Hii ndiyo mipango na maneno ya mwisho ya January na Maharage. Jee yataendelea kuwa na mashiko?

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
1. Mwaka jana walituambia kwamba uzalishaji wa umeme nchini umefikia 1,872 MW, wa gesi ukiwa 1,350 MW sawa na asilimia 65% na ule wa maji ukiwa 450 MW sawa na asilimia 35%. Umeme wa maji hasa unazalishwa kutoka kwenye mabwawa ya Kidatu (200MW), Kihansi (180MW) na Mtera (70MW). Tuliambiwa mahitaji ya umeme kwa nchi nzima hayazidi 1,300MW hivyo kuna ziada ya zaidi ya 500MW. Hizi takwimu zina mashiko na kwa kiasi kikubwa ni sahihi.

2. Mwaka jana watu hawa walituambia kwamba ingawa uwezo wa kuzalisha umeme unazidi mahitaji, tatizo liko kwenye uwezo wetu wa kuusambaza huo umeme. Kwamba mfumo wa usambazaji umechakaa na hauna uwezo. Kwamba katika awamu yote ya tano chini ya JPM ulikuwa haufanyiwi service au update yo yote. Hivyo walimuomba raisi makumi ya matrillion ya pesa ya kuufumua mfumo huo wa usambazaji na kuweka mpya wa kisasa. Mpango huo wa kuweka mfumo mpya wa usambazaji umeme ungalichukua si chini ya miaka 5. Katika kipindi hicho mgao wa umeme ungaliendelea kwani mambo haya ni ya kisayansi, siyo ya kisiasa.

Sijui kama maneno haya na mpango huu ni wa kweli na una mashiko. Kama ni kweli mambo haya ni ya kisayansi, basi tutegemee mgawo hadi pale transmission system itakapokuwa overhauled completely. Hili Biteko na timu yake mpya wanapaswa kuli verify scientifically.

3. Cha kushangaza na kuacha vinywa wazi, ni Makamba katika hotuba yake ya tarehe 30 June 2023 katika bunge la bajeti alisema:
- Mahitaji ya umeme yameongezeka mara nane katika mwaka uliomalizika tarehe 30 June 2023. Kwamba sasa hivi mahitaji ni 5,810MW wakati uzalishaji ni 1,872MW tu. Akasema kwamba mpango wa serikali ni kuzalisha angalao 5,872MW ifikapo 2025/26!

Hili tamko lina maana kwamba hata pale lile bwawa la Nyerere litakapoanza kuzalisha huo umeme wa 2,015MW bado tutaendelea kuwa na upungufu wa umeme na kuendelea na mgao. Utatuzi wake Makamba alipendekeza miradi kibao ya makampuni binafsi ya kuzalisha umeme jadidifu wa jua, upepo na joto ardhi kuziba pengo hilo ifikapo 2025/26. Bunge letu la bajeti lilipisha mapendekezo hayo na tayari hadi sasa zaidi ya makampuni saba binafsi yameanza kazi hiyo.

Biteko na wenzake wanapaswa ku verify ukweli na mashiko ya maneno haya. Ni kipi ndani ya mwaka mmoja mahitaji ya umeme yameongezeka mara nane, ili hali idadi ya viwanda haijaongezeka na vilivyokuwepo vingi vimepunguza uzalishaji na vingine vimefungwa.

- Katika hotuba yake hiyo ya bajeti, Makamba alisema pia kwamba ndani ya mwaka mmoja idadi ya njia za kusambazia umeme zinazohitajika ni kilomita 10,660.65 wakati zilizopo ni kilomita 6,110.28 tu. Yaani mahitaji ya njia za usambazaji umeme yameongezeka mara dufu ndani ya mwaka mmoja tu. Kwa lipi kwani hata miradi ya REA imekuwa ikisua sua. Hili nalo linahitaji verification.

4. Kufuatia hotuba hiyo ya bajeti, Maharage akaja na maneno haya:
  • Hata pale bwawa la Nyerere litakapoanza uzalishaji bei ya umeme haitapungua na umeme mwingi utauzwa kwa nchi jirani kwani shirika linahitaji pesa ya kulipa mkopo wa fedha uliotumika kujenga bwawa hilo. Hapa sasa unabaki kujiuliza, hivi mikopo ya serikali inayotumika kujengea miundo mbinu kama hospitali, SGR na barabara, si huwa inalipwa kutokana na kodi za wananchi kupitia TRA?
  • Mwezi August 2023 ulipoanza mgao wa umeme, Maharage alisema ni kwa sababu ya ukame (drought) kwani mvua zimechelewa, hivyo maji kwenye mabwawa ya Mtera, Kihansi na kidatu yamepungua. Kila mtu anajua mwaka huu hakukuwa na ukame, kiangazi kimekuwa kifupi sana na hakuna mifugo yo yote iliyo athirika kwa ukame mwaka huu.
  • Mwishoni hapa baada ya kubanwa maswali, Maharage akasema kwamba hatuna mgao bali tuna upungufu tu wa umeme. Mkurugenzi wa huduma kwa wateja (Bw. Martin Mwambene) akimsaidia Maharage kufafanua jambo hilo alisema kwamba grid ya taifa inategemea maji ya mabwawa ya Kihansi, Kidatu na Mtera. Maji yakipungua kwenye mabwawa hayo grid ya taifa inaweza kuhama. Ili grid ya taifa isihame inabidi uzalishaji wa umeme ufanyike kwa awamu hususani nyakati za usiku au mchana ili kuruhusu uhimilivu wa maji hayo na grid ya taifa kutokuhama. Hiki ndicho kinafanyika sasa ambacho sisi tunakiita mgao na Maharage alikiita ni upungufu wa maji kwenye mabwawa hayo. Hili linahitaji scientific verification na kama ni kweli utatuzi wa kisayansi wa kuepukana na balance ya grid yetu kutegemea mabwawa hayo.
 
Wapigaji hawa,sema makwao wana magenerator na mafuta ni bure so hawaathiriki. Yaani walishaona Samia ni Kilaza so wanaiba kupitia mahesabu tu na pesa anaruhusu zitoke za miradi hewa. Na ile bodi yao ilikuwa na kina Mchechu ndani yake unategemea nini?. Huyu huyu mchechu ambae makampuni yake binafsi ndo yalikuwa yanajenga nyumba kipindi yupo shirika la nyumba la taifa na anajilipa mabilioni.
Tanesco pale kunatakiwa wazalendo haswa.
 
Mboni umeniamsha?
 
Mjadala.mzuri, una mshiko na unamuumbuwa KIPARA na yule comedian MABEANS!
Screenshot_20230924-031413~2.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20230924-031518~2.jpg
    Screenshot_20230924-031518~2.jpg
    17.9 KB · Views: 1
Wapigaji hawa,sema makwao wana magenerator na mafuta ni bure so hawaathiriki. Yaani walishaona Samia ni Kilaza so wanaiba kupitia mahesabu tu na pesa anaruhusu zitoke za miradi hewa. Na ile bodi yao ilikuwa na kina Mchechu ndani yake unategemea nini?. Huyu huyu mchechu ambae makampuni yake binafsi ndo yalikuwa yanajenga nyumba kipindi yupo shirika la nyumba la taifa na anajilipa mabilioni.
Tanesco pale kunatakiwa wazalendo haswa.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 💯
 
1. Mwaka jana walituambia kwamba uzalishaji wa umeme nchini umefikia 1,872 MW, wa gesi ukiwa 1,350 MW sawa na asilimia 65% na ule wa maji ukiwa 450 MW sawa na asilimia 35%. Umeme wa maji hasa unazalishwa kutoka kwenye mabwawa ya Kidatu (200MW), Kihansi (180MW) na Mtera (70MW). Tuliambiwa mahitaji ya umeme kwa nchi nzima hayazidi 1,300MW hivyo kuna ziada ya zaidi ya 500MW. Hizi takwimu zina mashiko na kwa kiasi kikubwa ni sahihi.

2. Mwaka jana watu hawa walituambia kwamba ingawa uwezo wa kuzalisha umeme unazidi mahitaji, tatizo liko kwenye uwezo wetu wa kuusambaza huo umeme. Kwamba mfumo wa usambazaji umechakaa na hauna uwezo. Kwamba katika awamu yote ya tano chini ya JPM ulikuwa haufanyiwi service au update yo yote. Hivyo walimuomba raisi
matrillion ya pesa ya kuufumua mfumo huo wa usambazaji na kuweka mpya wa kisasa. Mpango huo wa kuweka mfumo mpya wa usambazaji umeme ungalichukua si chini ya miaka 5. Katika kipindi hicho mgao wa umeme ungaliendelea kwani mambo haya ni ya kisayansi, siyo ya kisiasa.

Sijui kama maneno haya na mpango huu ni wa kweli na una mashiko. Kama ni kweli mambo haya ni ya kisayansi, basi tutegemee mgawo hadi pale transmission system itakapokuwa overhauled completely. Hili Biteko na timu yake mpya wanapaswa kuli verify scientifically.

3. Cha kushangaza na kuacha vinywa wazi, ni Makamba katika hotuba yake ya tarehe 30 June 2023 katika bunge la bajeti alisema:
- Mahitaji ya umeme yameongezeka mara nane katika mwaka uliomalizika tarehe 30 June 2023. Kwamba sasa hivi mahitaji ni 5,810MW wakati uzalishaji ni 1,872MW tu. Akasema kwamba mpango wa serikali ni kuzalisha angalao 5,872MW ifikapo 2025/26!

Hili tamko lina maana kwamba hata pale lile bwawa la Nyerere litakapoanza kuzalisha huo umeme wa 2,015MW bado tutaendelea kuwa na upungufu wa umeme na kuendelea na mgao. Utatuzi wake Makamba alipendekeza miradi kibao ya makampuni binafsi ya kuzalisha umeme jadidifu wa jua, upepo na joto ardhi kuziba pengo hilo ifikapo 2025/26. Bunge letu la bajeti lilipisha mapendekezo hayo na tayari hadi sasa zaidi ya makampuni saba binafsi yameanza kazi hiyo.

Biteko na wenzake wanapaswa ku verify ukweli na mashiko ya maneno haya. Ni kipi ndani ya mwaka mmoja mahitaji ya umeme yameongezeka mara nane, ili hali idadi ya viwanda haijaongezeka na vilivyokuwepo vingi vimepunguza uzalishaji na vingine vimefungwa.

- Katika hotuba yake hiyo ya bajeti, Makamba alisema pia kwamba ndani ya mwaka mmoja idadi ya njia za kusambazia umeme zinazohitajika ni kilomita 10,660.65 wakati zilizopo ni kilomita 6,110.28 tu. Yaani mahitaji ya njia za usambazaji umeme yameongezeka mara dufu ndani ya mwaka mmoja tu. Kwa lipi kwani hata miradi ya REA imekuwa ikisua sua. Hili nalo linahitaji verification.

4. Kufuatia hotuba hiyo ya bajeti, Maharage akaja na maneno haya:
  • Hata pale bwawa la Nyerere litakapoanza uzalishaji bei ya umeme haitapungua na umeme mwingi utauzwa kwa nchi jirani kwani shirika linahitaji pesa ya kulipa mkopo wa fedha uliotumika kujenga bwawa hilo. Hapa sasa unabaki kujiuliza, hivi mikopo ya serikali inayotumika kujengea miundo mbinu kama hospitali, SGR na barabara, si huwa inalipwa kutokana na kodi za wananchi kupitia TRA?
  • Mwezi August 2023 ulipoanza mgao wa umeme, Maharage alisema ni kwa sababu ya ukame (drought) kwani mvua zimechelewa, hivyo maji kwenye mabwawa ya Mtera, Kihansi na kidatu yamepungua. Kila mtu anajua mwaka huu hakukuwa na ukame, kiangazi kimekuwa kifupi sana na hakuna mifugo yo yote iliyo athirika kwa ukame mwaka huu.
  • Mwishoni hapa baada ya kubanwa maswali, Maharage akasema kwamba hatuna mgao bali tuna upungufu tu wa umeme. Mkurugenzi wa huduma kwa wateja (Bw. Martin Mwambene) akimsaidia Maharage kufafanua jambo hilo alisema kwamba grid ya taifa inategemea maji ya mabwawa ya Kihansi, Kidatu na Mtera. Maji yakipungua kwenye mabwawa hayo grid ya taifa inaweza kuhama. Ili grid ya taifa isihame inabidi uzalishaji wa umeme ufanyike kwa awamu hususani nyakati za usiku au mchana ili kuruhusu uhimilivu wa maji hayo na grid ya taifa kutokuhama. Hiki ndicho kinafanyika sasa ambacho sisi tunakiita mgao na Maharage alikiita ni upungufu wa maji kwenye mabwawa hayo. Hili linahitaji scientific verification na kama ni kweli utatuzi wa kisayansi wa kuepukana na balance ya grid yetu kutegemea mabwawa hayo.
1. Mahitaji ya umeme yameongezeka mara 8 zaidi ya awali.

2. Tunahitaji Tri+ kufanya maboresho ya miundombinu ya njia za umeme

3. Hata bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere likikamilika umeme utaendelea kuwa wa mgao kwakuwa shirika litauza nje ili kulipa deni la ujenzi wa bwawa.

TANESCO NI LIDUDE FLAN IVI LIKUBWA, SIO RAHISI KAMA TUNAVYODHANIA, HASA UKIPEWA KULIONGOZA. KUNA MIZIZI NI UNTOUCHABLE.
 
Tusitegemee chochote kipya kwa Tanesco.

Wanaenda na nguvu na maneno magumu ila wote ni wapigaji tu.
 
Suala la umeme bongo huwa ni kama hadithi za Abunuwasi
 
Back
Top Bottom