Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hahaha
Ligi napenda kupita maelezo
Natumia cresta ila nikiona Range, au BMW huwa na respect ila awe na Roho ngumu kwani naweza clock 180k/h hata 2hrs sijafikiria kurudi ukiwa mwoga kwangu usijae mbele
Juzinimetoka Dar kuja Ar asubuhi mpaka nafika Moshi Nina faini ya 90,000 overspeed
Ha haa
 
Duh December nimenyoosha watu barabarani! Hizi Harrier sijui tako la nyani, Crown na ndugu zake nyoosha sana...! Ila ligi tamu sana
Bila shaka gti 300km/h ilihusika na shoo.

dodge
 
Ile benz inakimbia lakini hiyo scania Konyo nimepanda zote na kitaka kwenda mbeya napanda sauli au jinja hapo hata jaja na linyama na Deer zao wamesanda
Unapanda Jinja? Huogopi ajali kama ile kilitokea 2015 Iringa Majinja ilipondwa na contena
 
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
Kwa hiyo hapa unajiongelea wewe na hii tabia?!
 
Kuna siku jeep wrangler wagon nyeupe ilinipita, dah mimi mwenyewe mshale ulikuwa 140km/h, kilichonishangaza pamoja na speed hiyo jamaa alinipita nikahesabu kama sekunde hazijazidi 20, sikuiona tena ile gari.
 
Kuna siku jeep wrangler wagon nyeupe ilinipita, dah mimi mwenyewe mshale ulikuwa 140km/h, kilichonishangaza pamoja na speed hiyo jamaa alinipita nikahesabu kama sekunde hazijazidi 20, sikuiona tena ile gari.
Kuna gari hata zikiwa 180kph zinakuwa stable.

Ni rahisi kwa yeye kumantain hilo.
 
Nakumbuka nilifanya ligi moja Matata na nisoyemjua barabarani siku niliyotoka kupiga kura, mwaka 2015....

Barabara iliyohusika ni Ali Hassan Mwinyi kuanzia hapa mataa ya Serena hadi Bagamoyo Road maeneo ya Tegeta.

Mida ilikuwasaa kumi jioni.

Chanzo cha ligi, alinichomekea kiboya bin kibabe halafu akanioneshea like, nshakuchomekea utanifanya nini sasa.... mmaamaaeee nilimkanyagia mafuta nahisi alienda kumeza cofta kwa vumbi nililomuachia. Shida yangu niko mbishi sana...

Siku husika ilikuwa jumapili watu sio wengi barabarani na siku ya uchaguzi hivo barabara ilikuwa nyeupeee.

Gari alilotumia mleta ligi mwenzangu kama sijasahau ilikuwa Altezza maana ilikuwa hizi gari za chini. Mimi nilikuwa na Grand Car (yaani gari ya juu halafu iko branded grand uchomaji wake wa mafuta uko sawia na V8 hukoo).

Siku hizi nimekua kiasi nimepunguza ukorofi na ubishi, ligi za barabarani almost nimeziacha.

Ligi niliyobakia nayo ni ya Mahaba na Mziki tuu. Mtu akiwa tayari tufanye ligi ya kucheza mziki kuanzia saa nne usiku hadi jogoo la saa kumi alfajiri linawika bila kupumzika.....

Kasinde Platinum Matata.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Unajua kwel vituo..we ni dereva nin...maana nmeona uzi wa kujua vituo huu
 
Gari yangu ya kwanza kabisa ya kichovu toyota caldina, hapo natoka Moshi kuja dar na sina uzoefu sana na route za mbali, jamaa wa vits naye akaamua eti kunianzishia ligi, mimi niko 110 kph ananipita speed then mbele anaenda anapaki, nikipita tu huyu tena. Ama kweli ukiwa mchovu hata wachovu watataka ligi na wewe. Sasa hivi hata BMW akileta ligi na mimi ajipange kweli kweli, japo sita sahau kamwe dharau nilizoonyeshwa na vits kipindi nina gari la kichovu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom