Hii tabia ya pesa inashangaza mno

Hii tabia ya pesa inashangaza mno

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
373,211
Reaction score
864,642
Kama kuna kitu kinahakikiwa kwa umakini na kwa kurudiwa basi ni hiki kitu pesa.... Unaweza kumpunja mtu kwenye kitu chochote lakini sio pesa... Mpunje kwenye kipimo cha nafaka, ukamzidishia kilometer za mwendo ama hesabu fulani lakini sio linapokuja suala la fedha tasilimu....

Chakushangaza ni kwamba hata kama mtu hakudai na hufanyi naye muamala wowote wa kibiashara ama malipo fulani... Yani unampa tu kama hisani au zawadi... Ni lazima ahesabu hata kisirisiri bila kujali kwamba umemwambia wazi kiasi ulichompatia.. Iwe ni ndugu yako mzazi ama hata uzao wako mwenyewe.

Kituko zaidi cha pesa ni pale mtu anapoidharau pesa ndogo na kuithamini pesa kubwa... Hizi senti... Hizi shilingi shilingi hizi.... Hizi ndio za kuwapa ombaomba hizi ndio za kuwapa watoto kanisani na kwenye nyumba nyingine za ibada... Hizi ndio za kuwekwa kwenye draw za magari... Hazistahili kukaa kwenye wallet zenye mapene na pochi nene....!!!!

Wenye akili kubwa wameliona hili... Na wanaishi maisha ya bata za kufuru kupitia visent tuu.... Hivi ni wangapi huwa wanahakiki miamala yao mitandaoni mpaka visenti? Na ukivikuta havipo je ni nani anaweza kufungua shauri la madai?
Biashara zote za miamala ya mitandaoni kama forex nknk wao wanacheza na visent tuu.... Ukivilimbikiza kwa wingi kwa njia mbali mbali na kila aina ya ujanja unajikuta unatoboa kimasihara kabisa.....

Dogo mmoja jobless huko marekani alikaa chini akaumiza kichwa... Kisha akatoka na suluhu ya kushangaza mno
Kwa kutumia utaalam wake wa computer akajiunganishia aina ya mfumo unaokata visent tu kwenye akaunti za wateja kwenye bank moja kubwa huko huko marekani... Akaifanya computer yake automatic masaa 24 ikawa vicent vinamiminika kwenye akounti yake....!!!!

Alikuja kukamatwa baada ya maafisaa wa benki kustukia akounti yake yenye zaidi ya USD million 2 lakini ikiwa muda wote inapokea visent chini ya dola moja... Walishangazwa na hili na kujiuliza ni mtu gani huyu na anafanya biashara gani hii inayomuingizia Visent tuu lakini muda wote 24/7
Baada ya uchunguzi na kuvamia makazi yake walikuta nyumba iko tupu lakini kukiwa na laptop mezani iko kazini... Yeye alikutwa Las Vegas jiji la maraha akitumbua maisha na malaya 4 wa bei ghali
Ukimuona Mo anitathamini 50 usimuone mjinga bali jicheke...
 
Tunadharau hela ndogo kwasababu jinsi ya kuzi manage inakuwa shida. Pia hazina thamani tena, nioneshe kitu cha 50 sahivi.

Hata wewe ukiambiwa uchukue 10.000 ya noti au ikiwa na sarafu za 50 utachagua ipi? Bila shaka utachukua ya noti unless uwe unauza chenji.

Mimi huwa naziweka hizi hela za sarafu kwenye ndoo hapa nyumbani. Mfuko umejaa coins ila hazina thamani.

Ila siwezi beba coins mfukoni.
 
Tunadharau hela ndogo kwasababu jinsi ya kuzi manage inakuwa shida. Pia hazina thamani tena, nioneshe kitu cha 50 sahivi.

Hata wewe ukiambiwa uchukue 10.000 ya noti au ikiwa na sarafu za 50 utachagua ipi? Bila shaka utachukua ya noti unless uwe unauza chenji.

Mimi huwa naziweka hizi hela za sarafu kwenye ndoo hapa nyumbani. Mfuko umejaa coins ila hazina thamani.

Ila siwezi beba coins mfukoni.
Haimaanishi uzibebe ila usizidharau.. Thamani yake huonekana kwenye stock exchange markets
 
kuna kipindi nilianza mtindo kila niludishiwapo silimbi nazitupia ndani ya begi langu iwe 50,100,200.

nilikuja kushtuka begi limekuwa zito sana kuja kuzimwaga ziko kibao. nikaziacha nyumbani. ikawa ndio mtindo wangu naziweka ndani ya begi then baada ya week naziunganisha na zile za home. siku moja nimekwama kuja kuhesabu zile silimbi zimefika 60000+

hapo ndipo niliamini hakuna pesa ndogo ni kuimanage tu. mpaka sasa ndivyo nafanya.
 
Alafu tabia nyingine ya pesa ni hivi,
Mi nikiwa na hela nyingi nakosa kabisa appetite(hamu) ya kula...yaani naweza kaa kutwa nzima bila kula...ikifika muda wa kulala ndo nahisi njaa
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji848][emoji848][emoji848][emoji23][emoji23][emoji23]hii kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom