Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Hii tabia ya kudharau simu za Tecno itakwisha lini?

Kuna dogo mmoja (mhasibu) ameajiriwa mwaka jana anatumia simu ya 800k anajiona mjanja sana kila anaomba lift kwenda kazini na anaishi nyumba ya kupanga.

Watu wanaiga tu maisha, nunua simu huku ukijua matumizi yake na faida yake hasa. Unanunua simu ya 1.5m lakini matumizi yako na anatumia simu ya 150k sawa sasa maana yake nini?

Fanya matumizi makubwa ukishapata fedha za kutosha sio una ka mshahara ka 1.2m unababaika kununua simu ghali. Vijana mtakufa masikini
Mimi simshangai huyo kijana kwa sababu, simu ni mapenzi Kama ilivyo kwa magari, kuna mwingine mapenzi yake ni kuwa na gari nzito na mwingine kuwa na gari yenye nyepesi. Mfano huyu anapenda Toyota cruiser na huyu anapenda IST. Kwa iyo simu au gari sio utajiri ni kulizisha matakwa ya mtu.
 
Wabongo wanaoziponda Tecno na Huawei ndo hao hao wanaoziponda Passo na Vits na ndo hao hao wanaokwambia hawawezi kuishi sehemu kama Chanika au Mbagala. Ni watu flani wanaojiona so special and classic hivyo tuzoee tu kuishi nao ndo wameumbwa hivyo
✓Na ndio umesahau hawa watu ndio wanaishi kinondoni,sinza,masaki,Ubungo, mikocheni lakini wanakaaa kwy nyumba za wazazi wao waliopigania Uhuru. Mfano Lemutuuuuuuuzzzzzzz
 
Lenovo K5 Pro inauzwa less than 230k. Ina 64GB na Ram 4GB halafu ina processor ya snapdragon siyo takataka kama MTK ya tecno.
Hawajitangazi, ngumu sana hata kuwaza kwenda kununua simu ya lenovo... najua tu laptops zao zipo gado sana kwenye bei na uwezo
 
Smart phone 3 bora Dunia
1)iPhone
2) sumsung
3)Sony experia
NA hapo Sony na sumsung wanashinda
wangombania namba mbili

Smart phone za hovyo 3 Dunia
1)Tecno
2)Huawei
3)iflnix
Mimi sijawai kutumia simu ya smart ya kichina toka simu za kawaida kipindi hiko nilikuwa natumia Nokia sumsung blackberry hizo ndio simu zangu na Sasa natumia Sony kwa matumizi ya kawaida kwa sababu inabebeka na iPad tablet ni ya nyumbani
Mkuu bora ukae kimya tu Huijui Huawei wewe hakuna iPhone inayokalibia p40 pro
 
Waafrika alietuloga sijui alivuta Cha wapi[emoji35]
tapatalk_1590691370200.jpeg
 
Mkuu bora ukae kimya tu Huijui Huawei wewe hakuna iPhone inayokalibia p40 pro
[emoji769]Brand yoyote ya simu ya kichina hata kama ukiwasha inatoa dhahabu. Electronics devices ukitumia baada ya miezi 6 simu inakuwa kama ina mawenge ivi. Vifaaa vya kichina ni Tatizo kama ukubali ujatumia vitu vingi vya kichina uwezi kuelewa ninachoongelea
 
Aaaaaah mkuu ni kweli unachokisema mimi mwenyewe nilianza kutumia itel nikahamia Tecno lakini kwasasa natumia iPhone lakini sijawahi kumcheka mtu ujue watu tunapenda ufahari tu aiseee mimi natumia iPhone lakini inatumia chaji balaaaah mpaka naikumbuka Tecno yangu niliyomgawia mdogo wangu kwahiyo watu waelewe hayo sio maisha kama umejaliwa kutumia kampuni kubwa za simu sio sasa uvimbe wakati huna kitu.
 
Pole sana mkuu huna exposure ya nje ya nchi na wala hujui teknolojia.

Huawei ana simu kali na nzuri kuliko hayo mauchafu yako ya iphone na samsung

Vivo ana simu kali sana kama za nex , Teknolojia ambayo samsung na iphone bado, Hujatembea wewe na unategemea simu za kibongo bongo.

One plus series ni simu kali kuliko hizo samsung na iphone

Hebu jaribu kutembea kidogo.

Mimi binafsi siwezi beba simu ambayo kila mtu ana hiyo brand mfano samsung au iphone

Simu kama one plus 8 pro, Vivo nex dual screen, Huawei P 40 huwezi linganisha na takataka za samsung au iphone.

Wewe unanunua simu Tanzania, kuna simu hapa Tanzania haziletwi kutokana na umaskini wa watu ila mtandaoni unanunua.

Simu ya Vivo nex 1805 ya mwaka 2017 imeizidi hata samsung galaxy s10+ ya mwaka jana 2019
Umewah kuishika s10 au unawashwa s10 plus ndio habar ya mjin ile sio simu tena maanaa imevuka mipaka fingerprint password mpaka za macho iris na kasi ya internet ni balaa tupu lte only una stream tu hamna loading movie unadownloadinng kwa dk na feature kibao na kiswahili voice typing yaan ukiingia samsung lazima uizarau techno iphone nampa heshima yke ila sijawah miliki iphone
 
Techno waongo balaa kwenye maboksi utasikia camera 16MP kumbe 8MP intrrnal memory utasikia 4GB ukijaribu ingiza ata movie moja haiingii toka siku io sitaki techno kutugeuza sisi mashamba boi kwa kutuwekea maspecification ya uongo

TECHNO HAJITATHIMIN
 
Wapenda picha ndio wanahangaika ila kama unatumia whatsap kwaajil ya kazi tu tecno inatosha
 
Ishu ya Techno na iPhone ni mindset ya mtumiaji.. Ulimbukeni ni mzigo.😎
 
Hivi mtu unaanzaje kudharau kitu ambacho hukumchangia mtumiaji hata mbuni ili akinunue?
watu wanavuka sana mipaka kiasi wanaingilia uhuru wa simu za watu!! Wakinikuta mtu kama mimi ambae sipangiwi wakisema hicho hakifai mimi ndo nakikumbatia na kukitetea mpaka wataona aibu. Maamuzi yangu halafu mtu mwingine ayaingilie [emoji2] atajua ajui
 
Ukipata tecno inayotengenezwa na mchina halisi (mzalendo) utafurahi ila mchina koko utalia
 
Naskia tochi ya TECNO inawasha mishumaaa, inawasha jiko la gesi na kubabua mahindi, kinachotakiwa we washa tochi elekeza eno usika kwa dakika mbili tuuuu!! [emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom