiri? Usizungumzie ilani inayotekelezwa bali jadili ni nani mwajiri wao.
 
Hivi ni kweli? Hivi rais hazioni kasoro hizi za waziwazi? Waziri mkuu yabidi utoe semina elekezi kwa hawa wakuu wako wa mkoa na wilaya vinginevyo ni mahoka haya!
Makonda, hao ni watendaji na waajiriwa wa serkali kuu na siyo makatibu wa ccm. Kuwapa ilani ya ccm ni kuwatuma kuwatumikia wanaccm tu. Hii siyo haki na hsikubaliki. Haijawahi kutokea popote katika historia ya taifa hili tangu ukoloni. Magavana popote duniani hukabidhiwa katiba ya nchi na ilani huikuta kwenye ofisi za chama waendako. Mamlaka husika kemeeni mikurupuko hii kwani hata mkilazimisha kupendwa kwa ccm haiwezekani tena.

Ndg, kwanza yakupasa kuekewa kuwa udc ni vyeo vya mkoloni na vya kikoloni. CCM ni Mkoloni Tanzania. Vyeo wamepewa na Mkokoni wa CCM. Unashangaa nini?

MUHIMU NI KUPAMBANA JINSI YA KUMNG'OA MKOLONI CCM. BILA KUMNG'OA KWA MABAVU KAMWE VYEO HIVYO HAVITATOKOMEA. RASIMU YA PILI YA WARIOBA ILIVIONDOA VYEO HIVYO VYA KIKOLONI. LAKINI KATIBA PENDEKEZWA YA MKOLONI CCM WAKAVIREJESHA.

HAWA JAMAA NI PASUA VICHWA. NCHI HII WALIPEWA KWA DAMU NA WAO WATAIACHIA KWA DAMU. JIEPUSHE SANA NA SIASA ZAO. JITAFUTIE RIZIKI ZA MAISHA. ACHANA NA MAMBO YAO.
 
mtoa mada napenda kukufahamisha pia kuwa si wakuu wa mikoa na wilaya tu,pia unapoandaa mpango wa kazi iwe wa miaka 5,3,2 au 1 unaandaa kwa kuzingatia ilani ya chama kilikuwa madarakani si vinginevyo.hata km ww ungekuwa ukawa na upo serikalini uwe mkurugenzi au mkuu wa taasisi flani ya serikalui unapoaandaa mpango wako wa kazi lazima uangalie vipaumbele kwa kuzingatia ilani ya chama kilichokuwa madarakani
 
Ilan anapewa mtumishi wa chama husika na sio mtumishi wa serikali ndg! Cheo cha mkuu wa wilaya sio chakichama na mtu yoyote anaweza kuwa sio lazima we wa chama tawala hizi ni nafasi za uteuzi

Ni kama alivyoteuliwa mbunge Mbatia na Kikwete halaf apewe ilan ya CCM??
Kati ya wale wanaojua wanajua' Kumbe hajui ni pamoja na wewe!
Jenga uelewa kwanza kabla hujabandika hoja yako na kuonekana ni Mbumbumbu'
 
Vijana siku hizi mnasoma shule gani? Yaani hili ni suala la kuumiza kichwa kweli? Kwamba iweje wakuu wa wilaya watumie Ilani ya CCM? Yaani hili ni la kushangaa na kulipigia kelele?

Toba Yailahi!
 
Jamani cheo cha mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ni vya ma kada tu wa ccm sasa mimi sishangai viongozi wa ccm kuvunja taratibu
 
Si ma DC peke yake wanapewa ilani ya CCM. Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, na watumishi wote wa umma hupewa ilani hiyo. Mipango kazi ya idara/wizara hubadilishwa ili kuhakikisha yale yaliyoko kwenye ilani yanatekelezwa. Kimsingi, kila mmoja katika serikali anafanya kazi ya kutekeleza ilani ya CCM.
 
Kwa hii miaka mitano mpaka madiwani na mameya wa CHADEMA wanatekeleza Ilani ya chama tawala CCM. Wakati wa kampeni kila chama kilikua kinanadi ilani ya chama chake. chama kinachoshinda Ilani yake ndio inayoshinda na ndio itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa lugh nyepesi ni kama kumtokea demu kila mmoja anatoa ahadi zake sasa yule anayekubaliwa ndo anatakiwa azitimize hizo ahadi
 
Irani ya Ccm!!!!!!!!! Naomba kujuzwa kama Chenge.. Tibaijuka... Ngereja... Lugemalira... Seth Singh... First lady aliyechuma ktk Enjios fulani! nk wote wamepewa Irani?
 
Back
Top Bottom