Mkuu.Hivi tunaposema kwa mfano:
Nimekula WALI KWA KUKU au WALI NA KUKU, huwa tupo sahihi???
Wataalamu wa lugha tafadhali...
Mkuu.
Zote hizo mbili ni sahihi.
ya pili ni orodha.
ya kwanza ni masimulizi.
...halafu si unaelewa kuwa huwa ni sinia au sahani bonge na kipaja kimoja cha kuku?
Yaani wali pomoni, tele lakini mchuzi au mboga ni kijinofu kadogo!!! Mitaani kwetu...pengine wengi wangesema " uswahilini".
Pia ni sawa.Na tukisema: Wali kuku!
Nimependa maelezo yako. Good!
Mkuu.Nazani zote ni sahihi
Hivi tunaposema kwa mfano:
Nimekula WALI KWA KUKU au WALI NA KUKU, huwa tupo sahihi???
Wataalamu wa lugha tafadhali...
Kwa mtazamo wangu, zote zinaweza kuwa sahihi au sio sahihi kwa kutegemea unataka kusema nini hasa (kufikisha ujumbe gani) lakini kilicho dhahili ni kuwa hizo sentesi mbili hazina maana iliyo sawa!
Nimekula 'WALI NA KUKU': (ni kama unasisitiza zaidi aina ya vyakula ulivyokula) ingawa kwa usahihi zaidi ungepaswa kusema umekula 'wali na nyama ya kuku' (labda kama unakula kuku kama afanyavyo nyegere!). Kama kuna mtu jina lake ni Kuku (au hata kama unataka kumpa kuku ndege ubinaadamu kwa sababu maalumu), sentensi hiyo inaweza kuashiria pia wewe pamoja na huyo kuku mmekula wali mkiwa pamoja.
Nimekula WALI KWA KUKU: Kama kuna mtu jina lake ni Kuku, sentensi hiyo inaweza kuashiria pengine ulienda nyumbani kwa huyo Kuku na ukala wali. Lakini kwa matumizi ya kawaida, sote tunajua nyama ya kuku (kuku) hutumika kama kitoweo na kwa ajili ya kuliwa kwa pamoja na chakula kingine (wali, ugali etc). Katika muktadha huu neno kuku naona linabeba dhana ya kitendeo kwa maana kuwa ungewea kula wali wako kwa kutumia (pamoja na..) maharage, nyama, mlenda nk.
Mkuu
Uchambuzi wako umenichekesha sana...wacha utani bwana....inafaa sana hii katika utani.
Na hiyo red Search Results for 'dhahiri' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'dhahiri' | The Kamusi Project
Kwenye rangi hapo, neno sahihi ni nadhaniNazani zote ni sahihi
Ni kweli kabisa zote mbili zinaweza kuwa sahih, lakini katika mantiki ya kitendo cha kula, wakati tunaelewa kuwa kilichokusudiwa ni chakula gani na mboga/kitoweo gani vilivyoliwa na mlaji, inapendeza zaidi kutumia "na" ambayo ina maana moja tu "and" kuliko "kwa" ambayo ina maana nyingi "with, by, to...." hali ambayo inaweza kuleta utata.Kwa mtazamo wangu, zote zinaweza kuwa sahihi au sio sahihi kwa kutegemea unataka kusema nini hasa (kufikisha ujumbe gani) lakini kilicho dhahiri ni kuwa hizo sentesi mbili hazina maana iliyo sawa!