Hii thinking ni ya Japan au Old Europe na USA lakini sio Afrika

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,409
8,908
Alitaka kujenga treni ya Umeme Tanzania, swali likaja umeme atautoa wapi wa kuendesha hiyo treni?

Akapiga akili akagundua kuna uwezekano wa kupata zaidi ya 2000 MW green energy huko Rufiji Delta, akaingia lab kazi ikaanza, Bwawa la kuzalisha umeme zaidi ya 2000 MW likaanza kujengwa fasta sambamba na Miundombinu ya treni ya umeme.

I mean this is genius, kafikiria Tanzania inategemea Utalii kwa mapato lakini Watalii wanaletwa na foreign Airlines hivyo sehemu kubwa ya mapato kwenda nje badala ya nchini kaingia lab kaja na suluhisho kununua ndege zitakazoleta Watalii moja kwa moja nchini.

Tanzania inauza maua nje lakini inategemea Kenya Airways/KLM kusafirisha kwenda EU kaingia lab kaja na suluhisho tunahitaji ndege ya Cargo ili kusafirisha maua moja kwa moja ndege imepokelewa juzi.

Akili hii ipo Japan, Ulaya na USA ya zamani tu.
 
La kwanza kuhusu SGR Magufuli was perfect, spot on, alitaka treni ya umeme, akajua huu umeme wa Tanessco tulionao wajanja walishaugeuza dili kwao, wakawa wanatupiga watanzania kupitia hapo, wajanja kila mwezi wanalipwa mapesa mengi tu.

Sasa kwenye kuwakwepa hao, ndipo Magufuli akaenda na Bwawa la Nyerere, hapa mafisadi wakaungana na wazungu kupiga kelele Bwawa la Nyerere litaharibu mazingira, mvua hazitanyesha kisa amekata miti sijui milioni ngapi!.

Magufuli hakuwasikiliza, akasimamia kile alichokiamini, leo tunaambiwa Bwawa linakaribia kujaa, tena tunatangaziwa hivyo na mpinzani aliyeamua kukubali ukweli ili asijitese nafsi yake, tena linajazwa na zile mvua walizosema zisingenyesha.

Magufuli aliniachia somo kubwa sana, hasa nikimlinganisha na huyu mtawala tuliyenaye sasa.

Kiongozi siku zote lazima awe na maono, ajue kutumia akili yake ili kutimiza maono yake kwa manufaa ya wale anaowaongoza, awe na msimamo wenye mantiki, sio wa kijinga kama kukumbatia mawaziri mizigo mpaka wakuharibie, na awe na kichwa cha kufikiri, sio kusaidiwa kufikiria na watendaji wake hata wenye mentality ya wizi na ufisadi na kuwatetea kwa nguvu.
 
Yaani nawaza watu disaini ya legendary JPM kwa nini hawatakiwi duniani!.

Ila pamoja na yote hata hawa waliofanya kazi yao mioyo yao inaendelea kuvuja machozi, japo nje tunaona meno ya kicheko.

Historia itadumu hata kama atasemwa huyu au yule ndiye alileta hiki au kile, bado JPM atabaki kuwa mwenye kuthubutu hasa.
 
Alitaka kujenga Treni ya Umeme Tanzania, swali likaja umeme atautoa wapi wa kuendesha hiyo treni? Akapiga akili akagundua kuna uwezekano wa kupata zaidi ya 2000 MW green energy huko Rufiji Delta, akaingia lab kazi ikaanza, Bwawa la kuzalisha Umeme > 2000 MW likaanza kujengwa fasta sambamba na Miundo mbinu ya Treni ya umeme, I mean this is genius, kafikiria Tanzania inategemea Utalii kwa mapato lkn Watalii wanaletwa na foreign Airlines hivyi sehemu kubwa ya mapato kwenda nje badala ya nchini kaingia lab kaja na suluhisho kununua ndege zitakazoleta Watalii moja kwa moja nchini.
Tanzania inauza maua nje lkn inategemea Kenya Airways/KLM kusafirisha kwenda EU kaingia Lab kaja na suluhisho tunahitaji ndege ya Cargo ili kusafirisha maua moja kwa moja ndege imepokelewa juzi, akili hii ipo Japan, Ulaya na USA ya zamani tu, …
Wenye akili ya kuku hawajui kuwa wazo la umeme wa Stieglers Gorge lipo hata kabla ya uhuru.
Mwalimu alisha anza kuliweka kwenye bajeti kwa kuanzisha RUBADA.
Utoto nao mzigo.
 
Africa/Tanzania naomba niongelee Tanzania ni nchi yenye watu makini sana yaani wenye akili nyingi sanaa isiyo na mfano tena akili asilia kabsa na ukiacha kufichwa fichwa vitu lakini sisi bado tuna uelewa mkubwa sana ambao sio wa kufundishwa na dunia nzima inajua yaani mataifa yote ya nchi yanafahamu hakuna asiyejua Tanzania ni nani?

Na akili hizo kila secta sema tu sasa hivi kuna ujinga mwingi mpaka hizo akili sasa hizi hazitumiki tena imeingia tamaa tu na uhujumu ndio tatzo wamefanya watu wafikilie pesa tu yaani wamesahau uzalendo lakini ukiacha yote hayoo watanzania ni binaadamu wenye akili sana tena asilia yaani uwezi amini ila ni taifa hatari sanaa wanatufanya tuwe na njaa tufikirie tutakula wapi? Ili tuache matumizi mazuri ya uelewa wetu ambao hatujafundishwa popote sasa akili ya kuzaliwa plus kufundishwa taaluma haumgusi MTANZANIA hapo
 
Swali kama hili ni sawa na kuuliza kwa nini mtoto hatembei baada ya kuzaliwa. Maendeleo ni process siyo tukio
Ni kweli, lakini Kama process inachukua miaka hamsini na wananchi wanataabika kwa kukosa umeme huo ni ujuha!!! Lazima tubadilike!

Kwahiyo unataka kuniambia kama mtoto ameshindwa kutembea kwa miaka zaidi ya hamsini tutegemee kuna kutembea kweli?
 
Back
Top Bottom