Hii salamu ya shikamoo imekaaje?

Hii salamu ya shikamoo imekaaje?

Huwa najiuliza maswali mengi, kwa ufahamu wangu mdogo najua salamu ni kujuliana hali baina ya watu

Ila napata mkanganyiko kwenye salamu kwa kutumia neno shikamoo maana naona halina maana ya kujua hali kwani ukisalimiwa shikamoo jibu ni marhaba, kwahiyo hata kama unatatzo utajibu marhaba

Mbaya zaidi yule anayekusalimia kama ni mtoto hapati haki yake ya yeye pia kujuliwa hali ila ataulizwa hujambo jibu lake lazima aseme sijambo awe na tatizo au asiwe na tatizo atajibu sijambo

Mimi naona salamu sahihi ni habari yako ,hiyo ndo inaleta uhalisia wa salamu ya kweli.

Soma pia
Nipo chini ya miguu yako!!
 
Back
Top Bottom