Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hapo ni Kifo kilikuwa kinawaita. Tumshukuru MUNGU kama mlifika salama
 
Usiseme inaunafuu mkubwa kuliko bus yoyote kwa sasa wakati gemilang zipo kibao kwa Rungwe, tashriff, dar exp n.k
Hiyo scania ya Sauli weka mbali na watoto imekaa vizuri hata ikipita kwenye matuta inaunafuu mkubwa kuliko basis lolote kwasasa
 
In remembrance
IMG-20190421-WA0033~2.jpeg
 
Ligi ndo mpango mzima..safari ikiwa haina ligi inaboa kama una haraka
 
[emoji28][emoji28][emoji28] kuna kipindi flan nilipanda gari moja ya tour, kutoka Ngorongoro pale getini kuja Arusha town, jamaa alinipa lift kiroho safi!! Nahisi alikuwa amevuta bangi kidogo, kwasababu alikuwa rafu sana.
Ameshuka kwenye ule mlima kutoka Karatu kuingia mto wa Mbu kama kichaa, kutoka Mto wa mbu to Makuyuni kuna vizibiti mwenda vya chini (downs). Huyu jamaa alikuwa anazipiga balaa, aisee!! Nilivumilia sana kwa kweli.

Hizi gari za kijapani sio comfortable cars especially hizi Land cruiser hardtop
LC Hardtop ni gari ya kazi sio ya mashindano
 
kwani kidukulilo anasemaje kuhusu kushindana na vyombo vya usafiri barabarabi ilhali wewe una gari tena ford escape...najua unapitia nyuzi zake hapa daily;hukuwapa hata ofa ya nyama choma njiani??
Mkuu tumtag @KIDUKULILO atupe uzoefu wake.
 
Siyo ligi, mimi binafsi huwa napenda kumark gari moja na kutembea nyuma yake na huwa sipendi aniache sana, mkitembea kwa pamoja muda mrefu mnakuwa kama ndugu kiasi kwamba akikuacha muda hasikuone hujikuta akijiuliza yule jamaa kapata shida gani, na husishangae anakusubiri na ukipata shida husishangae mnakesha wote barabarani, so huu ni urafiki wa magari unaojijenga automatically. Magari yanafahamiana bwana!
 
Nakumbuka nilifanya ligi moja Matata na nisoyemjua barabarani siku niliyotoka kupiga kura, mwaka 2015....

Barabara iliyohusika ni Ali Hassan Mwinyi kuanzia hapa mataa ya Serena hadi Bagamoyo Road maeneo ya Tegeta.

Mida ilikuwasaa kumi jioni.

Chanzo cha ligi, alinichomekea kiboya bin kibabe halafu akanioneshea like, nshakuchomekea utanifanya nini sasa.... mmaamaaeee nilimkanyagia mafuta nahisi alienda kumeza cofta kwa vumbi nililomuachia. Shida yangu niko mbishi sana...

Siku husika ilikuwa jumapili watu sio wengi barabarani na siku ya uchaguzi hivo barabara ilikuwa nyeupeee.

Gari alilotumia mleta ligi mwenzangu kama sijasahau ilikuwa Altezza maana ilikuwa hizi gari za chini. Mimi nilikuwa na Grand Car (yaani gari ya juu halafu iko branded grand uchomaji wake wa mafuta uko sawia na V8 hukoo).

Siku hizi nimekua kiasi nimepunguza ukorofi na ubishi, ligi za barabarani almost nimeziacha.

Ligi niliyobakia nayo ni ya Mahaba na Mziki tuu. Mtu akiwa tayari tufanye ligi ya kucheza mziki kuanzia saa nne usiku hadi jogoo la saa kumi alfajiri linawika bila kupumzika.....

Kasinde Platinum Matata.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mkuu post picha ukiwa unacheza mziki.
 
Siyo ligi, mimi binafsi huwa napenda kumark gari moja na kutembea nyuma yake na huwa sipendi aniache sana, mkitembea kwa pamoja muda mrefu mnakuwa kama ndugu kiasi kwamba akikuacha muda hasikuone hujikuta akijiuliza yule jamaa kapata shida gani, na husishangae anakusubiri na ukipata shida husishangae mnakesha wote barabarani, so huu ni urafiki wa magari unaojijenga automatically. Magari yanafahamiana bwana!
Hii ni kweli kabisa mkuu.
 
Kukimbia kwa gari sio Sababu unatumia gari gani!
Mbio ni Moyo wa mtu, kuna watu wana roho ngumu sanaaaa.
Gari ni ishu kubwa sana barabarani mkuu.
Nikuambie tu kama una gari yenye engine capacity below 1900cc. Wewe ligi waachie wengine kabisa!! Hata uwe una moyo wa mbio.
 
Usiku sio salama kwa ligi.

Si rahisi kuona zaidi ya 200M, ukiwa speed zaidi ya 100kph, ni ngumu kukwepa hatari ya ghafla.

Usishindane na watu wa magazeti, hao wanapita hiyo njia kila siku tena usiku. Wanaifahamu vizuri sana.

Na usiku kuna ajali nyingi sana za uzembe na kukosa umakini.

Kuwa makini, usishindane na usiemjua.
Safari za usiku sitaki hata kusikia maana unakuwa Kwenye wasiwasi muda wote sasa hiyo shida yote ya nini
 
STI unaifahamu lkn?

Ukiachana na Vw polo R hebu tuweke hapa records wa gari za Germany nyingine kwny WRC tulinganishe na Subaru.
STI ni kelele tupu.

Nazifahamu, nimeshaendesha.

Labda uzishindanishe na kina Noah.

Hakuna kitu mule.
 
Kweli kabisa, sasa ni kute njiani na Kilitime yangu speed 220, halafu nipo mwenyewe ndio utajua ile ni vvti 2.0 or not.
Napenda sana ila nikiwa peke yangu,nikishakuwa na familia nyie piteni tu kwa raha zenu...
 
Gari ni ishu kubwa sana barabarani mkuu.
Nikuambie tu kama una gari yenye engine capacity below 1900cc. Wewe ligi waachie wengine kabisa!! Hata uwe una moyo wa mbio.
Kweli cc zinachangia mkuu lkn not a must,nilikua na mazda rx 8 ina cc 1300 ila hio Ford Escape uliyokua nayo nakupita kama umesimama vile mkuu.
 
Siyo ligi, mimi binafsi huwa napenda kumark gari moja na kutembea nyuma yake na huwa sipendi aniache sana, mkitembea kwa pamoja muda mrefu mnakuwa kama ndugu kiasi kwamba akikuacha muda hasikuone hujikuta akijiuliza yule jamaa kapata shida gani, na husishangae anakusubiri na ukipata shida husishangae mnakesha wote barabarani, so huu ni urafiki wa magari unaojijenga automatically. Magari yanafahamiana bwana!
Hii ni nzuri.

Naitumia pia. Mnaenda pamoja hata kama kuna shida anarudi kukusaidia chap.

Inakufanya unakuwa active muda wote.
 
Kweli cc zinachangia mkuu lkn not a must,nilikua na mazda rx 8 ina cc 1300 ila hio Ford Escape uliyokua nayo nakupita kama umesimama vile mkuu.
[emoji23][emoji23][emoji23] huwezi kwenda mbali kamanda.
 
Back
Top Bottom