Hii ndo tatu bora ya wagombea wa CCM

Hii ndo tatu bora ya wagombea wa CCM

Status
Not open for further replies.
Huyu atashindwa kupitishwa kwa kigezo cha elimu tuu, lakini sidhani kama anayo kashfa yeyote ya kimaadili kama hao uliowataja.
View attachment 259125
Wana Kigoma noma, huyu jamaa anajuwa elimu yake hairuhusu kugombea urais lakini yumo tu, kama vile aya.atol.lah komeni anavyojuwa umri wake haumruhusu lakini bado anataka urais!
 
Hivi wewe unadhani hii ni Tanganyika? Wazanzibari watakuponyesha usipowaingiza kwenye tatu bora?
Mwaka huu wanaweza ingiza Mtanganyika mmoja (mwanaume), Mzanzibari mmoja (mwanaume) na mwanamke mmoja (anaweza toka upnade wowote).

Uko sahihi kaka, maana siku hizi hatuangalii uwezo bali kuibalance gender, dini na pande za muungano
 
Acha kuweweseka ww...Lowassa ndio mpango wa CCM...labda uko mbali sana na CCM insiders...as well labda hufautilii wanapokwenda kutafuta udhamini uone NGUVU ZAO KUKUBALIKA NA WANANCHI, Lowassa hata uunganishe wagombea wengine wooooote CCM hawafikii nusu ya Nguvu na influence za Lowassa kwa wananchi...!!

Ndugu yangu. Lowassa hatafika kwa wananchi kwa tkt ya ccm hata angekua na nguvu kama za Maywether, labda kwa wananchi atafika kwa tkt ya ACT. Kamuulize J. Malecela alichofanyiwa. Hao 'wanaomkubali' sio wananchi, ni vikundi vya wana ccm. Upinzani watapata urahisi sana wa kupiga kampeni dhidi ya Lowassa kuliko hata huyo jamaa wa std 7
 
LOwassa asipoingia 3 bora CCM ijiandae kuzikwa Rasmi ... Kashfa za Kipuuzi zisitunyime Rais Bora ..
 
Hotuba ya Mwigilu inasifiwa kubwa ni nzuri kuliko watangaza nia wengine wa CCM, ile hotuba iko too theoretical, haina uhalisia wowote, mambo aliyoyadadavua kada huyu ni magumu sana kuwa implemented na serikali yake ya CCM, ni kama ame - copy na ku-paste hoja za Wapinzani - kifupi ile ni hotuba ya vitabuni (madesa) - alichofanya huyu mtangaza nia ni sawa na kufurahia radha ya chakula mdomoni wakati inakwenda kukuvuruga tumboni.

Kwangu mimi siwezi kumweka kwenye best 3 za CCM so far.
 
Mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.

Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya msingi pekee lakini nao wamechukua fomu, kuna ambao wamejiuzulu kwa kashfa za wizi nao wamechukua fomu.

Maoni yangu ni kwamba peformance ya kiwango cha chini iliyooneshwa na rais aliyepo sasa imesababisha hali hii.

Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na CCM kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark Mwandosya,
2. Mwigulu Nchemba na
3. John Magufuli
,


Na huenda John Magufuli akawabwaga wenzie katika hatua hiyo na kupewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM. Mpambano kati ya Dr. Magufuli na Dr. Slaa utakua na msisimko wa aina yake.

Tupia maoni yako, unadhani ni nani wana nafasi ya kupitishwa na CCM?

Itavire, Itavire, Itavire
 
Kati ya vitu vilivyonisikitisha katika mchakato wa uchukuaji fomu za kuelekea Magogoni mwaka huu wa 2015, ni kitendo cha Ofisi ya CCM Makao Makuu kuchukua fedha za mwananchi wa Kigoma (Tshs. 1,000,000.00) wakati tayari walishaweka vigezo 13 na kimojawapo kikisema mgombea lazima awe na elimu kiwango cha chini iwe ni Chuo Kikuu au elimu inayoendana na kiwango hicho.
Ushauri wangu Chama kimrejeshee fedha yake kwa nia njema tu, kwani inaonekana walipiwa pande zote mbili(Waandaa vigezo na mchukua fomu), labda kama vigezo vile vilitajwa kumaanisha kitu kingine. Nachelea kusema huu sasa ni utapeli
 
mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.

Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya msingi pekee lakini nao wamechukua fomu, kuna ambao wamejiuzulu kwa kashfa za wizi nao wamechukua fomu.

Maoni yangu ni kwamba peformance ya kiwango cha chini iliyooneshwa na rais aliyepo sasa imesababisha hali hii.

Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na ccm kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark mwandosya,
2. Mwigulu nchemba na
3. John magufuli
,


na huenda john magufuli akawabwaga wenzie katika hatua hiyo na kupewa fursa ya kupeperusha bendera ya ccm. Mpambano kati ya dr. Magufuli na dr. Slaa utakua na msisimko wa aina yake.

Tupia maoni yako, unadhani ni nani wana nafasi ya kupitishwa na ccm?

katiba ya tanzania inaruhusu kila mtu kutoa maoni so uko sawa kabisa kiongozi,ila rais ndo hivyo tena ni lowasa
 
Kama akipitishwa magufuli angalau anaweza kuondoa uozo serikalin pia uwajibikaji endapo hatatekwa na mafisadi
 
Serikali hii inahitaji kiongozi mwadilif na pia awe na asili ya udicteta mambo yatasonga maana mtanzania bila kufokewa hawajibiki wengi hujisahau wanapopew nyadhifa maofisini ,na kufanya kaz kwa mazoea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom