Hii ya Wakuu wa Wilaya Kupewa Ilani ya CCM imekaaje?

Huwa Ninapata wasiwasi sana pale Mr Magu Anaposema "Yeye ni Rais Wa Wanyonge"

Ndiyo Kina Nani Hao Wanyonge??
Mtumishi Wa Serikali Anayesimamia Wilaya Yenye Wanyonge Anapewa Ilani Ya CCM, sasa je Huyu Atasimamia Maslihi Ya Wanyonge au Atasimamia Maslahi Ya CCM uchwara??

Hii Ni Nchi ya Kusadikika....
 
image.jpeg
 
Naona makonda anawaapisha kisha anawa ilani ya chama cha mapinduzi

Ivi hawa ni watumishi wa chama au serikali? Me navyojua watumishi wa serikali wangepewa katiba ya nchi na waape kuilinda sasa mbona wanapewa ilani ya chama?

Attach
37409f08d6ea617f661c268bdceacc7e.jpg
Ilani na ahadi zinazo tekelezwa ni za chama tawala CCM.
 
Hivi ni kweli? Hivi rais hazioni kasoro hizi za waziwazi? Waziri mkuu yabidi utoe semina elekezi kwa hawa wakuu wako wa mkoa na wilaya vinginevyo ni mahoka haya!
Makonda, hao ni watendaji na waajiriwa wa serkali kuu na siyo makatibu wa ccm. Kuwapa ilani ya ccm ni kuwatuma kuwatumikia wanaccm tu. Hii siyo haki na hsikubaliki. Haijawahi kutokea popote katika historia ya taifa hili tangu ukoloni. Magavana popote duniani hukabidhiwa katiba ya nchi na ilani huikuta kwenye ofisi za chama waendako. Mamlaka husika kemeeni mikurupuko hii kwani hata mkilazimisha kupendwa kwa ccm haiwezekani tena.
Ndugu ysngu mtumishi yeyote laxima aelewe ilani ya chama tawala ndio yenye kuongoza hakuna kosa hapo ndio magufuli aliinadi na kuchaguliwa huo ndio muungozo kwa serikali.ingekuwa ni katiba ya ccm hapo tungehoji
 
Bila kupoteza wakati nilisha sema na ninarudia tena na tena uDC ni ukada wa CCM tu na hauna manufaa kwa Watz. zaidi ya kulinda maslahi ya Chama.
Hivyo NIKUFUTILIA MBALI NAFASI ZINGINE ZISIZO NA TIJA, CCM achecni uwoga kama kweli mnania ya kubadilisha Tz.iwe ktk uchumi wa Kati tupate KATIBA MPYA YA WANANCHI KWA KUBORESHA ILE YA WARIOBA, mnachoogopa nini hasa?????????????
Na mnapendwa na Watz.....
 
Pointi ya muhimu sana hiyo:Rais huapa kwa Katiba.

Kwa mtindo huu wa kuwapa ilani ya CCM badala ya Katiba, ni kuwagawa Watanzania kwa misingi ya tofauti zao za kisiasa...
Na huu ndo msingi wa swali langu
 
Wakuu wa Wilaya na Miko ni political post na ni lazima watekeleze matakwa ya chama kilichowateua. Tofauti na wakurugenze wa Halmashari ambao ni watendaji na ambao wanabanwa kotekote japo kuwa nao ni lazima wasikilize kwa chama kilichowateua!!! Ni ngumu sana kwa hasa Tanzania na nchi nyingi za Afrika kutenganisha Siasa na Utendaji.
 
Kuna shida kubwa katika hii katiba ya sasa, tusipo angalia watazigawa hizo katiba zao mpka ktk nyumba za ibada.
 
Ukawa mu wepesi mno wa kusahau,mgombea wenu wa kudumu wa urais aliita mameya wote wa ukawa akawapa ilani akawaambie wakafanyie kazi mkasifia sana humu leo mnashangaa chama chenye serikali kutumia ilani?
Wakuu wa wilaya ndio nyenzo muhimu katika usimamizi na utekelezaki wa ilani
Ccm wanawapa ilani watu wao wakafanyie kazi,ukawa ilani yao ipo mtandaoni
 
Back
Top Bottom