Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Hii Tabia ya Kupenda ligi barabarani

Na mashine yako iwe ya ukweli, na unaofanya nao ligi wawe na mashine nzuri.
Kuna muda uko speed 180km/h, lakini unashangaa kuna mjinga anakuovertake, sio mchezo!!! kwanini mnapenda ligi? [emoji3]
Hahaha
Ligi napenda kupita maelezo
Natumia cresta ila nikiona Range, au BMW huwa na respect ila awe na Roho ngumu kwani naweza clock 180k/h hata 2hrs sijafikiria kurudi ukiwa mwoga kwangu usijae mbele
Juzinimetoka Dar kuja Ar asubuhi mpaka nafika Moshi Nina faini ya 90,000 overspeed
 
Hahaha
Ligi napenda kupita maelezo
Natumia cresta ila nikiona Range, au BMW huwa na respect ila awe na Roho ngumu kwani naweza clock 180k/h hata 2hrs sijafikiria kurudi ukiwa mwoga kwangu usijae mbele
Juzinimetoka Dar kuja Ar asubuhi mpaka nafika Moshi Nina faini ya 90,000 overspeed
aisee
 
Wakuu, nimezoea sana kutembea safari ndefu haswa Dar-Kahama-Geita na Dar-Mwanza, mara chache Dar-Bukoba.
Mara nyingi napenda kusafiri jioni au asubuhi sana.

Hizo route nilizozitaja hapo juu hazina Magari madogo mengi usiku, zaidi ya malori na mafuso. So huwa hatujui mambo ya ligi kabisa.

Kuna hii route ya Arusha-Dar na ligi huwa inaanzia pale Njia panda ya Himo, wakuu kuna watu wanapenda kushindana sana, kwenye barabara.

Juzi kati hapa tumetoka Arusha kwenda Dar tulivyofika Pale Njia Panda ya Himo, kulikuwa kuna gari kama tatu ndogo, Mark x nyeupe, Murano moja nyeusi na Alphad ya Silver, plan niliyokuwa nayo nikupoteza muda pale Njia Panda, at least usumbufu upungue barabarani kumbe zile gari zilikuwa zinatafuta abiria wa Dar, mimi kwenye gari ninayoendesha tulikuwa watatu. Sikuwa na wazo la kuchukua abiria.

Ilivyofika saa kumi na mbili kama na nusu hivi yule jamaa wa Alphad akang'oa, baada ya kama dakika kumi, Mark X akang'oa.
Hapo nimepaki upande wa pili wa barabara.

Ukapita tena muda kidogo Murano akang'oa...Tukamaliza mambo yetu tukaanza kuondoka, nilijua nikipiga mashine vizuri nitaenda kuwatoa kabla hata hawajafika Same!!
Tumeanza kutembea sio kwa speed kali hiyo jioni jioni ya saa moja bado watu ni wengi barabarani na mibasi + magari makubwa mengi yakitoka Dar kuja Moshi, Arusha.

Haikuchukua dakika nyingi saana kufika Mwanga, nikaiona ile Murano ndio inaondoka, nikajua labda alikuwa anaongezea abiria, nikawa nimempita mbele kabla ya Kisaranga nikaipita na ile Mark x, Alphad sikuiona. Giza linazidi kuongezeka naona na barabara inapungua jam.

Tumepita Lembeni kwenye Kivuko cha treni jamaa wa Mark X akaovertake kwa speed kali kuianza Tambarare flan hivi kuelekea Same, hapo ndio ikawa shughuli hakuniacha mbali sana, kabla ya sehemu inaitwa mgagao Murano akaniovertake akaenda akaovertake na mark x..

Baada ya Murano kunipita nikagundua Mark X kaongeza speed zaidi kwasababu alianza kuniacha kwa mbali kidogo.

Nikagundua hawa watu kama vile wanafanya ligi hapo road, nikaamua na mimi kujihusisha nao, ule mtiti haukuwa wa kawaida Tukaanza kutembea sasa pita nikupite ikaanza, jamaa wa Mark X tulikuwa tunamuacha sana...

Mpinzani wangu mkubwa alikuwa jamaa wa Murano, hadi tunafika Korogwe, kwenye kona yakuelekea Old Korogwe, kuna beria, tukamkuta jamaa wa Alphad pale na gari nyingine ndogo mbili, zote zinaenda Dar, ebwana eeh kama ni ligi ndio ilikuwa kama vile inaanza piga nikupige,

Jamaa walikuwa wanatoa changamoto sana, hata kusinzia huwezi muda wote unawaza kumtangulia aliyeko mbele yako na kutokukubali aliyeko nyuma yako akupite! Huu mfumo ulifanya tukafika Dar mapema sana! Huu utaratibu wa Ligi kwenye hii barabara sijui kama ni wa kila siku, Kuna mashindano sana.

Ni barabara yenye ligi tena matata sana.
Kuna MwanaJf anayependa ligi barabarani, share na sisi.
kumbe ndio maana magari madgo yanapata sana ajali wkt wa usiku nimeshajua ni ligi ndio linawamaliza vijana wengi na ujinga mwingi sasa hapo mngetoana meno csa ivi mngekuwa mnaonewa huruma dah
 
Takwimu zinaonesha magari madogo yanaongoza kwa ajali, yamezidi hata bodaboda! Tulikuwa tunasema bodaboda ni wavuta bangi na wanywa viroba sasa inaonesha madereva wa magari madogo ni zaidi ya bodaboda.
 
Takwimu zinaonesha magari madogo yanaongoza kwa ajali, yamezidi hata bodaboda! Tulikuwa tunasema bodaboda ni wavuta bangi na wanywa viroba sasa inaonesha madereva wa magari madogo ni zaidi ya bodaboda.
Mimi barabara niliyokuwa napita kila siku (kuanzia Tegeta mpaka Posta) hukosi kuona ajali. Tena nyakati zile napenda club na kutoka karibia na alfajiri nisipokuta ajali njia panda kawe itakuwa Africana au njia panda Kunduchi. Tumepoteza Watu wengi sana na kusababisha ulemavu.

Jamani hizo speed za 140 kimbizeni mkiwa kwenye misafara ya Pm au Rais. Hakuna barabara hiyo Bongo kwa maana ya madereva makini, kusipokuwa na wanyama na Binadamu wanaovuka hovyo, uimara wa magari, barabara zisizokuwa na 'mawimbi' na pot holes nk.
 
Wewe ndio unajifanya mjuaji wakati watu umetaja fani zetu kwa kuwalisha watu matango pori!!

Ivi umenielewa kwanza nilichoongelea??
Tatizo lako unakuja kuanzisha ubishi bila kujua unabishia kitu gan
Ok ngoja nikueleweshe maana we mgumu kuelewa
Ninachosema magari yanatofautiana odometer kuringangana na nchi inayotokea, engine za magari hasa v8 na v6 ni zilezile, nikimaanisha nyingi hutengenezwa sehem moja na uwezo ni uleule, ila katika odometer kwa sheria za japan, ukizidisha ikasoma juu zaidi ya 180kmph lazima ulipie hiyo model, na kadri unavyoweka juu zaidi ndo unailipia zaidi, nikimaanisha anaeweka 260km/h analipia zaidi ya ataeweka 220km/h
Kuna aina za subaru zimelipiwa na sio kuwa haziwez zikaenda zaidi ya apo
Nchi kama ujeruman hawana speed limit
Na upande wa kushoto wa barabara zao hutakiwi kuendesha kama unaendesha speed ndogo, kule ukifika ata 400km/h hizo barabara we endesha tu kifo ni chako, ndo maana magari yao yana odometer zinazosoma speed ya juu ambazo hazifikishi

Tukirudi kwenye magari ya magazeti, yale ni wananunua special yenye speed kubwa, pale mwananchi mfano kuna isuzu mistubish flan hivi ziliingia mwaka juzi zenye speed adi 240,

Na kuna friend wangu mwenye ZX VX yenye engine ya v8 yenye odometer ya 180kmph, sio kuwa haina uwezo wa kuzidisha apo sema wameiwekea speed limit ya 180, na gari zenye engine hiyohiyo za ikulu zina 280kmph, apo ni kuwa za ikulu zilitoka kiwandani zikiwa special za ikulu, ila sie tunanunua magari kwenye soko la wajapani

Na kama tanzania tungekuwa tunatengeneza magari, basi serikali yetu ingekiamuru kiwanda kiwekee magari ya kawaida speed ya 110km/h magar madogo na 80km/h kwa malori na mabasi

Kama hujaelewa basi
 
Kwani tatizo ni 100 ? Tatizo barabara . Unakimbia 100 kwa sekunde tuu mkuu mfano rahisi huwez toka bunju mpaka posta ukapata sehemu utembee 100 hata kwa dakika 1. Bisha????? Njee mjini hakuna tatizo hata 150 safi kabisa. Mfano nakumbuka kuanzia tangibovu pale mpaka makumbusho hapo barabara iko ovyo saana mfano pale kwa komba unaposhuka kile kilima.. makongo pale unaweza toka njee ya barabara eti🤣

Yeah, barabara hyo sehem kubwa ni mbovu na matuta ya kijinga kutokana na ubovu, ila kiukweli barabara hyo kutembea kwa speed zaidi ya hyo ni kujipotezea mafuta maana brake utashika sana
 
Ushasema ni ya kawaida halafu ni special?
Hebu nioneshe Toyota hiace yenye 240 na Coaster yenye 240

Aahh mkuu apa nimekupata ulicho maanisha sahv, inaonesha kutokana na wengi unaowajua wanatumia hiace na coaster kusafirisha magazeti

Mi naowajua wanatumia isuzu pickups
 
Mimi barabara niliyokuwa napita kila siku (kuanzia Tegeta mpaka Posta) hukosi kuona ajali. Tena nyakati zile napenda club na kutoka karibia na alfajiri nisipokuta ajali njia panda kawe itakuwa Africana au njia panda Kunduchi. Tumepoteza Watu wengi sana na kusababisha ulemavu.

Jamani hizo speed za 140 kimbizeni mkiwa kwenye misafara ya Pm au Rais. Hakuna barabara hiyo Bongo kwa maana ya madereva makini, kusipokuwa na wanyama na Binadamu wanaovuka hovyo, uimara wa magari, barabara zisizokuwa na 'mawimbi' na pot holes nk.
Ni kweli mkuu.
Kukimbia inategemea sana na aina ya barabara na namna unavyoijua.
Niseme tu magari madogo usiku yanakimbia sana.
Juzi jumapili kuna mtu nilienda nae airport Kia from Moshi town ilikuwa kama saa kumi kasoro alfajiri, alinipita jamaa akitokea Arusha kwa haraka haraka alikuwa kwenye speed ya 200km/hr.
Kwasababu alivyonipita siku mwona tena...

Watu wanakimbia sana.
 
Takwimu zinaonesha magari madogo yanaongoza kwa ajali, yamezidi hata bodaboda! Tulikuwa tunasema bodaboda ni wavuta bangi na wanywa viroba sasa inaonesha madereva wa magari madogo ni zaidi ya bodaboda.
Duuh
 
Back
Top Bottom