Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,554
1,381
Nimekuwa nasoma hotuba za bajeti za wizara nzito za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Kilimo na Miundombinu. Zinapatikana kwenye national website ya Tanzania.

Bajeti ya Kilimo ni 123 bn/= (more precisely ni TSh. 123,093,381,600)

Bajeti ya Miundombinu ni 464 bn/= (more precisely ni TSh. 463,881,945,000)

Bajeti ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni 240 bn/= (more precisely ni TSh. 239,650,710,900).

Ukijumlisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya wizara hizi tatu muhimu, zinafika 827 bn/= (more precisely TSh.826, 626,037, 500).

Sasa basi, jumla ya fedha zote zitakazotumika na serikali mwaka huu wa fedha ni TSh. 4.85 trillion. Maana yake ni kwamba wizara tatu muhimu za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Kilimo na Miundombinu, zimetengewa asilimia 17 tu ya matumizi yote ya serikali.

Linganisha hilo jambo na matumizi ya serikali ya Kenya ambako Elimu peke yake imetengewa asilimia 27 ya matumizi yote ya serikali.

Swali ninalotaka mnijibu ni hili: Kama hatutumii hata 20% ya bajeti yetu kwenye Kilimo, Elimu na Miundombinu (combined) hela yetu inatumikaje? Kwa nini jirani zetu waweze kutumia 27% ya bajeti yao kwenye Elimu wakati sisi hatufikii hiyo asilimia hata tukijumuisha Kilimo na Uchukuzi?

Augustine Moshi
 
Moshi
Uchambuzi wako ni wa muhimu; na ni vema tukalijadili suala hili na lile ulilopost kwa chifu Ihunyo. Ni kweli hata mimi naona wengi wa wapenda majukwaa haya wanapenda siasa....is easy going.....payuka tu kinachokuja kichwani...kama ilivyo tu kwenye masuala ya dini....sorry.

Nami nashangaa kama mambo muhimu ya kushughulikia kama kilimo ulio uti wa mgongo, na miundo mbinu na elimu zinapewa hela ndogo namna hii, hela nyingi zinakwenda wapi?

Najua wewe ni mtu wa hesabu, tuletee hizo hesabu za ulinganisho wa aina mbili. Kwanza kipaumbele za bajeti kipo wapi(asilimia kubwa ya bajeti). Pili, are our East African neighbours equally idiots like we are?
 
A Moshi

Heshima yako Mkuu. angetokea Mheshimiwa mmoja pale Dodoma kujumuisha na kuhoji serikali yetu inaelekea wapi kutokana na mtizamo huo kama wako hapo juu,
nina imani mitizamo/mind ya wananchi wangejiuliza sana.

Namkumbuka ushauri wa Mzee Rufiji na Mzee Kyoma kuwa hii seriakli iliyoko madarakani ili iweze kuwajibika ipasavyo, inabidi siku zote tuwaweke/tuwaulize maswali yatakayowaweka kweney "offensive side".

Dr. Slaa, Zitto Kabwe et al hongereni kwa hoja zenu na endeleeni kuwapa vidonge, ipo siku wananchi tutazinduka na kuwawajibisha wahusika ktk uwanja wa demokrasia.

Invincible,
Halafu eti tunaambiwa, Dr AK aliwasaidia kuandaa budget........oooh no, relative to our neighbors, we may all be idiots BUT i think we are more!!
 
The Invincible,

Bado sehemu kubwa ya hotuba za bajeti hazijasomwa. Naona kwenye magazeti ya ippmedia wanasema Wizara ya Elimu ya Juu na Sayansi imeshawakilisha bajeti yake. Sijaiona bado kwenye national website.

Zikishapatikana hotuba za wizara kubwa nyingine (Afya, Ulinzi) tutalinganisha.

Augustine Moshi
 
Augustine Moshi,

Pia utatusaidia sana sisi akina mbumbumbu kama utabreakdown ni wizara gani zilizopewa kipaumbele katika fedha za matumizi katika bajeti ya mwaka huu.
 
(1). Serikali imeongeza bajeti ya maendeleo kwa ujumla, toka 32.2% mpaka 35.8%, hiyo ni Plus!

(2). Serikali inasema mchango wa bajeti ya ndani umeongezeka kutoka 18.4% mpaka 37% kwa mwaka huu, NONESENSE!

Hapa ni a big lie kutoka kwa waliotengeneza bajeti Meghji/Rostam & Kigoda,

look kuna Billioni 219.24 ambazo zilifutwa as madeni ya IMF, kwa hiyo hizo haziwezi kujumuishwa katika mchango wa ndani wa nchi katika bajeti, kwa hiyo zinastahili kuwemo kwenye fedha za wafadhili au za nje!

(3). Kilimo uti wa mgongo wa taifa letu na as a sera ya CCM inavyosema, umekatwa bajeti yake kwa 28%, yaani toka Billioni 65 mpaka Billioni 45.8,

sasa pamoja na maendeleo kwa ujumla kuongezeka toka 33.2% mpaka 35.8, ya kilimo ni only 2.6%! wakati maendeleo ya mifugo ni 0.57% tu

according to Meghji, sekta ya kilimo imepewa umuhimu kwa kupewa 3.2% tu, yaani kilimo na mifugo ni 3% tu bajeti yote, badala ya 10% kama vile SADC inavyozitaka nchi wanachama wake kufanya!

Katika urais wake wote Mkapa never went over 5%, lakini sasa ni 3% katika Kai mpya! na Ari mpya! NONESENSE!

(4). Awamu ya nne imekuja na cabinet kubwa ambayo haijawahi kutokea, as if tumetoka kwenye civil war kwa hiyo tunahitaji kujumuisha vikundi vyote vilivyoshiriki kwenye hiyo vita, kwa kuwapa vyeo,

look at this Wizara ya fedha peke yake matumizi yameongezeka kutoka Sh. TRILIONI 1.7 mpaka TRILIONI 2.0, for what? Hakuna maelezo maana yake hizo zitakuwa ni hela za kusaidia mukitano ya CCM kule Chimwanga, kuwalipia wajumbe 2000 kukutana kwa siku tano kumchagua mwenyekiti ambaye wanajua tayari kuwa ni lazima awe rais wao, kwa nini kamati kuu isiamue tu na kumpa bila kutu-cost wananchi ambao sio wote wana-CCM?

(5). Waziri Mkuu, toka 1.7 Billioni SH. mpaka 4.0 Billioni, ongezeko la 130%, for what? Look here shillingi millioni 600 kwa ajili ya kununulia magari tu! toka shillingi millioni 170 za mwaka jana,

ina maana Sumaye aliondoka na magari yote? Au amelipia shule anayosoma sasa kule Boston? NO, zitanunua magari mapya ya Mwinyi, Mkapa, Warioba, Salmini, Seif, Jumbe, Salim, JM, Sumaye, Bilali, Msuya, Kawawa, ni lazima wapate magari mawili mapya kila mwaka!

(6). 46% ya bajeti yetu tutapata toka kwa wafadhili, lakini tutatumia shillingi millioni 300 kwa ajili ya kununulia furniutre za viongozi!

Mungu Ibariki bongo!
 
Asante Field Marshall ES, kwa mchango wako mzito katika kuangalia hii bajeti ya JK.

Ni hali ya kusikitisha kuona kwamba nchi yetu inatumia asilimia 3.2 tu ya bajeti yake kwenye KILIMO, na asilimia 4.9 tu kwenye ELIMU. Wakati huo huo, imetenga asilimia 41.2 ya bajeti itumike kwenye Wizara ya Fedha, ambavyo kama ulivyotoboa, ni fedha ambazo zitaliwa zaidi na viongozi wa CCM. Huku ni kuwaibia wananchi. Kwa nini nusu ya fedha za nchi zitumike Wizara ya Fedha?

We need to put our money where our mouth is. Hatuwezi kuendelea kuwadanganya wananchi kila waka kwamba ELIMU ndiyo kitu tunakazania wakati tukirudi serikalini tunainyima fedha. Ni ulaghai kukubaliana na wenzetu wa SADC kwamba tutatumia 10% ya bajeti kwenye Kilimo kisha tukatenga 3.2% peke yake.

Kama nilivyosema, Kenya wametenga 27% ya bajeti yao kwa ajili ya Elimu. Sisi tunaojiunga nao kwenye soko huria, tutakuwa vibarua wao siku zijazo. Tusishangae hata sasa kuona waajiri wawekezaji wanapenda zaidi kuchukua wafanyakazi toka Kenya. Kiwango cha Elimu Kenya ni mara 4 zaidi yetu. Uganda ni mara 3 zaidi yetu. Na kwa vile sisi tunazidi kuinyima Elimu fedha, pengo hilo litazidi kukua siku zinavyokwenda.

Tunatawaliwa na viongozi wanaolaghai wananchi kwa kuwadanganya kwamba wanatoa kipaumbele kwenye Kilimo na Elimu, kumbe sio kweli. Kutumia sehemu kubwa ya fedha za wananchi kwa ajili ya kujinunulia magari mapya kila mwaka na kujinufaisha kichama, ni WIZI. Kwa maana nyingine, viongozi wetu wamejenga tabia ya kuwaibia walalahoi. Na huo wizi wao wanaupitisha kwenye bajeti. Watu wengi hawaelewi kwani wananyimwa Elimu. Kulitengea taifa 4.9% tu ya bajet kwa ajili ya Elimu, ni kulinyima Elimu kuliko wazi kabisa.

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,

Heshima yako mkuu, hii serikali ya awamu ya nne inaendelea kuvinjari over wananchi wasioelewa wala kuuliza what is going on!,

(1). Hii serikali ina mipango kama MKUKUTA, TMTP 2020, MKURUBITA, MKUMBITA, yote yenye nia ya kuikwamua taifa na kulisogeza mbele katika maendeleo,

lakini ukweli ni kwamba hizo plan zote hazijapitishwa kisheria as they should, halafu mpaka leo serikali kuanzia za awamu ta tatu mpaka leo ya nne, hazijui gharama za kuendesha hiyo miradi, kwa hiyo ni njia tu nyingine ya kuwapa viongozi mlo!

(2). Wakati umefika kwa serikali kuutumia mfuko wa NSSF katika kusukuma maendeleo ya nchi, kama nchi nyingi za Asia na West zinavyofanya,

kwa mfano kitendo cha NSSF kununua Quality Plaza kwa zaidi ya shillingi Billioni 45, ni upumbavu wa hali ya juu mno kwani wataalamu mbali mbali walishatoa tathmini kuwa taifa letu linahitaji benki yenye mtaji wa Billioni 50 tu! ili kuendeleza maendeleo ya wananchi, kwani benki yetu ya maendeleo TIB leo ina mtaji wa shillingi Billioni 24.9, sasa ingepewa hizo Billioni 45 si ingepewa hiyo benki kwa ajili ya maendeleo ya taifa badala ya hiyo Plaza mabyo ni utata mtupu?

(3). Ukiangalia kwa makini kufutwa kwa kodi ya gesi, nia na madhumuni ni kuwapatia nafasi wakubwa wanaotumia majiko ya gesi kutolipa kodi kubwa,

masikini wote hutumia majiko ya mafuta ya taa ambayo kodi yake haikuondolewa, hivyo basi masikini ataendelea kulipa shillingi 52 za kodi ya mafuta ya taa kila wanaponunua lita moja, as opposed kwa wakubwa wanaotumia gesi!

(4). Ubinafsishaji, kwa mwaka 2005 peke yake mshirika 11 yaliuzwa, yakiwa na mali 126, hivyo katika miaka 13 iliyopita toka zoezi lianze mashirika 322 yenye mali 647 yameuzwa tayari,

lakini to this day serikali zote tatu hazijawahi kusema hadharani tathmini ya mafanikio ya huu mpango wa ubinfsishaji, je ajira imepungua au imeongezeka? Je wawekezaji katika mashirika yaliyonunuliwa wametimiza masharti ya serikali ya sheria ya bunge ya uwekezaji?

Vipi ATC imefikia wapi? Kwa nini serikali imeingia gharama za ajabu kulikwamua shirika hilo na kuyaacha mengine? Kwa nini tume ya kamati ya mashirika umefukuzwa kazi yote bila taarifa maalumu ya sababu yake?

(5). Mpaka leo serikali haijasema lolote kuhusu ripoti ya Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Serikali, aliyesema kuwa Rushwa inachukua 30%, Ufisadi 20%, Mgongano wa masilahi 25%, kutojali sheria 25%, ya fedha za serikali, na CCM ikiwa inachukua sehemu kubwa ya pesa hizo kwa ajili ya mikutano yao?

(6). Kwa nini serikali ilinunua ndege ya rais kwa gharama ya shillingi Billioni 42, ambayo leo haitumiki tena? Hizo pesa zilikuwa zinatosha kabisa kuanzisha benki ya maendeleo ya taifa!

Kule KIA, uwanja umekodishwa kwa mgeni anayeliilipa serikali dola 1,000 tu kwa mwaka, wakati yeye hulipwa dola 5,000 kwa siku na KLM peke yake, sasa hivi mgeni huyo amefikia mahali anakodisha mashamaba ya eneo hilo kwa wananchi kwa shillingi 20,000 kwa eka! What a joke kwa taifa letu? Na serikali kwa nini imegoma kabisa kuuangali8a mkataba huo wa KIA? Nani yuko nyuma yake?

(7). Iweje wilaya kama Geita, kuwa na wakazi wapatao 62% ambao hawana maji, wala umeme pamoja na utajiri mkubwa uliomo katika wilaya yao?

Matokeo yake ni wilaya tatu tu za Tanzania, ambazo umasikini ni mchache Bukoba Mjini 11%, Arusha Mjini 12%, Mbeya Mjini 12%,

sasa serikali iseme imekuwaje hizi wilaya kuwa na uwezo mkubwa wakati hazina madini au utajiri wowote unaofahamka kitaifa?

Serikali inaondoaje kodi ya mafuta ya ndege na kuacha mafuta ya taa yanayotumiwa na wananchi wanyonge walio wengi? Ni wananchi wangapi wanaopanda ndege?

Serikali inaelekezaje 60% ya hela za maendeleo kwenye Halmashauri za Wilaya ambazo tayari experience inajieleza wazi wazi kuwa hakuna usimamizi mathubuti ya pesa hizo?

Hawa wawekezaji wa madini ndio kabisaa ni mazingaombwe matupu, kwani wawekezaji hawa kazi yao ni kuipa serikali mahesabu ya uongo ili kukwepa kulipa kodi, sasa either viongozi wetu wahusika hawaelewi au wanakula nao makusudi?

Wakati umefika kwa serikali yetu kuingia ubia na wawekezaji hawa kwa kutumia mtaji wa madini yenyewe kama Botswana inavyowafanyia wawekezaji wao, na kuwalazimisha wawekezaji kufidia gharama za wataalamu, na kugawana nao mapato 50%, kama Botswana, badala ya kusubiri 3%, hayo ni maajabu ya dunia!

Mungu Aibariki Bongo!
 
Mzee Es,

Kufutwa kwa kodi ya gesi kutasaidia wananchi waanze kutumia gesi badala ya mkaa na kuni. Itabidi kufuta kodi ya majiko ya gesi vile vile. Kwa vile tuna gesi nyingi sana, basi ni vema kuhimiza utumiaji wa energy source hiyo, badala ya mafuta ya taa, mkaa au kuni.

Mikataba mingi ambayo serikali imewekeana na wawekezaji, haikuzingatia maslahi ya taifa. Kuondoa tatizo hili, itabidi ipitishwe sheria kwamba mikataba yote ya serikali lazima ipate kibali cha Bunge kabla ya kutumika.

Nataka sasa nirudi kwenye swala la bajeti ya Elimu. Nasikia Waziri Mama Sitta amekataza ada za shule binafsi kuzidi sh 380,000 bila ridhaa yake. Naona amefanya kosa kubwa sana. Hatua hiyo, kama ikitekelezwa, itarudisha nyuma sekta ya Elimu ya shule binafsi.

It is my ardent hope that well informed Tanzanians like Mama Rwakatare will prevail so that Mama Sitta does not succed in plunging our educational sector into mediocrity, again. Kwa kiasi, Mama Sitta anajipa madaraka yasiyo yake. Hizo shule asiacha alivyozikuta. Sio za serikali, aache kudhani kwamba anatawala kila kitu. Ni uchu wa madaraka ndio umemfanye atake yeye kutoa kibali cha ada iwe kiasi gani.

Sh 380, 000 kwa miezi 8, ni kama sh. 47,000 kwa mwezi. Huwezi kumpatia mtoto elimu bora shule ya boarding kwa dola 45 kwa mwezi. Itabidi watu waelewa waanze tena kupeleka watoto wao kusoma shule za msingi na sekondari Kenya. Kenya wao wanakazania shule binafsi kiasi kwamba kwenye bajeti yao ya mwaka huu, wameondoa kodi ya vifaa vya ujenzi kwa mtu yoyote atakayejenga jengo la shule au la hosteli ya shule.

Tangu ateuliwe kuwa waziri, Mama Sitta amejaribu kutwaa madaraka ya kutawala shule binafsi. Sio zake, sio za serikali, aaache kuziingilia. Mpango wake ni wa kipuuzi na utatuharibia elimu yetu.

Nadhani waziri wa Elimu ametaka tu kutafuta umaarufu kwa kutaka konyesha kwamba yeye na serikali wanajali wanyonge. Hilo sio kweli. Kama wangewajali wanyonge basi wangefanya ifuatavyo: Mwaka huu, tuna wanafunzi wa sekondari 675,000 (angalia hotuba ya bajeti ya Mama Sitta, kwenye National Website). Bajeti yote ya serikali ni shilingi trillion 4.85. Kama serikali ingetumia 10% ya bajeti kwa ajili ya kusomesha watoto wetu wa sekondari basi kila mmoja angelipiwa zaidi ya shilingi nusu milioni (more precisely sh. 718,518) kwa mwaka. Hizo zingetosha, na huko ndio kungekuwa ni kuwajali wananchi.

Vile vile, 2% (TWO PERCENT) ya fedha ambazo serikali imetengea Wizara ya Fedha (zaidi kwa ajili ya matumizi ya wakubwa) ni sh. 40 bn. Hizo ni fedha zinatosha kuipa kila moja kati ya shule 196,391 za serikali, za sekondari, zaidi ya shilingi milioni 200 (more precisely sh. 203,675,321).

Tuache kulaghai wananchi. Tatizo kubwa lililoko sio la kukosekana fedha, ni la viongozi kutumia wao karibu nusu ya fedha zote za wananchi

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,

Ni lazima kwanza tufanye operation ya kujenga nyumba zinazofaa kupitisha mitambo ya gesi, kwani walizonazo wananchi sasa hivi ni vigumu kupitisha hizo system,

nyumba nyingi za wananchi wetu hazifai, kwa hiyo mkaa, kuni, na majiko ya mafuta ya taa yataendelea kutumika na wengi, halafu kumbuka pia sisi inaonekana ni jadi yetu kutumia mikaa na kuni, wewe nenda hata huko Obey, utakuta nyumba ya waziri pamoja na yote ya kizungu kuwepo, bado kuna majiko ya mkaa na kuni kwa nyuma, duka la soda mbele, na vitumbua, halafu hawakosi mbuzi na ng'ombe, pamoja na kuku,

bado wananchi wetu pamoja na viongozi wanahitaji kuelimishwa sana ili tuweze kuishi kistaarabu na kihadhi pia, kwa hiypo serikali kwa sasa inahitaji kuondoa kodi ya mafuta ya taa pia kuwawezesha walala hoi nao wanufaike pia, badala ya kutoa kodi ya mafuta ya ndege na gesi,

huo ni uhuni wa serikali, kwani ni wananchi wangapi wanaopanda ndege? Na ni wananchi wangapi wanaotumia gesi? Huo ni uhuni wa mchana wa serikali ya awamu ya nne!
 
Mzee ES,

Ni shida kumwambia mtu aliyezoea kuishi na mbuzi na kuku aache kufanya hivyo. Atajisikia hajakamilika. Hiyo biashara ya kioski inayoonekana kwenye nyumba za wakubwa ni kinga. Ukiuliza imekuwaje awe tajiri hivyo, atakuwa na jibu kwamba anafanya biashara.

Ni muhimu kuhimiza matumizi ya gesi, hata kama ni asilimia kidogo tu ya Watanzania wana nyumba zinazoweza kuwekwa majiko ya gesi. The number of users will grow with time. Ni sawa kabisa kufuta kodi ya gesi kwa sasa. Taifa linahimiza utumiaji wa nguvu za jua na gesi badala ya mafuta, mkaa na kuni.

Ili kupata watalii wengi, inabidi kuvutia mashirika ya ndege yatue kwetu. Ukiweka kodi kubwa kwenye mafuta ya ndege, unawakimbiza wenye ndege na utapunguza idadi ya watalii. Kumbuka kuwa jumbo jet linachukuwa mafuta lita 28,000 kwa mpigo. Ni sawa kupunguza kodi ya mafuta ya ndege.

Utalii ni sekta inayoweza kutuletea fedha nyingi za kigeni kuliko hata kilimo. Ni lazima kuweka vivutio vya mashirika ya ndege kuja Dar badala ya kuishia Nairobi tu. Itabidi vile vile tutoe ruhusu kwa wageni kuomba visa baada ya kufika kwetu. Hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa Singapore.

Augustine Moshi
 
Mzee Moshi,

Kuwasaidia watalii, kabla ya kujisaidia sisi wenyewe ni dhana nyepesi, halafu nini faida ya kukusanya hela nyingi za watalii wakati hela zenyewe hatuzioni?

Mahospitali yako hoi, shule ndio hivyo hamna madawati, umeme wa kugawana leo 2006!, halafu hawa jamaa ndio kwanza wanavaa masuti makubwa kwenda nje kujitambulisha kwa wazungu,

Tutengeneze nyumbani kwanza, baadaye ndio tuwaangalie watalii, wananchi kwa sasa wanahitaji a break ya kodi ya mafuta ya taa, kwani ni asilimia kubwa ya wananchi inayoyatumia mafuta hayo, unless kama mzee umeondoka siku nyingi, bado mafuta ya taa ndio kila kitu kwa mwananchi wa kawaida, tena hasa katika huu umeme tulionao sasa,

Maneno yako mengine ni mazito na ni kweli!
 
Mazingaombwe, Mazingaombwe, Mazingaombwe!!! Hakuna kitu kibaya kama Taifa la wajinga, taifa la watu wasiokumbuka!

Watanzania tunafanywa (samahani mheshimiwa spika) kuwa sisi ni wajinga na vichwa vyetu havina uwezo wa kufikiri. Kama Taifa letu haliwekezi kwenye hizi sekta nne: miundo mbinu, elimu, afya na kilimo, hatuwezi kupiga hatua kubwa ya maendeleo. Tutaendelea kudhamiria, kunuia tu lakini hatuendi popote.

Tanzania haiwezi kuendelea bila kilimo.. period!! kudhamiria kuwa na uchumi wa kisasa kwa kuwa na viwanda vya uzalishaji wa bidhaa kubwa ni kujidanganya.. kudhania uchumi wetu utajengwa kwa madini na utalii, ni kujidanganya! kudhania kuwa maisha ya wananchi wetu wengi yanaweza kuboreshwa kwa kitu kingine zaidi ya kilimo ni uongo mkubwa!

Kilimo, kilimo, kilimo ndio njia pekee inayoweza kufungua mlango wa mafanikio kwa wananchi wetu. Hata hivyo kwa mtindo huu wa bajeti, itabakia kuwa ndoto isiyotimia!!!
 
Nasikitika kuona logic ya Mzee ES imekuwa tena ya wasiwasi. Tunataka kuvutia watalii wengi kwa faida yetu, sio kwa faida ya hao watalii. Mwaka jana, tulipata watalii laki sita, na waliingiza fedha za kigeni $700 million. Mazao ya kilimo yaliingiza chini ya $500 million.

Mzee ES, iweje ukemee watu kuishi na mbuzi na kuku na huku unataka tuendelee kukazania majiko ya mafuta ya taa? Inabidi kukumbatia mabadiliko ya kuleta maendeleo moja kwa moja, sio nusu nusu. You cannot be a little bit pregnant.

Mzee wa kijiji anasema haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutegemea utalii na madini. Mbona Misri imeleta maendeleo (relatively) kwa kutegemea utalii? Nguvu ya uchumi wa Kenya ni utalii. Mwaka huu, Kenya wanatarajia watalii 1.8 mil. That should bring in about $2.5 billion. Yaani Kenya itaweza kuingiza zaidi ya nusu ya fedha za bajeti yote ya tanzania kwa njia ya utalii peke yake.

Inabidi tulime, kwani kama alivyosema Mwalimu, tusipolima tutakufa. Lakini, ili kupata fedha nyingi za kigeni, inabidi kukazania zaidi utalii. Utalii ndiyo sekta yenye uwezo mkubwa kuliko zote Tanzania, wa kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Nashauri msome vile vile hii paper kuhusu bajeti ya kilimo (2006) ambayo imeandikwa na mtaalamu wa SUA. Iko hapa:

http://www.tzonline.org/pdf/implicationofthe20062007budgetonthedevelopment.pdf

Augustine Moshi
 
Wananchi wa Tanzania asilimia 80%, wanaishi vijijini ambako hakuna umeme wala gesi, na uwezekano wa kutumia gesi haupo for the next 50 years!

Mafuta ya taa ndiyo nyenzo muhimu kwa maisha ya hawa wananchi, mpaka tutakapofikia kuwa na uwezo wa kuwapa gesi, mimi na wewe hatutakuwepo tena duniani,

kwa hiyo wanahitaji break ya kodi ya mafuta hayo sasa!, ili waache kulipa shillingi 52 zaidi ya bei ya mafuta hayo, kuondoa kodi ya mafuta ya ndege kwa wakati na kuacha ya mafuta ya taa ni a big joke kwa wananchi ambao wengi wananishi vijijini, na hata wale wa mjini ambao wengi hawana uwezo wa kuwa na gesi au kupanda ndege,

Huhitaji kuwa na big logic au smart logic, au kuwa intellectual kujua hilo, kuwa wananchi wanaokwenda kazini kwa miguuu toka Kimara mpaka mjini, au ndugu yangu simama pale Jangwani asubuhi uone wananvyoteremka kwa miguuu maana hawana nauli ya basi,

sasa hawa wataweza gharama za gesi?
 
Mzee ES,

Ni sawa kuondoa kodi ya mafuta taa. Ni pesa kidogo sana. Haifiki hata 0.1% ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Fedha.

Ndege zinazotua Tanzania ni chache sana. Nimetembea sehemu nyingi, lakini sijaona mji mkuu wenye ndege chache kiwanjani kuliko Dar. Sasa kodi kubwa ya mafuta ya ndege ya nini? Nasisitiza tena kwamba kodi ya mafuta ya ndege imeondolewa kwa faida ya wananchi. Kama fedha za kigeni zinazoletwa na watalii zikipungua, basi shilingi inashuka bei, na matokeo yake bei za bidhaa kama mafuta taa zinapanda.

Utalii inabidi ukuzwe ili uwe muhimili wa uchumi wetu. I would say that our tourism potential is about $3 bn per year. Hatua za kukuza utalii ni pamoja na kuweka vivutio vya mashirika ya ndege kuleta ndege zao kwetu. Ukiwa na kodi kubwa ya mafuta hawaji.

Gesi inauzwa kwenye chupa, na chupa ndogo sio bei ya kutisha. Bei ya jiko dogo la gesi sio ya kutisha vile vile. Majiko ya gesi ni kitu kinachoweza kutumiwa na sehemu kubwa ya Watanzania, sasa na sio miaka 50 baadaye.

Augustine Moshi
 
Unajua kwa maoni yangu ni kwamba Watanzania, as serikali wakati umefika wa kuamua mambo muhimu ya uchumi, maisha, na siasa zetu bila ya kujali watu wa nje,

Kama ni suala la kuweka masharti nafuu ya biashara kuwakaribisha wawekezaji wageni, tayari tumeshaona faida yake hapa Royal Palm, tunaambiwa toka ianzishwe as Sheraton, mpaka leo inamilikiwa na wale wale yaani the original owners, lakini kwa ajili ya kukwepa kodi imebadilishwa majina wee ili kutudanganya kuwa imekuwa ikinunuliwa na watu wapya, na hilo linaendelea katika kila sector ya biashara hapa nchini,

Hatuwezi kuendelea na hizo siasa za kujali tuuu watu wa nje, ndege haziji kwa sababu bongo hatuna kitu cha kuzifanya zije, watalii watakuja tu hata kama bei iwe kubwa kiasi gani, kwa sababu ikiwa ni pamoja na zingine nyingi kuwa wanakuja kuona vitu ambavyo ni natural sio man made, sasa kwenye hilo ni lazima tuwalipishe ipasavyo kulingana na matakwa ya uchumi wetu lakini hatuwezi kupunguza bei ya biashara zetu kwa sababu ya kuvutia watalii,

kufuta kwa kodi ya mafuta ya ndege peke yake kunapunguza at least 10%, ya pato la serikali kwa mwaka, sasa mzee Moshi katika bajeti ambayo inategemea 46%, toka kwa wafadhili unapata wapi pesa za kufidia hiyo 10%?

Mimi sio mtu wa mahesabu, wala namba huwa sizipendi maana hawa mawaziri wanaohusika na hizo namba, tunawasikia mara kwa mara wakiwa nje ya bunge wakijicheka kuwa wanayosema bungeni hayawezekani, kwa hiyo hiyo imenifanya kwa siku nyingi nisiziheshimu hesabu za mawaziri wa bongo, tena Marehemu Malima alikuwa mtu wa kwanza kumsikia akizicheka hesabu zake mwenyewe, lakini for the benefit of the forum na debate, kuondoa 10% ya bajeti yetu bila ya kusema utakaptoa hela za kufidia ninauona ni usanii wa serikali mpya,

Halafu regardles ya thamani ya mafuta ya taa, lakini kumbuka kuwa shillingi 52, kwa mwananchi wa kawaida ni hela nyingi sana, halafu tuko kwenye mafuta ya taa kwa muda mrefu sana ujao, mzee tembelea vijijini ujionee yalivyo muhimu kwa wananchi, na hata raios mwenyewe anapotembelea sehemu nyingi za nchi ni mafuta ya taa ndiyo yanayosaidia sana kwenye guest house au nyumbani kwa mkuu wa wilaya, miji kama Mahenge/Ulanga mzee Moshi huko bila ya mafuta ya taa ni kiama, na huwezi kusema kuwa serikali ina mpango wa kupeleka umeme au gesi hivi karibuni, maana hata kwenye mto Kilombero ili kuvuka kwenda Mahenge ile pantoni au ferry, sijui ni ya mwaka gani?, yaani hata mimi nilikuwa sijazaliwa yaani ile ferry inaenda kwa sababu ya wafanyakazi wake kuvuta kamba ya wire au sometimea kuikanyaga kwa miguu, ndipo fery iende bro!

Jamani mnapokuja bongo hebu tembeleeni mikoani na vijijini ili mujionee wenyewe kwa macho, ninakuapia mzee ukienda huko Mahenge ndio utajua bongo tuko nyuma kiasi gani, maana hata ule mji mkuu wa wilaya ni hawa wakatoliki mission ndio wametusaidia mno ama sivyo kungekuwa hakuna mji kabisaaaaaa! Na viongozi wetu hawaoni aibu wanapokwenda huko na kukaa missionary kwa mapadri, ambako ndiko kuna umeme!

Tufanye maamuzi ya kiuchumi ya kukidhi mahitaji yetu kwani hayo ya kuwasaidia wageni bado hayajatuletea mabadiliko kimaisha au kiuchumi, kama ni thamani ya hela yetu, hilo limeshaonekana kuwa hatuna uwezo nalo, ni wazee wa West ndio wenye uamuzi,

Mwalimu peke yake ndiye aliyeliweza hilo, ingawaje swali sasa ni kwamba aliliweza kweli au ndiyo tunalipia sasa?
 
Mzee ES,

Katika bajeti hii ya 2006/2007, kodi ya mafuta ya taa imepunguzwa toka sh. 122 kwa lita hadi sh. 52 kwa lita. Mtu akisoma unavyoiandika atadhani imepanda

Kwenye hotuba ya Waziri wa Fedha (angalia kwenye national website) ukurasa 42, inasema wazi kwamba ushuru wa mafuta ya taa umepunguzwa. Umeshuka kwa 57% sasa, na labda utamalizika kabisa mwakani

Augustine Moshi
 
Hapana, ninasema hata hiyo ya shillingi 52 bado ni nyingi kwa mwananchi wa kawaida, nayo pia ipunguzwe au iondolewe kabisaa,

hiyo ripoti nimeisoma kabla hata haijatolewa humu!
 
Ndugu zangu,

Naona lazima tujaribu kujiuliza kwa dhati namna tunavyotumia fedha zetu. Kufikia hapa, tumeona kwamba Zambia wanatumia 24% ya bajeti yao kwenye Elimu, Kenya wanatumia 27%. Sisi mwaka huu tunatumia 4.9% tu ya bajeti kwenye Wizara ya Elimu na Ufundi. Sijajua bado Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu imepangiwa kiasi gani. Naamini ukijumlisha zote, bado tutakuwa tunatumia chini ya 10% ya bajeti yetu kwenye Elimu.

Malawi mwaka huu wanatumia 15% ya bajet yao kwenye Elimu. Nimeposti hapa chini makala inayotoa hizo takwimu za Malawi.

Sijui hadi sasa ni asilimia gani ya bajeti ya Tanzania ya 2006 itatumika kwenye Afya. Naona Malawi wametambua umuhimu wa Afya na Elimu, na kwa pamoja wamezitengea 34.6% ya bajeti yao.

Kwa nini Tanzania tumeficha karibu nusu ya fedha zote za Bajeti kwenye Wizara ya Fedha? Zitatumikaje? Kwa nini hakuna uwazi?

Augustine Moshi
===============

Agriculture, social sector get lion's share of Malawi budget.

afrol News / The Chronicle, 19 June -

The Ministries of Agriculture and Food Security, Health and Education have respectively been given a lion's share in the tentative 2006/07 budget presented by the Minister of Finance Goodall Gondwe last Friday in the House.
The budget, pegged at kwacha 134.704 billion but with expenditures amounting to K138. 705b leaving a deficit of K4billion, grants K16.817b to Agriculture and Food Security representing 12.2% of total budget.

"This is an action-packed budget that would ensure that people do not go hungry even in the absence of the rain," said Gondwe presenting his budget.

In the social sector, Education gets an overall of K20.5b including Universities and this, according to the Finance Minister is the highest lot the sector has got in the Sadc Region.

From the Education budget Universities get a cut of K3b from which Mzuzu University gets K650m, with K40m specially allocated for development at the college.

Gondwe also announced that the construction of the Lilongwe University of Science and Technology (LUSTEC) commences this year with an allocation of K50m.

Ministry of Healthy gets an overall chunk of K22.634b, representing16% of total expenditure.

"Social sectors, particularly consisting of Education and Health have an allocation accounting for approximately 34.6% of total expenditure in the 2006/07 budget," Gondwe said adding that this is in parallel with the sectors, which President Mutharika described as priorities for immediate economic growth purposes.

The 2006/07 has also taken on board the legislature's long over due outcry of constituency development fund pegging it at K2m per constituency which the Finance Minister said would be monitored by the MPs.

"Each MP would decide on what kind of development to embark in their constituencies and it would be the MP's responsibility to supervise and account for the expenditures," said Gondwe amid murmuring from the House.

The opposition has so far welcomed the budget statement but said more need to be done for it to benefit the Malawians.

In its pre-budget submission the Civil Society Coalition for Quality Basic Education (CSCQBE) proposed an allocation of at least 18% of the total budget to education in pursuit of the 26% international recommendation required to meet the education for all (EFA) and education millennium development goals (MDGs)

CSCQBE Research Monitoring and Evaluation Officer, Clara Chindime, who made the pre-budget presentation in Lilongwe prior to the budget sitting, declined to comment immediately after the Finance Minister's budget presentation saying it was too early to do so.

"We can not comment now, we need to go through the whole budget statement and all related

documents before we make a comment. Besides, Limbani Sapato would be the right person to comment on behalf of (CSCQBE).



By Kondwani Magombo


© afrol News / The Chronicle
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom