Hii ndiyo NMB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo NMB

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by oba, Jun 19, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuweka pesa akaunti isiyo yako 1000.00, kuangalia salio 200, kuchukua pesa ATM 400, kuchukua pesa ndani 700, service charge per month 500. Hii ni nini kama siyo wizi? kuna faida gani ya kuweka pesa benki? naona nirejee mbinu ile ya babu ya kutunza vichele vyangu kwenye kibuyu, pesa yenyewe naipata kwa shida, akaunti yenyewe ina pesa isiyofika hata 200000, niweke NMB so what?naibiwa tu!
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  huu wizi,nadhani ndio chanzo cha mapato walichokibuni hawa makabulu
   
 3. S

  Sharp lady Senior Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hyo ndo NMB zaidi ya usivyoijua na ukitumia NMB MOBILE ndo utashangaa zaidi wanakuibia live.
   
 4. d

  dropingcoco Senior Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio mkome, kwani si uhame bank, ni hiyo moja tu ipo
   
 5. l

  lucy mboya Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh na wale ambao wanalipwa kupitia nmb c ndo wataibiwa hadi mwisho!
   
 6. N

  NCHABIRONDA JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Acheni kuhangaika wekeni hela tu kwenye M- PESA.
   
 7. P

  Pat Gucci Senior Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! Maskini poleni, naona mnalia lia tu...
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,114
  Likes Received: 6,596
  Trophy Points: 280
  Ndo maana yule Mh. aliiita benki ya makabwela kumbe mambo yake makubwa ati,
   
 9. T

  The Priest JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hii siyo bank waliibia sana kwenye NMB mobile sina hamu nao.
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  majizi!lakini watumishi wa umma hawana choice cuz taasisi za serikali zina account na nmb,..ukijifanya mshahara upitie benki nyingine utapata mshahara baada ya wiki mbili tokea wa nmb wapate(mshahara wenyewe kichekesho)
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi wajameni, Tanzania ni Benki gani yenye afadhali?
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sio NMB tu. Kacheki makato ya mnayosema ni benk yenu, CRDB!
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Benki ya posta aka saccos
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nao hawa pia wezi..
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,119
  Likes Received: 7,368
  Trophy Points: 280
  Kibubu bank ndo mambo yote, faida zake ni kama,
  haina foleni,
  network haisumbui,
  24 hrs,
  huwez kusahau password,
  haina makato/charges,
  atm card haimezwi,
  teller na customer ni wewe mwenyewe n.k.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa NMB ni kama wewe ni mtu wa kusafiri hasa vijijini ndiyo utaona unafuu wake vinginevyo waizi tena chunga sana kutumia simu wanaiba sana...
   
 17. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mh kumbe ndio walivyo yani ukiweka pesa wanakuchaji? Ukitoa ivyoivyo? Ss inafaida gani kwa walalahoi benki ya ukweli ni azania bank akuna upuzi wa makato
   
 18. A

  Aine JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli NMB wanaboa, hivi kwa nini wasitangaze kwanza kwa muda fulani ndo waanze kukata hayo makato yao ili tuangalie ustaarabu wetu! Maana last week nimeenda kutuma hela wakaniambia nilipe sh. 1000 nami sikuwa najua, yaani niliboreka sana nikauliza ina maana hata ATM nayo ukitoa hela unakatwa? teller akaniambia hapana, kumbe unakatwa? jamani kuweka hela bank ni usumbufu kwa kweli kufungua account kwenyewe taratibu zake yahitaji moyo!!!!!!!! ndio maana babu zenu walikuwa wanazichimbia chini na kwenye vibuyu kuliko style hii yaani ni hasara tupu!
   
Loading...