Hii ni kwenu nyie kina dada.

Jamani, thamani ya kitu utaijua pale unapokikosa:

Kabla hujamuoa huyo mkeo alikuwa kifaa ambacho hukuweza lala bila kumwona au msikia. Ushamweka ndani basi value yake imekwisha na kuanza kusaka barabarani wale waliobeba chupi mkononi.

Cha ajabu wewe mume unalalamiaka eti mkeo hakufanyii kama huyo kimada. Je WEWE UNAMFANYIA MKEO HAYO UNAYOMFANYIA KIMADA? Pengine huko unakuwa kama shamba boy.

Mimi ninauita huo ni ulimbukeni wa kujifanya mambo mnayaweza kumbe si lolote.
Mtahangaika saaana, mtaishia kufirisika na mtupwe nje kama mbwa aliyechoka.

Ngoja nikupe sifa chache
za nyumba ndogo:
1. hazitaki tenda ya jumla, ni rejareja tu , in that case hawataki majukumu ya kulea mume
(no commitments), just hit and run
2. Wanataka kuwa huru na wapo tayari kwa mwekezaji yeyote
3. Ukitereza kipesa kwake biashara imekwisha

In other-way tunaweza kuwaita CDs ambao ni home based, tofauti na wale wanojiuza barabarani.

Poleni sana WANAUME umnaodhani umnatafuta amani ya roho kumbe mnalikaribia kaburi.

USHAURI WA BURE
Penda mkeo, mfanyie mazuri yote, mkeo ni dhamana, fainali uzeeni.

Stay blessed



 
WENGINE WANAWAPA MALIMBWATA HAMFURUKUTI..
akili ya kimungu hamuwezi kufanya hayo.....

Mimi napinga kabisa hakuna cha LIMBWATA wala nini kule ni FULL MAUTUNDU na MAUFUNDI. Ndoa nyingi zimejaa ubize na katika yote mama ndiye anachoka zaidi. Sasa inapokuja kwenye suala la SEX wanawake wanakuwa tayari wameshachoka na shughuli za ndani kwa hiyo perfomance inakuwa chini. Mwanaume yeye akishaachana na shughuli zake huko yupo free yeye anakuwa bado na nguvu za ziada kumiliki GAME!

Nyumba ndogo zipo strategic kwa sababu zinatafuta LIFE SURVIVAL ni lazima zikukuruke kwelikweli kila staili na kila mtindo wa kimapenzi ili mradi mwisho wa siku mwanaume anakuwa ametekwa!
 
Mapenzi ndugu zangu hayana tofauti na mjasiriamali.Bila kuwa na ubunifu awe mke au mume utabaki kulalamika kuwa mwenzio kalogwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom