Kama wana CCM watampitisha Lowasa itadhirisha kuwa ni chama ambacho hakina nia ya dhati kuwakomboa watanzania kutoka kwenye lindi la umasikini linalo sababishwa na rushwa, ufisadi, mmomonyoko wa maadili na mengine mengi. Lowasa alipokuwa waziri mkuu alitumia madaraka vibaya hata akajianzishia Richmond, akiwa waziri wa kilimo na mifugo alijimilikisha sehemu ya mbuga. Je akiwa rais atatuacha ? anahubiri ajira kwa watanzania ili hali BOT akiwa waziri mkuu alijaza nafasi kwa watoto wa vibopa. Tanzania tusitegee rais bora kutoka CCM, CCM kwa sasa wamechoka hata akitokea mtu tunaeamini atafanya kazi vizuri atabanwa na mfumo mbovu wa CCM