maatope
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 1,422
- 958
Yes,kumbe na wewe uko team jangala,safi sanaJamani tusimsahau na mzee Jangala
Yes,kumbe na wewe uko team jangala,safi sanaJamani tusimsahau na mzee Jangala
Hakuna kazi ngumu kama kutabiri top 3 ya CC ya CCM.
Mpaka kufikia jana jioni tar. 10/06/2015, takriban wanachama 29 wamechukua fomu au kutangaza nia ya kugombea urais wa nchi hii.
Hii ni idadi kubwa sana ya watu kutangaza kutaka urais wa nchi yetu, nadhani kiti cha rais sasa kimeonekana cha kawaida sana, kiasi kwamba kuna ambao wana elimu ya msingi pekee lakini nao wamechukua fomu, kuna ambao wamejiuzulu kwa kashfa za wizi nao wamechukua fomu.
Maoni yangu ni kwamba peformance ya kiwango cha chini iliyooneshwa na rais aliyepo sasa imesababisha hali hii.
Kwa maoni yangu, kati ya wote waliokwishacukua fomu au kutangaza nia; watu watatu wanaoweza kupitishwa na CCM kufikia fainali (mkutano mkuu) ni
1. Mark Mwandosya,
2. Mwigulu Nchemba na
3. John Magufuli,
Na huenda John Magufuli akawabwaga wenzie katika hatua hiyo na kupewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM. Mpambano kati ya Dr. Magufuli na Dr. Slaa utakua na msisimko wa aina yake.
Tupia maoni yako, unadhani ni nani wana nafasi ya kupitishwa na CCM?
Hakuna kazi kama ambao wana ahueni kwenye kashfa za rushwa na ufisadi ni Mwandosya na Mahiga hawa wanaweza kupitishwa, wakitaka kurudia uchafu uliofanywa 2005 na Kikwete na mtandao wake ambapo mabilioni ya pesa za kifisadi yalihongwa kwa wajumbe hakuna wa kushindana na fisadi Lowassa na fisadi Magufuli.
Acha kuweweseka ww...Lowassa ndio mpango wa CCM...labda uko mbali sana na CCM insiders...as well labda hufautilii wanapokwenda kutafuta udhamini uone NGUVU ZAO KUKUBALIKA NA WANANCHI, Lowassa hata
uunganishe wagombea wengine wooooote CCM hawafikii nusu ya Nguvu na influence za
Lowassa kwa wananchi...!!
mkoa wa kigoma una watu wa maajabu!!!
hii ni ajabu nyingine baada ya zitto na kabour
Mkuu sipingi mtizamo wako lakini umetumia kigezo kimoja tu, nchi kila mtu ni fisadi ila tunatofautiana viwango na umaarufu. Hata kwa kigezo hicho bado kupata top 3 ni ngumu maana wapo wengi nao (6, mwezi wa kwanza, mwigulu et al)
Hao uliowaweka kwenye brackets kwa maoni yangu hata kwenye top 5 hawastahili kuwemo, kwa kifupi ni kwamba ni lazima MACCM wampitishe mgombea wao kutoka kwenye huu utitiri kama tukiangalia sifa za kiongozi bora wa kuliongoza Taifa letu katika huu utitiri hakuna hata mmoja. Wote hawa walikaa kimya wakati nchi inaangamia kwa mika kumi ili kulinda maslahi yao ya siku za usoni badala ya yale ya Tanzania na Watanzania na hivyo kuacha ufisadi ukishamiri, rushwa ikishamiri, ujangili ukishamiri, utendaji na uongozi mbovu ukishamiri n.k. hadi kufikia nchi kutoswa na Wafadhili. Walikuwa wapi wote hawa kwa miaka kumi huku nchi ikiangamia!? Mbona hatukuwasikia kukemea madudu mbali mbali nchini yaliyofanywa katika kipindi hicho.
Ndo maana nilisema ni vigumu sana kutabiri top 3 ya ccm kutokana na sifa na sababu mbalimbali. Ulianza na ufisadi sasa umekuja na kufumbia macho mambo mengi. I still believe that the screening process isn't an easy job for cc
Lowasa the boss
This makes a lot of sense ukifuatilia siasa za kutafuta raisi na kauli za makada wenye nafasi za juu lakini si presidential aspirants na wanaowania kikubwa ni agenda ya kuvua gamba kama imeibuka tena.Kumbuka ile kauli ya Kikwete ya "kulivua gamba" kwa kutaka kuwafukuza CCM ""wachafuzi" wa CCM mafisadi Lowassa, Rostam, Chenge na wengineo wengi lakini baada ya kutishwa kwamba yeye akianza wao watamaliza na "Ikulu hakutalalika" kauli ile ikaanza kukimbiwa na wengine ndani ya CCM hata kukanusha kauli ile ilimaanisha nini. Ndiyo sababu nilihitimisha kwamba katika huu utitiri hakuna mwenye sifa hata mmoja ndio sababu wakajaribu tena kumshawishi SAS ili abadili msimamo wake na hata Augustino Ramadhan, ila hilo la CCM kuwa na mgombea wao ni lazima walikamilishe pamoja na kuwa kwenye huu utitiri hakuna anayestahili.