Hii pekee ipo Rwanda

Hii pekee ipo Rwanda

Habari wandugu!

Leo ndio narudi Tanzania nikitokea Rwanda kwa ajili ya likizo ya mapumziko kiukweli kuna mengi niliyoyaona na kujifunza nikiwa Rwanda ila nafurahi maana mengi ni mazuri.

Suala la usalama hilo liko wazi kwa kila mmoja Rwanda ndio nchi pekee ambayo nimetembea usiku mnene na Polisi akawa ananifuata nyuma mpaka nikaingia lodge ndo akarudi bila hata kuniharass wala kunisemesha. Mfumo wao wa doria ni hatari sana. Wanakuwa askari kadhaa kwenye Gari then wengine wanatembea kwa miguu wakiachiana hatua kama tano tano single file. Ajabu guest niliyofikia kulikuwa na makahaba wengi jirani yake pamoja na kapub ila polisi wanawalinda kwa adabu na nidhamu kubwa.

Rwanda ndio nchi pekee ambayo pombe yake maarufu Primus inaujazo mkubwa sana hivyo ni kawaida sana mtu akakusalimia na akapiga funda kadhaa then akaondoka, nimeona wapenzi wengi wakishare liprimus limoja na hakuna shida. Hii imeongeza umoja na upendo miongoni mwao yaani Rwanda kuna love mpaka unaogopa sijui sababu wana makovu ya chuki na vurugu ndo maana wanaheshimu sana amani. Upendo na kuheshimiana pia kuvumiliana maana nimetembea kwenye bar na pub sijakuta watu wakirushiana maneno makali au kupigana hapana! Its peace!

Rwanda ndo nchi pekee ambayo salam ya hi! Jibu lake ni fine!

Rwanda ndio nchi pekee ambayo mji mkuu kila mtu anamjua mtu Fulani. Watu almost wote wanajuana mji mkuu.

Rwanda ndio nchi pekee ambayo idadi kubwa ya raia anavaa nguo zinazofanana na za kijeshi na hakuna noma iwe kofia pekee, au suruali, au shati au hata buti na hakuna police wala mjeshi anaehoji wazee wa usalama hawana maneno wao ni ulinzi tu kwa kwenda mbele.Kuna time nlikutana na jamaa mchana kuanzia cap mpaka boot ni la jeshi afu jamaa anauza vocha stendi ya bus. Ahahahaha.

Rwanda ndio nchi pekee ambapo Polisi na jeshi wanashika doria za usiku na mchana.

Rwanda ndo nchi pekee ambapo polisi wana aina moja ya uniform kwa askari wote.mf hapa bongo yaani FFU, askari wa kawaida, traffic, wote wawe na sare moja.

Rwanda kigali ndio mji mkuu pekee ambao sijaona mfuko wa plastic wala karatasi imezagaa barabarani.

Rwanda ndo mji pekee east Africa ambapo diamond yuko celebrated than local artist wa pale. Wale wasiojua kiingereza pale Rwanda wanaamini diamond platinum ni neno la kiswahili. Nimeenda club kadhaa na kila club ilipiga nyimbo za diamond zaidi ya nne tofauti na wasanii wengine. Ilifika time nikang'oa mpaka demu mkali wa kitutsi kwenye club moja VIP kwa kiki la kwamba diamond ni jirani yangu pale Dar ilhali ukweli nakaa Mwanza, nyegezi.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambapo wimbo wa pressure wa afsa kazinja na banana upo kwenye chati na unapigwa kwenye baadhi ya bar na pub hapa mjni Kigali.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambapo magodoro yake yamewekewa "plastic cover" sijui hata ni kwa sababu gani, mtanisaidia tafadhali wandugu.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambao nimekutana na mwanamke na nikamwambia wewe ni mrembo saana afu akajibu "urakoze" afu akaunga stori nyingine like its normal then that's it. Nahisi Washaambiwa saana we ni mrembo ndo maana hawashangai tena kuambiwa warembo. Daamn!

Rwanda ndo mji pekee ambao ukiagiza ugali na nyama utaletewa ugali na kongoro...ahahaha!

Kwa ujumla sijajutia likizo yangu Rwanda.
Hahaaa Kaka umetisha.Tutajonea huko.Asante.
 
1473192730733.png
1473192771415.png
1473192888672.png
1473192923752.jpg
1473192948075.png
1473192973805.png
1473193016808.png
Kigali-Rwanda
 
Vipi ulikutana na wale wajeshi walioua Watanzania wale wa Bukoba....wanaongoza kwa.....

i wanna visit there... ila Mbona hujatoa Onyo lolote huko maana am sure ukikosea kitu kule sidhani kama utarejea salama even your dead body sijui...

Ndege zao na zetu zipi nzuri? na wao wana mapangaboi kama yetu?
 
ONYO: Ukiwa Rwanda usijaribu kuzungumzia kwa kukosoa muundo wa uongozi, siasa na mambo yote ya ki usalama.

1473196994610.jpg
1473197002216.jpg
1473197060533.jpg
1473197094266.png
 
Habari wandugu!

Leo ndio narudi Tanzania nikitokea Rwanda kwa ajili ya likizo ya mapumziko kiukweli kuna mengi niliyoyaona na kujifunza nikiwa Rwanda ila nafurahi maana mengi ni mazuri.

Suala la usalama hilo liko wazi kwa kila mmoja Rwanda ndio nchi pekee ambayo nimetembea usiku mnene na Polisi akawa ananifuata nyuma mpaka nikaingia lodge ndo akarudi bila hata kuniharass wala kunisemesha. Mfumo wao wa doria ni hatari sana. Wanakuwa askari kadhaa kwenye Gari then wengine wanatembea kwa miguu wakiachiana hatua kama tano tano single file. Ajabu guest niliyofikia kulikuwa na makahaba wengi jirani yake pamoja na kapub ila polisi wanawalinda kwa adabu na nidhamu kubwa.

Rwanda ndio nchi pekee ambayo pombe yake maarufu Primus inaujazo mkubwa sana hivyo ni kawaida sana mtu akakusalimia na akapiga funda kadhaa then akaondoka, nimeona wapenzi wengi wakishare liprimus limoja na hakuna shida. Hii imeongeza umoja na upendo miongoni mwao yaani Rwanda kuna love mpaka unaogopa sijui sababu wana makovu ya chuki na vurugu ndo maana wanaheshimu sana amani. Upendo na kuheshimiana pia kuvumiliana maana nimetembea kwenye bar na pub sijakuta watu wakirushiana maneno makali au kupigana hapana! Its peace!

Rwanda ndo nchi pekee ambayo salam ya hi! Jibu lake ni fine!

Rwanda ndio nchi pekee ambayo mji mkuu kila mtu anamjua mtu Fulani. Watu almost wote wanajuana mji mkuu.

Rwanda ndio nchi pekee ambayo idadi kubwa ya raia anavaa nguo zinazofanana na za kijeshi na hakuna noma iwe kofia pekee, au suruali, au shati au hata buti na hakuna police wala mjeshi anaehoji wazee wa usalama hawana maneno wao ni ulinzi tu kwa kwenda mbele.Kuna time nlikutana na jamaa mchana kuanzia cap mpaka boot ni la jeshi afu jamaa anauza vocha stendi ya bus. Ahahahaha.

Rwanda ndio nchi pekee ambapo Polisi na jeshi wanashika doria za usiku na mchana.

Rwanda ndo nchi pekee ambapo polisi wana aina moja ya uniform kwa askari wote.mf hapa bongo yaani FFU, askari wa kawaida, traffic, wote wawe na sare moja.

Rwanda kigali ndio mji mkuu pekee ambao sijaona mfuko wa plastic wala karatasi imezagaa barabarani.

Rwanda ndo mji pekee east Africa ambapo diamond yuko celebrated than local artist wa pale. Wale wasiojua kiingereza pale Rwanda wanaamini diamond platinum ni neno la kiswahili. Nimeenda club kadhaa na kila club ilipiga nyimbo za diamond zaidi ya nne tofauti na wasanii wengine. Ilifika time nikang'oa mpaka demu mkali wa kitutsi kwenye club moja VIP kwa kiki la kwamba diamond ni jirani yangu pale Dar ilhali ukweli nakaa Mwanza, nyegezi.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambapo wimbo wa pressure wa afsa kazinja na banana upo kwenye chati na unapigwa kwenye baadhi ya bar na pub hapa mjni Kigali.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambapo magodoro yake yamewekewa "plastic cover" sijui hata ni kwa sababu gani, mtanisaidia tafadhali wandugu.

Rwanda Kigali ndo mji pekee ambao nimekutana na mwanamke na nikamwambia wewe ni mrembo saana afu akajibu "urakoze" afu akaunga stori nyingine like its normal then that's it. Nahisi Washaambiwa saana we ni mrembo ndo maana hawashangai tena kuambiwa warembo. Daamn!

Rwanda ndo mji pekee ambao ukiagiza ugali na nyama utaletewa ugali na kongoro...ahahaha!

Kwa ujumla sijajutia likizo yangu Rwanda.
TANZANIA pia ni nchi pekee ambayo ukifeli form 4
Unaenda CHUO KIKUU.
 
..Si yeye ndio ametembea hadi hapo sasa wewe usimseme kaongeza chumvi..jamaa anayosema ni kweli!kumbuka Congo ina waasi pia wana uniform zao mzee...hakuna chumvi yupo sawa tu!
Waasi wana uniform zao zipi?

Hilo la uniform sio kweli, DRC na Burundi Askari wote ukitoa wanajeshi tu wanavaa uniform zinazofanana
 
..hiyo ndo tofauti sasa"kikoti cha reflector tu"
Hata Rwanda wanavaa hivyo vikoti wakiwa barabarani, naongea kwa experience mkuu, Rwanda, DRC Na Burundi Police wao wanavaa sawa yaani nguo za Dark blue na hao trafic huwa wanaongeza hivyo kikoti vyenye reflector
 
Kwa kuongezea tu:
Kigali ndio mji pekee ambapo Askari polisi/wanajeshi wanapokua patrol iwe ya mchana au usiku wanajihami kwa silaha na radio call kama wako vitani frontline tena porini. Na hawakai chini au kwenye viti.

Gisenyi-Rwanda ni mji pekee duniani ukiongea kiswahili cha kitanzania watu hudhani wewe ni mwanajeshi. Na kama wewe unapenda mademu unawapata kirahisi bila kutumia gharama kubwa.

Kigali-Rwanda ni jiji pekee Africa ambapo mwizi hawe kuiba na kukimbia zaidi ya mita 100 bila kukamatwa akiwa hai au maiti.

Rwanda ni nchi pekee dunianiani ambapo raia wote wa nchi za Africa wanaingia bila viza.

Rwanda ni nchi pekee africa ambapo sheria za nchi zinaruhusu kila mwanandoa kumiliki mali alizochuma kabla ya ndoa na iwapo wataachana mali hizo mali hazimuhusu mwenza wake.
da interested cjui nkaoleee huko?
 
Back
Top Bottom