Hii ni dhahiri kuwa viongozi na wanachama wa CHADEMA hawana busara, huwezi kumuombea kifo mwenzako

Lema ni Mchaga mwenzangu ila kuna mambo huwa simkubali huyu mtu..

Mambo ya kumtabiria mwenzako kifo sijapenda.

Ila na wewe mtoa mada, jifunze kutofautisha msimamo wa Lema na msimamo wa chama chake. Hapo na wewe umekosea.. usiipake Chadema matope kwa maneno ya mtu mmoja.
Dede Mushi ako
 
Kumbe Mashekhe, wachungaji na mapadre wanapokuwa wanatuhimiza kutengeneza mambo yetu na Mungu (kutubu na kaucha dhambi), huwa wanatuombea kifo?

Isa 38:1

Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

yeye lema ana assurance kiasi gani kwamba hafi siku za karibuni!!!!

huyu anawadharau wafuasi wa chadema.
 
Mistari ya kuombea watu kifo?
Hii hapa mkuu!

Zaburi 109
1 Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze,

2 Kwa maana wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.

3 Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure.

4 Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa naliwaombea.

5 Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya upendo wangu.

6 Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.

7 Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.

8 Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine.

9 Wanawe na wawe yatima, Na mkewe na awe mjane.

10 Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao.

11 Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake.

12 Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa kuwahurumia yatima wake.

13 Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika kizazi cha pili.

14 Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya mamaye isifutwe.

15 Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.

16 Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamfisha mtu aliyevunjika moyo,

17 Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye,
 
Tengua kauli yako,mfano nasi tukisema viongozi na wanachama wa ccm ni wauwaji utaniunga mkono?mawazo na bensanane na wengine waliopotea....
Kuwa na busara
 
Hivi kufa nako ni jambo la kutabiri? Mbona inafahamika kila nafsi itaonja mauti. Hizi chuki za kisiasa mbona zinatuondolea ubinadamu.
 
Lema ni Mchaga mwenzangu ila kuna mambo huwa simkubali huyu mtu..

Mambo ya kumtabiria mwenzako kifo sijapenda.

Ila na wewe mtoa mada, jifunze kutofautisha msimamo wa Lema na msimamo wa chama chake. Hapo na wewe umekosea.. usiipake Chadema matope kwa maneno ya mtu mmoja.
hiyo kusema huyu ni mchagga mwenzako umeulizwa? kuendekeza ukabila ni ushenzi na upumbavu.keep it
 
Back
Top Bottom