Hii ya Wakuu wa Wilaya Kupewa Ilani ya CCM imekaaje?

Kimsingi watumishi wa umma wote wanatekeleza Ilani ya Chama kinachotawala ambacho kwa sasa ni CCM.

Hivyo, hata wasingepewa hiyo Ilani ya CCM hao wakuu wa Wilaya, bado wana jukumu la kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya CCM ktk Wilaya na halmashauri zao.
 
Ni makatibu wa Chama tawala ! Sasa sijui mishahara wanalipwa na chama au Serikali?
 
Ilan anapewa mtumishi wa chama husika na sio mtumishi wa serikali ndg! Cheo cha mkuu wa wilaya sio chakichama na mtu yoyote anaweza kuwa sio lazima we wa chama tawala hizi ni nafasi za uteuzi

Ni kama alivyoteuliwa mbunge Mbatia na Kikwete halaf apewe ilan ya CCM??
Anaenda kutekeleza hicho alichopewa
 
Watumishi wote wa serikali wanatakiwa (lazima) kutekeleza ilani ya chama kinachoongoza , hivyo kwa kuwa ccm ndiyo inayoongoza basi serikali yote na watumishi wake wanasoma na kutekeleza ilani ya ccm. Hata kama ilani hiyo ni mbovu itatekelezwa hivyo hivyo kwa kuwa si ndicho mlicho chagua?. Vyama vya upinzani ni kuwaambia wananchi nini kimeshatekelezwa na nini bado kwenye ilani hiyo ya ccm na hatua za kuchukua. Hii ni kwa chama chochote kile kitakachoshika hatamu.
 
ukifuatilia sana mambo ya nchi hii utakuwa chizi so tuhesabu siku tu "ikawa asubuhi ikawa jioni......." kama hadi soldiers wameteuliwa cjui nao ni kada?
 
Swali hilo kweli TATA NA MUULIZAJI MTATA AMA hajui analotaka, ama anataka kusikia twasemaje.
1.Chama tawala ndicho chenye kuelekeza 'ROAD MAP' na hilo linafikiwa tu kupitia ILANI YAKE.
2.Hata Meya akiwa wa Chama mbadala bado itambidi kutekereza sera za Chama tawala, kikubwa mnachweza kufanya ni kuona Wananchi wanahudumiwa vema , kuhakikisha budget inayopitiswa inatumika ipasavyo kwa manufaa ya walengwa
 
Swali hilo kweli TATA NA MUULIZAJI MTATA AMA hajui analotaka, ama anataka kusikia twasemaje.
1.Chama tawala ndicho chenye kuelekeza 'ROAD MAP' na hilo linafikiwa tu kupitia ILANI YAKE.
2.Hata Meya akiwa wa Chama mbadala bado itambidi kutekereza sera za Chama tawala, kikubwa mnachweza kufanya ni kuona Wananchi wanahudumiwa vema , kuhakikisha budget inayopitiswa inatumika ipasavyo kwa manufaa ya walengwa
Swali jepesi sana mkuu wa wilaya ni mtumishi wa uma au wa chama? Kama ni wa chama sawa ila kama ni wa uma anapaswa apewe katiba ambayo atailinda au ilani ya chma?
 
Hivi hujui chama kikishachaguliwa kinaongoza serikali kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi ambayo hasa ndio iliyochaguliwa na wananchi iwaongoze???
Hujui kwamba tukitaka kuhoji kufaulu ama kufeli kwa serikali tunatumia ilani yao ya uchaguzi???
Hivi na wewe kweli ndio umeamua kuandika haya ili great thinkers wasome?????.
 
Matatizo matupu,mkulu wao kasema siasa zimekwisha,huku wanapitisha pitisha njano na kijani,tena kwenye media ili tuone wengi,UKAWA imeshika watu pabaya
 
Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ni wawakilishi au wasaidizi wa rais katika ngazi husika,kwa maneno mengine ndio marais wa maeneo hayo,ndio maana wanamsaidia rais kutekeleza ilani yake aliyoinadi kwa wananchi.
Heeeee marufuku kuita raisi katika ngazi husika,huyo ni mkuu wa wilaya.Tukikwambia utupe tafsiri ya neno raisi,haitataja mkuu wa wilaya/mkoa koma kabisa
 
Wakati mwingine tuache siasa na tuangalie uhalisia. Ndugu mkuu wa mkoa au wilaya no muwakilishi wa raisi aliye mteua kumsaidia usimamizi na utekelezaji wa shuguli za kila siku ambazo ameziahidi katika kampeni zake hadai akachaguliwa na wapiga kura wake chino ya ilani aliokuwa anainadi. Sasa nini cha ajabu kumpa msaidizi wako mwongozo wa utendaji kazi chini ya ilani iliyokuweka madarakani? Jamani tuwe wepesi wa kutafakari mambo. Vitu vingine havihitaji hata elimu kubwa. Hata Leo hii ukiajiliwa sehemu yoyote lazima upewe mwongozo wa kufuata ili uweze kutekeleza kazi husika kwa malengo na faida ya mwajili wako.
 
Back
Top Bottom