Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Binadamu mnapenda kujitafutia vifo kabla ya mda wenu

Hizo ligi zinafaida gani?
 
Ligi tamu kuanzia saa 10 jioni kutafuta kale kagiza cha saa 1 kasoro baba unakutana na V8 flani STK dereva anayejitambua, ligi inakuwa tamu sana. Yeye anaamini v8 inachanja mbuga na 220 yake mnyama BMW unasoma 240 halafu boss wake amelala hahahaha au na yeye anapenda ligi dereva anamwambia kuna mshezi anakuja kasi hapo nyuma unaona boss anachungulia kwenye mirror unaona v8 inaanza kuchanganya 180- 190 anachezea hapo kijana namuashia indicator napita anapagawa.

Mara mbele mteremko sipiti asije akasema nimetumia advantage ya mteremko nasubiria muinuko tunavyoanza kukamata tambarare basi napita.

Mjerumani nyoko sana BMW forever
Jaribu na Ford Mustang....hawa ndio wazee wa mwendo...
 
Naona warning lights za kutosha hapo kwenye dashboard.

Una amani kabisa ukiwa na hizo lights na umemaliza kisahani?
Red warning lights ndio za hatari....
sio hizi za njano....hizi ni minor case the damage does not go to the root....
ni fault ndogo zimekuwa detected....
infact zinakuja na kupotea....
 
Nakumbuka nilifanya ligi moja Matata na nisoyemjua barabarani siku niliyotoka kupiga kura, mwaka 2015....

Barabara iliyohusika ni Ali Hassan Mwinyi kuanzia hapa mataa ya Serena hadi Bagamoyo Road maeneo ya Tegeta.

Mida ilikuwasaa kumi jioni.

Chanzo cha ligi, alinichomekea kiboya bin kibabe halafu akanioneshea like, nshakuchomekea utanifanya nini sasa.... mmaamaaeee nilimkanyagia mafuta nahisi alienda kumeza cofta kwa vumbi nililomuachia. Shida yangu niko mbishi sana...

Siku husika ilikuwa jumapili watu sio wengi barabarani na siku ya uchaguzi hivo barabara ilikuwa nyeupeee.

Gari alilotumia mleta ligi mwenzangu kama sijasahau ilikuwa Altezza maana ilikuwa hizi gari za chini. Mimi nilikuwa na Grand Car (yaani gari ya juu halafu iko branded grand uchomaji wake wa mafuta uko sawia na V8 hukoo).

Siku hizi nimekua kiasi nimepunguza ukorofi na ubishi, ligi za barabarani almost nimeziacha.

Ligi niliyobakia nayo ni ya Mahaba na Mziki tuu. Mtu akiwa tayari tufanye ligi ya kucheza mziki kuanzia saa nne usiku hadi jogoo la saa kumi alfajiri linawika bila kupumzika.....

Kasinde Platinum Matata.
Hebu tafuta hii album #kitaaolijia toka cheusidawa just search insta hutojuta yani utakuwa unarewind tu hadi kunakucha
 
Hebu tafuta hii album #kitaaolijia toka cheusidawa just search insta hutojuta yani utakuwa unarewind tu hadi kunakucha

Siko instagram, nimeingia youtube zimekuja nyimbo tofautitofauti sijajua ulimaanisha wimbo gani...



Au ulimaanisha huu...

 
Watu pekee wendawazimu wapenda ligi ni IT na gari za gazeti tu, wale mbwa wanajua kuchoma wese ile mbaya.
Mimi na ubishi wangu road huwa sina ubavu kufukuzana nao, unaweza jikuta ghagla bin vuu matairi yapo juu halafu mseleleko wa vyuma tu ile unaona chechee halafu mwenzako yuleeeeee kasepa hahahaaa.
 
Ligi za barabarani ndio ilikuwa michezo yangu but toka nimeoa na kuwa na familia nimepunguza manake naogopa kupasua nyanya/kupata ajali.....
Hereinbelow is one of my race nikiwa na Crown Athlete....
I was a dumb mthefcker racer...
[emoji3][emoji3][emoji3] Ungejaribu na ambazo zinaenda zaidi ya hapo.
By the way kama picha umeipiga mwenyewe na gari iko kwenye huo mwendo uko vizuri...
Na naona dash board yako taa nyingi zinawaka pia ni risk sana
 
Kuna watu wengi wamekufa kwa mwendo huo. Mimi nimenusurika zaidi ya mara 10 kwa ajali za aina hiyo.

1. Pale Ruvu nimenusurika kugonga gari yenye taa moja nikidhani pikipiki.

2. Igunga, nilinusurika kulivaa lori lililopaki pembeni.

3. Wami, nilinusurika kulivaa lori liliharibika katikati ya barabara.

Na mengine mengi tu. Usiku ni risk sana kukimbia kama huifahamu njia vizuri.
Ishu hapo ni kuifahamu njia mkuu.
Njia ya Dar-Mwanza naifahamu sana.
Nafahamu changamoto zote za hiyo njia.
Nimenusurika mara nyingi pia
 
Watu pekee wendawazimu wapenda ligi ni IT na gari za gazeti tu, wale mbwa wanajua kuchoma wese ile mbaya.
Mimi na ubishi wangu road huwa sina ubavu kufukuzana nao, unaweza jikuta ghagla bin vuu matairi yapo juu halafu mseleleko wa vyuma tu ile unaona chechee halafu mwenzako yuleeeeee kasepa hahahaaa.
IT wengi natoka nao Dar jioni, na wanabaki nyuma sana... Na ishu ni aina ya magari wanayotumia. Hivi Vi spacio na vi raumu haviwezi ligi kabisa.
 
Back
Top Bottom