Hii ndo tatu bora ya wagombea wa CCM

Hii ndo tatu bora ya wagombea wa CCM

Status
Not open for further replies.
CCM hamna tatu bora wala moja bora

Utamsifia mwanao wa kwanza darasani kwenye darasa ambalo wote wamepata F???

Utamsifia? Basi kama unampoza mwambie ukweli kuwa hongera kwa kuogoza wajinga wenzio
 
Lowasa utamchagua wewe lkn sio mtanzania mwenye akili zake timamu.hana jipya yani.


Mimi ni mmoja wa wasio na akili kwa utashi wako, ila nina muunga hoja victormztz. Kuwa lowassa ni mbora kuliko wote cc na ccm nzima.
 
Acha kuweweseka ww...Lowassa ndio mpango wa CCM...labda uko mbali sana na CCM insiders...as well labda hufautilii wanapokwenda kutafuta udhamini uone NGUVU ZAO KUKUBALIKA NA WANANCHI, Lowassa hata uunganishe wagombea wengine wooooote CCM hawafikii nusu ya Nguvu na influence za Lowassa kwa wananchi...!!

Kilichotufikisha mpaka hapo ni udhaifu wa serekali,vinginevyo Lowassa mpaka sasa angekuwa ana zunguka magerezani kutafuta udhamini kwa wafungwa wenzake ili aweze kuwa Rais wao.
 
bundewe hao ni kwa mujbu wa ndoto zako na inakubidi usali sala zote uombe wabaki hao. lakini kwa mujibu wa demokrasia iliyopo ndani ya chama chetu watapigiwa kura na watabaki watano watakaopelekwa mbele kupata jina moja
Kuna vyama ambavyo mgombea wao huamuliwa kwa maoni ya watu wachache wenye his a kubwa CCM si moja ya vyama hivyo kavisaidie vyama hivyo vingine kutoa maoni yako hayo
Vikao vitaamua kabsa nani anafaa kupeperusha Bender ya chama..
CCM siyo SACCOSS ya kisiasa..ushindi uko pale pale
 
uvccm na lb7 bwana maoni ya mtu mnaanza kulalama eti mnavuruga mchakato kwa kumtaja dr.slaa
 
Mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.

Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya msingi pekee lakini nao wamechukua fomu, kuna ambao wamejiuzulu kwa kashfa za wizi nao wamechukua fomu.

Maoni yangu ni kwamba peformance ya kiwango cha chini iliyooneshwa na rais aliyepo sasa imesababisha hali hii.

Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na CCM kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark Mwandosya,
2. Mwigulu Nchemba na
3. John Magufuli
,


Na huenda John Magufuli akawabwaga wenzie katika hatua hiyo na kupewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM. Mpambano kati ya Dr. Magufuli na Dr. Slaa utakua na msisimko wa aina yake.

Tupia maoni yako, unadhani ni nani wana nafasi ya kupitishwa na CCM?


1.Sumaye
2.muhongo
3.Mwigulu.
 
Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na CCM kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark Mwandosya,
2. Mwigulu Nchemba na
3. John Magufuli
,

Hivi wewe unadhani hii ni Tanganyika? Wazanzibari watakuponyesha usipowaingiza kwenye tatu bora?
Mwaka huu wanaweza ingiza Mtanganyika mmoja (mwanaume), Mzanzibari mmoja (mwanaume) na mwanamke mmoja (anaweza toka upnade wowote).
 
Huyu atashindwa kupitishwa kwa kigezo cha elimu tuu, lakini sidhani kama anayo kashfa yeyote ya kimaadili kama hao uliowataja.
View attachment 259125

Do not take things for simplicity, anaweza akawa na kashifa sana kwa level yake pale kijijini! Akija huku juu kwa urais atakuwa na kashifa kwa level ya juu kama hawa wa CCM walio juu!
 
mkoa wa kigoma una watu wa maajabu!!!
hii ni ajabu nyingine baada ya zitto na kabour

You sound like a tribalist. What is so strange was done by Kabourou and Zitto that have not been done before?
 
Inatia raha sana kuona wana CHADEMA wakiwa makini kujadili safu ya watangaza nia wa CCM!

Jamani, huko UKAWA mna Lipumba na ametanga nia tayari, kwanini msimjadili huyo!?!
 
Haaahaa, huyo Mpina atukuwepo katika kumi bora mambo ya fainali atafungulia TV atazame wenzie..
Mpina, Lugora, Sumaye Bulaya na wachache wengine ni viongozi wakweli, waadilifu na wenye uwezo mkubwa. Tatizo ni kwamba Kimwili, fikra, maatendo, maongezi na matamanio ni WANAUKAWA ila wana roho ya Woga na ndio bado wanaogopa kuchukua hatua sahihi!. Wanaogopa kesho! Si wajasiri kwa kuitendea nchi haki kama wanavyobwabwajika kwenye majukwaaa haswa bungeni. Kama wanathubutu waje UKAWA tutawapa kwanza ubunge kisha tuwachemshe watapike roho ya Woga na baada ya 5-10 yrs watakuwa watu wakubwa sana. Vinginevyo watazeeshwa kama Malechela na Mrema bila kuona ndani. CCM Mwaka huu tayari wana agenda ya siri ya ushindi, Wanataka kuja na hoja ya " mwaka huu ni Mzanzibari au Mwanamke" na wenye akili zetu tunamwona Dr. Shein au Migiro. Wengine wape pole.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom