Hii ndio Tanzania ya Magufuli, Unashangaa nini?

Hii ndio Tanzania ya Magufuli, Unashangaa nini?

Kutetea uongo na kuwa mnafiki unatakiwa kuwa na phd ya chama tawala. Yaani hadi ripoti ya cag na yenyewe haiwapi mwelekeo wapi tulipo na tunakoenda

Ndio . Tunasifia upepo kwa kuvuma na kusahau madhara yake. Tanzania hii kama tulitegemea wasomi imekula kwetu. Nani wa kusema na kusikika ? tunasubiri tuzame wote kwenye maji huku tunapiga kelele kuwa hatuzami.

inabowa sana. Hii nchi hii.......
 
Maombi yako waombee wazazi wako watoke kwenye umasikini - mwaka unaanza mpaka unakata ni MALALAMIKO na MANUNG'UNIKO tu - soon UTAOLEWA

Msamehe- Twendeni taratibu hapa jukwaani.
 
Wewe inaonekana una matatizo yako binafsi! Mbona Rais Magufuli anafanya vizuri tu!! Sema tu nyinyi ndiyo, kama wewe umetoka chuoni hivi karibuni, wale wanafunzi wenye mawazo ya kuajiliwa serikalini tu na hawataki kujituma kwa kutumia elimu yao kubadili hali inayowazunguka. Kama wewe ni muajiliwa, basi nyinyi ndiyo wale mliozoea kuiba hela ya serikali na sasa mianya hiyo imezibwa, mnaishia kulalama tu! Kwa ujumla, wakati nyinyi mnamlalamikia, sisi wengine tunamuona kama ni mkombozi wa Taifa letu kwa kuwa amebadilisha mfumo wa maisha na sasa ni heshima tu, nje na ndani ya nchi. ifikapo 2020, tutampigia kura nyingi za kutosha ili aweze kuendelea hadi 2025.

Nilitegemea utajibu maswali yake.
 
Nimegonga like bahati mbaya so siihesabu. Je, unafahamu hii report ni ya kuanzia mwaka gani mpaka mwaka gani? Hii ni ya mpaka June 30 2016. Unataka kuwadanganya nini watu wewe ndugu? Tatizo mnarukiaga magari kwa mbele. Someni muelewe.
Kwani june 2016 nani alikuwa presdaaa?
 
Wanasiasa ndivyo walivyo

Mahakama ya mafisadi imekosa kesi ,pesa zetu zimepotea bure

Tatizo nchi hii hata ukikosoa kwa nia njema unaitwa mpinzani,mara muuza ngada mara mpiga dili
 
Wewe inaonekana una matatizo yako binafsi! Mbona Rais Magufuli anafanya vizuri tu!! Sema tu nyinyi ndiyo, kama wewe umetoka chuoni hivi karibuni, wale wanafunzi wenye mawazo ya kuajiliwa serikalini tu na hawataki kujituma kwa kutumia elimu yao kubadili hali inayowazunguka. Kama wewe ni muajiliwa, basi nyinyi ndiyo wale mliozoea kuiba hela ya serikali na sasa mianya hiyo imezibwa, mnaishia kulalama tu! Kwa ujumla, wakati nyinyi mnamlalamikia, sisi wengine tunamuona kama ni mkombozi wa Taifa letu kwa kuwa amebadilisha mfumo wa maisha na sasa ni heshima tu, nje na ndani ya nchi. ifikapo 2020, tutampigia kura nyingi za kutosha ili aweze kuendelea hadi 2025.
UNAIJUA BEI YA UNGA WA SEMBE KWA SASA ?
 
Ni vizuri kwa kuwa umetumia neno "sisi wengine"! Hata siku moja haitatokea watu wote kuwa na mawazo au mtazamo unaofanana. Ambacho kinaweza kujadiliwa, labda, Rais anayejadiliwa katika andishi hili alipata asilimia 58 ya kura zote. Tuliambiwa na akina Nape kwamba kulikuwa na goli la mkono, akina Makamba Jr nao walicheza na teknolojia lakini wenzao walipotumia teknolojia ili kuizua teknolojia ya akina Makamba, wakakamatwa na kuswekwa ndani na kompyuta zao zikadukuliwa! Je, 2020 itakuwaje kwa kuangazia mazingira ya 2015 na kinaendelea kutokea sasa?
 
Msipende kupotosha watanzania. Someni muelewe. June 30 2016 serikali ilikuwa na miezi 8 tu. Ndiyo maana watu wametumbuliwa mkaanza makelele. Poleni sana. Magufuli tutamuongezea muda mpaka nchi inyooke.
Sio ninyi mliompongeza rais ndani ya siku 100 kafanikiwa kufanya makubwa ikiwemo kutokomeza rushwa na UFISADI? au 2016 alikua hajaanza kazi? tuachane na hayo, eleza ni mafisadi wangapi wamehukumiwa katika mahakama ya mafisadi?
hata usifie ujinga haitasaidia kitu kwa sasa, Nchi imekwenda mrama.
 
Hii ndio Tanzania yetu. Tanzania isiyokishwa kila aina ya maajabu. Na yumkini hayatakwisha kwa sababu ndio majaliwa yetu. Watu wanashangaa sana mimi nawashangaa hao wanaoshangaa hii Tanzania yetu ya awamu ya tano kwani mlitarajia nini ?

Kwamba unasema hutaki misaada ya masharti baadae unakubali imekuwaje ?

Makusanyo ya kodi yamepanda lakini utekelezaji wa bajeti za maendeleo haufiki hata asilimia 40% vipi tena . Huko halmashauri kumelalala fofofo vipi badala ya kuinuka na kuamka.

Unaunda mahakama ya mafisadi na kutumbuwa wanaoitwa mafisadi halafu mahakama inakosa mtu wa kushtakiwa punde ripoti ya CAG inaonesha ufisadi wa kutisha vipi ?

Unazuiya mikutano ya kisiasa ya hadhara halafu kutwa unatumia mikutano ya hadhara hiyo hiyo kushambuliya kila anaetofautiana nawe kimawazo vipi tena ?

Nchi ina manunguniko kila aina , badala ya kutafutwa suluhu unabeza na kudogosha mambo imekuwaje?

Tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 % lakini watu wanaachishwa kazi kila kukicha kwa ukata na bei za bidhaa zinapanda kuna nini ?

Tunachagizwa kuiombea mungu Tanzania yetu na rais wetu kila siku lakini mambo yanazidi kuwa magumu kunani ?

Unaahidi utawatendea haki watanzania wote lakini mbona kuna undumi la kuwili kwenye kutenda haki.

Unaahidi kushughulika na waliofoji vyeti unachukua hatua kwa baadhi lakini wengine wanaachwa kwa nini?

Unajisabu kusimamia sheria, sheria inavunjwa nyumbani mwako unanyamaza kimya na badala ya kuwashughulikia wavunja sheria, unawalinda na kushughulikia watetezi wa sheria kuna nini ?

Unataka kuijenga Tanzania ya viwanda, watu hawana maji, chakula na dawa, hawana afya wewe unajenga mji wa angani, wapi na wapi ?

MNASHANGAA NINI ?

Kwani hamjui kuwa kupanga ni kuchagua ? Kwani sisi tulipanga kweli? Hapana, leo hii mmesahau ?

Tulishakosea tokea awali, Tulikosea siku ile tulipoparaganyika kwa kushindwa kufanya maandalizi ya jemedari wetu. Wakati ulitusaliti tukafikiri kuwa yoyote anayetabasamu kuwa ni mwema, tulisahau kuwa kumbe ngoma ikivuma sana ndio hupasuka na tuliamini kuwa maneno ndio vitendo shangaeni tu.

Endeleeni kushangaa, shangaeni tu.

Ole wetu.

Iwafikie wote watu walio huru na GT pekee.

Kishada.
Na kweli ni only for GT.......
Nlifikiri kipa umbele kingekuwa
1. Elimi
2. Afya

Sasa tatizo ni International airport sehemu ambayo hata " Sesina" haiwezi kujaza abiria......
Upande wa Elimu tukafikiria watoto wanafeli sababu hawana madawati.....
Tukafikiria kuwabagua wanachuo kwa kutowapa mikopo ya elimu ya juu ndo kuinua kiwango cha elimu....
Wizara ya elimu ilifanya utafiti na kupata sababu ya nini kinawafanya wanafunzi wafeli?
Hatumpingi mkuu lakini tunakosoa pale pasipoenda sawa.
Wanaojidanganya heshima imerudi maofisini wajaribu kwenda hospitali za wilayani na vijijini
Waende halmshauri wafuatilie ulipwaji wa suppliers.....wanaofikiri rushwa zimeisha waende maofsi hayo hayo ya serikali waone vituko...TRA ni shida tupu...Traffic balaa tupu...
 
Wewe inaonekana una matatizo yako binafsi! Mbona Rais Magufuli anafanya vizuri tu!! Sema tu nyinyi ndiyo, kama wewe umetoka chuoni hivi karibuni, wale wanafunzi wenye mawazo ya kuajiliwa serikalini tu na hawataki kujituma kwa kutumia elimu yao kubadili hali inayowazunguka. Kama wewe ni muajiliwa, basi nyinyi ndiyo wale mliozoea kuiba hela ya serikali na sasa mianya hiyo imezibwa, mnaishia kulalama tu! Kwa ujumla, wakati nyinyi mnamlalamikia, sisi wengine tunamuona kama ni mkombozi wa Taifa letu kwa kuwa amebadilisha mfumo wa maisha na sasa ni heshima tu, nje na ndani ya nchi. ifikapo 2020, tutampigia kura nyingi za kutosha ili aweze kuendelea hadi 2025.
Jadili uhalisia acha vitu vya kusadikika...be objective n not subjective...mara kamaliza shule mara sijui wa kazini ..wewe cheki content kama ni za uongo sema uongo na si kurukaruka kama ndama hapa....don take it personal
 
Wewe inaonekana una matatizo yako binafsi! Mbona Rais Magufuli anafanya vizuri tu!! Sema tu nyinyi ndiyo, kama wewe umetoka chuoni hivi karibuni, wale wanafunzi wenye mawazo ya kuajiliwa serikalini tu na hawataki kujituma kwa kutumia elimu yao kubadili hali inayowazunguka. Kama wewe ni muajiliwa, basi nyinyi ndiyo wale mliozoea kuiba hela ya serikali na sasa mianya hiyo imezibwa, mnaishia kulalama tu! Kwa ujumla, wakati nyinyi mnamlalamikia, sisi wengine tunamuona kama ni mkombozi wa Taifa letu kwa kuwa amebadilisha mfumo wa maisha na sasa ni heshima tu, nje na ndani ya nchi. ifikapo 2020, tutampigia kura nyingi za kutosha ili aweze kuendelea hadi 2025.
Ni mtu mjinga peke yake atakayekimbialia kuwashutumu wahitimu wa chuo akiwaacha maprofesa wao ambao njaa inawaongoza kuwa makatibu wakuu na mawaziri wakizikana thesis zao kwa kuwa wameshindwa kujiajiri.

YAHERI MUNGU, Mungu akupe akili. Kuanguka kwa ajira kunawaathiri hata hao waliojiajiri. Tumia akili yako ndugu yangu, bidhaa unayozalisha ikikosa wateja basi kujiajiri kwako kumeingia dosari. Na ikiwa inaaminika kuwa VIJANA WANAPASWA TU KUJIAJIRI, kuna haja gani ya kuwasumbua vijana hao miaka 7 + 4 + 2 + 3 halafu waje kulima matikiti na kufuga kuku wa kisasa? Mbona Tupele anafuga kuku na aliishia darasa la 7?

Serikali ikikosa majibu ya ukosefu wa ajira isikimbilie 'MJIAJIRI', kwa maana katika miaka 7 + 4 + 2 + 3 kuna mwaka wowote umetengwa kuwafunda watu juu ya ujasiriamali?

Mimi humtukana mtu yeyote mnafiki. Jihesabu nimeshakutukana, maana ndio lililoko moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom