Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,654
- 46,314
Kama tunasema sisi ni taifa moja na hatubaguani kwa dini, rangi au itikadi za kisiasa tafsiri nzuri zaidi ya hili ni katika majanga na madhila mbalimbali ya kitaifa.
Katika matukio kama hili la Hanang si ingekuwa jambo bora zaidi hata Mbowe na Rais wakatembelea au kupanga kukutana baadhi ya sehemu zilizoathirika na kuonyesha mshikamano zaidi wa pamoja katika majanga?
Ifike mahali iwe jambo la kawaida viongozi/wanasiasa wa upinzani kukutana na wenzao wa CCM katika mambo ya kijamii yanayogusa maslahi ya watu wengi.