Kama kuna kitu kinahakikiwa kwa umakini na kwa kurudiwa basi ni hiki kitu pesa.... Unaweza kumpunja mtu kwenye kitu chochote lakini sio pesa... Mpunje kwenye kipimo cha nafaka, ukamzidishia kilometer za mwendo ama hesabu fulani lakini sio linapokuja suala la fedha tasilimu....
Chakushangaza ni kwamba hata kama mtu hakudai na hufanyi naye muamala wowote wa kibiashara ama malipo fulani... Yani unampa tu kama hisani au zawadi... Ni lazima ahesabu hata kisirisiri bila kujali kwamba umemwambia wazi kiasi ulichompatia.. Iwe ni ndugu yako mzazi ama hata uzao wako mwenyewe.
Kituko zaidi cha pesa ni pale mtu anapoidharau pesa ndogo na kuithamini pesa kubwa... Hizi senti... Hizi shilingi shilingi hizi.... Hizi ndio za kuwapa ombaomba hizi ndio za kuwapa watoto kanisani na kwenye nyumba nyingine za ibada... Hizi ndio za kuwekwa kwenye draw za magari... Hazistahili kukaa kwenye wallet zenye mapene na pochi nene....!!!!
Wenye akili kubwa wameliona hili... Na wanaishi maisha ya bata za kufuru kupitia visent tuu.... Hivi ni wangapi huwa wanahakiki miamala yao mitandaoni mpaka visenti? Na ukivikuta havipo je ni nani anaweza kufungua shauri la madai?
Biashara zote za miamala ya mitandaoni kama forex nknk wao wanacheza na visent tuu.... Ukivilimbikiza kwa wingi kwa njia mbali mbali na kila aina ya ujanja unajikuta unatoboa kimasihara kabisa.....
Dogo mmoja jobless huko marekani alikaa chini akaumiza kichwa... Kisha akatoka na suluhu ya kushangaza mno
Kwa kutumia utaalam wake wa computer akajiunganishia aina ya mfumo unaokata visent tu kwenye akaunti za wateja kwenye bank moja kubwa huko huko marekani... Akaifanya computer yake automatic masaa 24 ikawa vicent vinamiminika kwenye akounti yake....!!!!
Alikuja kukamatwa baada ya maafisaa wa benki kustukia akounti yake yenye zaidi ya USD million 2 lakini ikiwa muda wote inapokea visent chini ya dola moja... Walishangazwa na hili na kujiuliza ni mtu gani huyu na anafanya biashara gani hii inayomuingizia Visent tuu lakini muda wote 24/7
Baada ya uchunguzi na kuvamia makazi yake walikuta nyumba iko tupu lakini kukiwa na laptop mezani iko kazini... Yeye alikutwa Las Vegas jiji la maraha akitumbua maisha na malaya 4 wa bei ghali
Ukimuona Mo anitathamini 50 usimuone mjinga bali jicheke...