DodomaTZ
Member
- May 20, 2022
- 71
- 107
Kuna kitu nimekuwa nikikitafakari kwa muda mrefu, nikahisi yawezekana ni mimi tu fikra zangu ndiyo mbovu au za kizamani, lakini baada ya kumsikia Jaji Warioba akizungumzia suala hilo, nami nimepata nguvu kuamini kuwa ninachowaza kuwa ni tatizo basi inawezekana ni tatizo kweli
Zamani nakumbuka viongozi wengi walikuwa na kawaida ya kwenda sehemu za ibada na katika shughuli za kijamii zao yaani majirani wa mtaa mmoja au mitaa ya karibu.
Hiyo ilikuwa ikifanyika sana tu, na walipokuwa wakifika katika shughuli hizo wengi wao licha ya kuwa walikuwa na majina makubwa, walijishusha na kuwa sehemu ya jamii hiyo na kufanya kile walichotakiwa kukifanya.
Kama ni msibani basi walishiriki kama wananchi wa kawaida lakini bado walipewa heshima yao na wananchi wengine wa kawaida, kama ni kwenye ibada, hivyohivyo hawakuwa na makuu.
Sasa viongozi wengi wa sasa na watu maarufu wa fani tofautitofauti sijui ndio tandawazi au mimi ni mshamba, wengi wao wakishiri lazima watataka wawe watu special hilo eneo husika.
Wengine mbali na kuwa special watataka wapewe nafasi wazungumze, kibaya zaidi wakipewa nafasi hiyo badala ya kuzungumza kile ambacho kimewafanya wawepo hapo, wao wanaleta mada nyingine kabisa za kisiasa.
Hii ni mbaya, inamaana kama mtu kaenda Msikitini au kanisani au kwenye msiba au harusi, wewe kiongozi ukipewa nafasi usitumie nafasi hiyo kutaka kumkwaza mtingine kwa kuingiza sera za uchama au udini wako ambao hauna sababu za msingi.
Mimi hili suala linanikera sana ndio maana kuna wakati nikisikia kiongozi fulani wa kisiasa yupo katika msiba au nyumba fulani ya ibada na ninajua sera zake na mimi zinapishana bora nisiende kabisa hiyo sehemu.