Mzee Moshi,
Heshima yako mkuu, hii serikali ya awamu ya nne inaendelea kuvinjari over wananchi wasioelewa wala kuuliza what is going on!,
(1). Hii serikali ina mipango kama MKUKUTA, TMTP 2020, MKURUBITA, MKUMBITA, yote yenye nia ya kuikwamua taifa na kulisogeza mbele katika maendeleo,
lakini ukweli ni kwamba hizo plan zote hazijapitishwa kisheria as they should, halafu mpaka leo serikali kuanzia za awamu ta tatu mpaka leo ya nne, hazijui gharama za kuendesha hiyo miradi, kwa hiyo ni njia tu nyingine ya kuwapa viongozi mlo!
(2). Wakati umefika kwa serikali kuutumia mfuko wa NSSF katika kusukuma maendeleo ya nchi, kama nchi nyingi za Asia na West zinavyofanya,
kwa mfano kitendo cha NSSF kununua Quality Plaza kwa zaidi ya shillingi Billioni 45, ni upumbavu wa hali ya juu mno kwani wataalamu mbali mbali walishatoa tathmini kuwa taifa letu linahitaji benki yenye mtaji wa Billioni 50 tu! ili kuendeleza maendeleo ya wananchi, kwani benki yetu ya maendeleo TIB leo ina mtaji wa shillingi Billioni 24.9, sasa ingepewa hizo Billioni 45 si ingepewa hiyo benki kwa ajili ya maendeleo ya taifa badala ya hiyo Plaza mabyo ni utata mtupu?
(3). Ukiangalia kwa makini kufutwa kwa kodi ya gesi, nia na madhumuni ni kuwapatia nafasi wakubwa wanaotumia majiko ya gesi kutolipa kodi kubwa,
masikini wote hutumia majiko ya mafuta ya taa ambayo kodi yake haikuondolewa, hivyo basi masikini ataendelea kulipa shillingi 52 za kodi ya mafuta ya taa kila wanaponunua lita moja, as opposed kwa wakubwa wanaotumia gesi!
(4). Ubinafsishaji, kwa mwaka 2005 peke yake mshirika 11 yaliuzwa, yakiwa na mali 126, hivyo katika miaka 13 iliyopita toka zoezi lianze mashirika 322 yenye mali 647 yameuzwa tayari,
lakini to this day serikali zote tatu hazijawahi kusema hadharani tathmini ya mafanikio ya huu mpango wa ubinfsishaji, je ajira imepungua au imeongezeka? Je wawekezaji katika mashirika yaliyonunuliwa wametimiza masharti ya serikali ya sheria ya bunge ya uwekezaji?
Vipi ATC imefikia wapi? Kwa nini serikali imeingia gharama za ajabu kulikwamua shirika hilo na kuyaacha mengine? Kwa nini tume ya kamati ya mashirika umefukuzwa kazi yote bila taarifa maalumu ya sababu yake?
(5). Mpaka leo serikali haijasema lolote kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Serikali, aliyesema kuwa Rushwa inachukua 30%, Ufisadi 20%, Mgongano wa masilahi 25%, kutojali sheria 25%, ya fedha za serikali, na CCM ikiwa inachukua sehemu kubwa ya pesa hizo kwa ajili ya mikutano yao?
(6). Kwa nini serikali ilinunua ndege ya rais kwa gharama ya shillingi Billioni 42, ambayo leo haitumiki tena? Hizo pesa zilikuwa zinatosha kabisa kuanzisha benki ya maendeleo ya taifa!
Kule KIA, uwanja umekodishwa kwa mgeni anayeliilipa serikali dola 1,000 tu kwa mwaka, wakati yeye hulipwa dola 5,000 kwa siku na KLM peke yake, sasa hivi mgeni huyo amefikia mahali anakodisha mashamaba ya eneo hilo kwa wananchi kwa shillingi 20,000 kwa eka! What a joke kwa taifa letu? Na serikali kwa nini imegoma kabisa kuuangali8a mkataba huo wa KIA? Nani yuko nyuma yake?
(7). Iweje wilaya kama Geita, kuwa na wakazi wapatao 62% ambao hawana maji, wala umeme pamoja na utajiri mkubwa uliomo katika wilaya yao?
Matokeo yake ni wilaya tatu tu za Tanzania, ambazo umasikini ni mchache Bukoba Mjini 11%, Arusha Mjini 12%, Mbeya Mjini 12%,
sasa serikali iseme imekuwaje hizi wilaya kuwa na uwezo mkubwa wakati hazina madini au utajiri wowote unaofahamka kitaifa?
Serikali inaondoaje kodi ya mafuta ya ndege na kuacha mafuta ya taa yanayotumiwa na wananchi wanyonge walio wengi? Ni wananchi wangapi wanaopanda ndege?
Serikali inaelekezaje 60% ya hela za maendeleo kwenye Halmashauri za Wilaya ambazo tayari experience inajieleza wazi wazi kuwa hakuna usimamizi mathubuti ya pesa hizo?
Hawa wawekezaji wa madini ndio kabisaa ni mazingaombwe matupu, kwani wawekezaji hawa kazi yao ni kuipa serikali mahesabu ya uongo ili kukwepa kulipa kodi, sasa either viongozi wetu wahusika hawaelewi au wanakula nao makusudi?
Wakati umefika kwa serikali yetu kuingia ubia na wawekezaji hawa kwa kutumia mtaji wa madini yenyewe kama Botswana inavyowafanyia wawekezaji wao, na kuwalazimisha wawekezaji kufidia gharama za wataalamu, na kugawana nao mapato 50%, kama Botswana, badala ya kusubiri 3%, hayo ni maajabu ya dunia!
Mungu Aibariki Bongo!