Hii Ndiyo Ilikuwa Msaada na VPN Haikuwa Msaada?

Hii Ndiyo Ilikuwa Msaada na VPN Haikuwa Msaada?

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,206
Reaction score
25,399
Kuna mandezi wengi sana mtandaoni, nahisi wengi humu ni vijana zetu wadogo sana.

Hawa ni wale ambao akipata kitu kipya na kigeni lazima awaonyeshe wenzake.

Karibu kila mtu alikuwa akipost aina ya VPN anayotumia, hapo nikaanza kujiandaa ikiwa wajomba wa switch wakizima itakuwaje, maana watazuia engo zote.

Sasa bana, siku moja kabla ya uchaguzi nilisearch web gani naweza kutumia ikiwa mtandao umefungwa nikapata moja hivi ambayo kwa uzembe usiku nikasahau kuidownload.

Na mimi nikapigwa lokoo ndiyo hadi leo.

Nilichojifunza ni kuwa watanzania pamoja na uoga tulio nao hatuwezi kukaa kimya kwa jambo ambalo linaweza kuwa faida kwa wakati ujao.
 
TCRA ilielekeza makampuni yote yenye leseni Tanzania kufanya filter ya maneno
Kuzima DATA kabisa
Mwanzo Cellular zilizima zikabakia Satellite na Fiber, baadae wakakata pote.
Waliobaki hewani ni wale ambao walikuwa wakitumia starlink au satellite internet ambazo hazijasajiliwa Tanzania
 
Wale wa Mipakani katika mikoa ya Tanga, Songwe, Ruvuma, Mara, Kagera, Arusha, Kilimanjaro walitumia nafasi zao kunyaka internet kwa kutumia lain za nchi jirani, walichoshindwa tu kupata video na picha kwa wakati kutokea Dar ila walijitahidi kuuhabarisha Ulimwengu kila walipopokea tu kutokea Dar
 
TCRA ilielekeza makampuni yote yenye leseni Tanzania kufanya filter ya maneno
Kuzima DATA kabisa
Mwanzo Cellular zilizima zikabakia Satellite na Fiber, baadae wakakata pote.
Waliobaki hewani ni wale ambao walikuwa wakitumia starlink au satellite internet ambazo hazijasajiliwa Tanzania
Mmmh kwahiyo mkuu, starlink iko tz?
 
Back
Top Bottom