bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,146
- 2,803
Kuna mahali kwenye uso wa dunia ambapo mfumo wa GPS haupo, barabara zote zinatokomea, na sheria pekee iliyobaki ni ile ya kinyama: mwenye nguvu ndiye anayeishi, na mdhaifu anazikwa na matope.
Amini usiamini, eneo hili si la kufikirika lipo. Linalojulikana kama Darién Gap, msitu huu wa kutisha unaounganisha Colombia na Panama ni lango la jehanum iliyopo duniani. Kila mwaka, mamia kwa maelfu ya roho zilizokata tamaa kutoka pande zote za dunia Venezuela, Haiti, Cuba, hadi barani Afrika na Asia wanatumbukia kwenye giza hili nene. Wote wana lengo moja tu linalowaka mioyoni mwao: kufika Marekani, kutafuta maisha bora. Lakini kabla ya kuigusa ndoto hiyo, lazima kwanza wapitie kwenye tumbo la mnyama huyu anayekula wanadamu.
Ni siku tano hadi kumi za kutembea kwa miguu kwenye matope mazito yanayokula miguu hadi magotini. Hakuna barabara, hakuna magari, wala hakuna daktari wa kuokoa maisha. Mito ya eneo hili hufurika kwa sekunde chache bila tahadhari ikimeza watu mbele ya macho ya familia zao huku wakiwa hawana uwezo wa kufanya chochote zaidi ya kupiga yowe. Na kama maji hayajakuchukua, nyoka wenye sumu ya kuua kwa dakika chache na joto la kuchemsha ubongo viko tayari kumaliza kazi, ukiweka na wanyama wakali, wote wamo humo.
Lakini hatari kubwa zaidi msituni hapa haina wanyama wala sumu ina sura ya binadamu.
Darién Gap inamilikiwa na wanyama wa kibinadamu: magenge ya wauza dawa za kulevya na majambazi hatari kama vile Clan del Golfo. Watu hawa hawana huruma. Wanakubana njiani, wanakupora kila dola uliyonayo, na kuwafanyia kila wanacho ona wao sahihi kwao. Ukikosa fedha za kuwapa, maisha yako yanafikia kikomo hapo hapo, na mwili wako unaachwa ukitokota kwenye jua.
Saikolojia ya mwanadamu inasema ukweli mmoja wa kutisha: Mtu anapofikia hatua ya kutokuwa na cha kupoteza, hofu ya kifo inatoweka kabisa.
Watu hawa wameuza kila kitu nyumba za familia, mashamba, na mifugo ili tu kupata dola elfu chache za kulipa mawakala wa kuwasafirisha. Wanaingia msituni wakijua fika kwamba mmoja kati ya watu kumi hatatoka akiwa hai. Maji ya kunywa yasipopatikana, wanajikuta wakinywa maji ya mito iliyojaa miili ya wasafiri wenzao waliofia njiani. Wanatembea wakikanyaga mifupa ya wale waliozidiwa na uchovu au majeraha na kuachwa nyuma.
Katika Darién Gap, ukivunjika mguu au ukishindwa kutembea, huo ndio unakuwa mwisho wako. Hakuna wa kukubeba; kila mtu anapambania pumzi yake mwenyewe.
Na ukifanikiwa kuimaliza Darién gap, ukaingia Panama, omba MUNGU usiangukie kwa walinzi wa mipaka manake wakikukamata unarudishwa.
Na hata ukipokelewa, bado unasafari ndefu ya kuvuka nchi nyingi mpaka ufike Mexico, ambapo unaweza sota, Maisha yako yote na Marekani usiingie.
Marekani imekuwa nchi ambayo hata wale wanaowaponda Wazungu pia wote hupitia hapo hapo waking'ang'ana kufika, sio waraabu, sio waafrika, sio wahindi sio nani.
Bado, licha ya kutisha huku kote, maelfu wanaendelea kumiminika kila siku. Kwa sababu kwao, kubaki nyumbani kwenye umaskini uliokithiri, vita, na utawala wa kilaghai ni kifo cha polepole kinachowatafuna kila siku. Wanaona ni bora kukabiliana na majinamizi wa Darién Gap mara moja tu ili kupata hata nafasi ndogo ya asilimia kumi ya kubadilisha maisha ya familia zao, kuliko kubaki mahali ambapo matumaini yalishakufa zamani.