Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,671
- 11,339
Mtu aliyezaliwa 1965 akisema fursa ya vyuo ilikuwa haipo ni kwa sababu alikuwa kilaza tena hakukuwa na ufisadi na kusoma ilikuwa bureee bwerere tena yeye akiwa palepale jikoni enzi za analogue alikuwa na advantage. Lakini sasa yaonekana alikuwa mtoto wa kijiweni kupata stori za Yanga na Simba hivyo book haikuwa saana. Lakini jihadharini watu wa namna hiyo huwa pia ni TISS maana kipindi wanapotea wanaenda mazoezi wakirudi wanaibukia kwenye makampuni binafsi na mipira kama Azan
Mkuu tunaomba pia cv za wabunge wa chadema tulinganishe na hii.Ingekuwa ni vizuri mno
hilo nalo neno ndo maana wanaishia kuomba rushwa.mie naomba kiingereza kipitishwe wawe wanaongea bungeni wengine kila siku watakuwa wagonjwa.
Ni kweli kabisa flora msoffe haya majamaa majinga sana na yalaaniwe milelena ndo maana wanaua watu na kuwatwanga makonde badala
ya kutumia akili kutafuta suluhu
yanatumia nguvu sababu hayana akili
Ni kweli kabisa flora msoffe haya majamaa majinga sana na yalaaniwe milele
Hizo Diploma zina utata sidhani kama TCU wanazitambua incase unataka kuingia university ila tusimlamu maana tatizo ni wananchi wenyewe ambao wengi wana link kipaji cha mtu / umaarufu na uwezo wa kuongoza pia tatizo lingine ni tume ya uchaguzi/katiba inahitaji sifa moja kuu ambayo ni kujua kusoma na kuandika (in most cases ukiwa STD 7) mengine ni sifa za ziada.
Unaweza kuja Kimbunga na CV yako nzuri tena ukiwa na practical experience nzuri ila kwa kuwa jina lako sio kubwa itakuwia ngumu kupata kura kwa siasa zetu za Tanzania na ndio maana unakuta watu wanaanza kwenye vyama vidogo vidogo na wakati mwingine wanaanzisha mashindano ya mpira na kuyaita kombe la Kimbunga ili mradi jina lake liwemo midomoni mwa watu.
Ifike mahala vyama viangalie uwezo binafsi wa uongozi bila kujali anakubalika vipi kwa jamii ndio maana miaka ya nyuma mtu alikuwa anashinda katika ngazi ya mkoa jina likienda taifa wanaliengua na wakiweka mtu mwingine wanaweka mtu makini.
STD & si hoja ila anatakiwa awe jembe hasa kwa lugha ya sasa maana kuna wengine wanajua issues na mbinu za ku-network na wasomi mbalimbali. (CONCLUSION: Tunatakiwa tubadilishe kipengele cha sifa za mgombea ubunge ili tuwafanye watu wanaokimbilia kwenye siasa wa-activate vichwa vyao kwa kwenda shule vinginevyo mijadala mikubwa ya kisheria na mingine ambayo inatumia general knowledge kama mtu huna shule ya kueleweka itakuwa tabu.
Mkuu nilikuwa na mpango wa kuanzisha kombe la Mbuzi naona sasa nianzishe tu kombe la Kimbunga kutangaza jina ili 2015 nami nijikumbushe siasa.
Mkuu juzi juzi Kenya walijaribu kubadili sifa hasa za kielimu ili wabunge wawe wenye degree lakini kulikuwa na upinzani sijui uliishaje. Unapokuwa na watunga sheria wengi ambao wana sifa za chini usitegemee mabadiliko ya kuwaengua yapate njia nyepesi.
nchi hii haitapata kuendelea kama vilaza wanakaa mbele na wenye akili na ujuzi wanawekwa nyuma yao. Uzoefu wa miaka 50 hamsini umeonesha ni namna gani usawa wa binadamu hauwezi kuendekezwa katika kuendeleza nchi hii. Ni lazima tutoe nafasi wataalamu washike hatamu na watu wenye upeo wa kutosha kufanya maamuzi. Sasa nimeelewa ni kwanini ccm inafanya vituko. Tafsiri mbovu sana ya usawa wa binadamu. Livingstone, jah people, azzan na wengine hawana ubavu wa kupeleka mbele gurudumu la maendeleo ya nchi hii. Kuongoza sio kupiga kelele kuliko wengine au kuhimili kadamnasi . Ccm think twice, we are loosing at the expense of your bogus politicskwa mujibu wa kanuni za chaguzi za ccm, sifa ya elimu anayotakiwa kuwa nayo mbunge ni elimu ya darasa la saba. Nadhani mjadala ukielekea huko utakuwa na tija zaidi ili kama kuna haja ya kufanya marekebisho basi hoja zijengwe in that context. Vinginevyo kwa mujibu wa kanuni za chaguzi za ccm, mheshimiwa azzan ni mbunge halali kwani per kanuni za chama cha mapinduzi as of today, mgombea akiwa na kiwango cha elimu cha form four, form six, certificate, diploma, degree, n.k, hiyo inachukuliwa kama ni ziada tu na haipewi uzito na vikao vya kupitisha/kuchuja wagombea. Suala la elimu kwa sasa ni suala la wapiga kura mmoja kwa mmoja kuwa na uelewa tu kwamba je, itumike kama kigezo au lah.
Na mara nyingi ukiwa mgombea mwenye elimu kubwa, ni kawaida sana kujengewa fitina kwamba umechakachua au kampeni zako haziwatendei haki wagombea wasio na elimu, au kwamba peleka elimu yako kwingine ukajenge taifa, sio kwenye nafasi ya ubunge kwani mujibu wa kanuni ya ccm, darasa la saba linatosha, na wananchi hawana haja ya kuzingatia kiwango cha elimu kama ni kigezo cha kukuchagua kama mgombea/mbunge. Nadhani mjadala ungeelekezwa zaidi juu ya kanuni hii badala ya kumjadili mh azzan ambae katika mazingira haya, hana hatia na ni mwakilishi halali wa wananchi wa jimbo la kinondoni.
Tatizo hata mwanamke wake ambae ni mbunge wa chadema grace kiwelu hajaenda shule pia unategemea kuna kushauriana kuhusu kuongeza elimu kweli hapo????​
akiri zao ni kama za huyu jamaaNyinyiEM wengi ni vilaza wa Darasa la saba na form iv au kama ni prof basi ni wale aliwazungumzia Rev Peter(mb iringa)