Hii ndio Tanzania ya Magufuli, Unashangaa nini?

Hii ndio Tanzania ya Magufuli, Unashangaa nini?

E.ngoyai lowasa alipata kusema.
"Hii nchi ni ya watu wa kulialia.
mkulima,analia,mfugaji analia,mwalimu analia,mkuu wa wilaya analia.mpaka mkuu wa .....analia.sasa ni muda wa kuchukua maamuzi si wa kulialia tena"
mleta mada bado unaendekeza kulialia.acha hizo.?

Vigezo na masharti kuzingatiwa. Mwandishi kawasilisha kwa niaba ya watanzania wengi.

Baada ya mwembwe zote hizo. basi angalia masuali na hoja. lete majibu.
 
Wewe inaonekana una matatizo yako binafsi! Mbona Rais Magufuli anafanya vizuri tu!! Sema tu nyinyi ndiyo, kama wewe umetoka chuoni hivi karibuni, wale wanafunzi wenye mawazo ya kuajiliwa serikalini tu na hawataki kujituma kwa kutumia elimu yao kubadili hali inayowazunguka. Kama wewe ni muajiliwa, basi nyinyi ndiyo wale mliozoea kuiba hela ya serikali na sasa mianya hiyo imezibwa, mnaishia kulalama tu! Kwa ujumla, wakati nyinyi mnamlalamikia, sisi wengine tunamuona kama ni mkombozi wa Taifa letu kwa kuwa amebadilisha mfumo wa maisha na sasa ni heshima tu, nje na ndani ya nchi. ifikapo 2020, tutampigia kura nyingi za kutosha ili aweze kuendelea hadi 2025.
Mfumo upi wa maisha uliobadilishwa??? Mi naona kabadili mfumo wa maisha kuwa mgumu zaidi,maisha kila mahali yamekuwa magumu sana.Na isitoshe kuna mfumuko wa bei mkubwa sana,Biashara kote zimedorora,maisha ni magumu sana huku mitaani hali si shwari mi binafsi ni mfanyabiashara toka nianze biashara 2001 sijawahi kukutana na dolo kama hii unakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni pesa unayoingiza ni aibu najiuliza tu kama ikifika miaka mitano hali hii hii tutakaofunga biashara tutakuwa wengi sana na hili suala msilichulie kisiasa mi binafsi namkubali rais huyu kwa baadhi ya mambo kafanya mema Ila Mengi kaharibu sana na atazidi kuharibu kwa sababu ya ujeuri na ukorofi wake wananchi wengi watafeli sana na naona gepu kubwa baina ya wenye nacho na wasionacho mpaka sasa hali hii sielewi itaisha lini
Hii ndio Tanzania yetu. Tanzania isiyokishwa kila aina ya maajabu. Na yumkini hayatakwisha kwa sababu ndio majaliwa yetu. Watu wanashangaa sana mimi nawashangaa hao wanaoshangaa hii Tanzania yetu ya awamu ya tano kwani mlitarajia nini ?

Kwamba unasema hutaki misaada ya masharti baadae unakubali imekuwaje ?

Makusanyo ya kodi yamepanda lakini utekelezaji wa bajeti za maendeleo haufiki hata asilimia 40% vipi tena . Huko halmashauri kumelalala fofofo vipi badala ya kuinuka na kuamka.

Unaunda mahakama ya mafisadi na kutumbuwa wanaoitwa mafisadi halafu mahakama inakosa mtu wa kushtakiwa punde ripoti ya CAG inaonesha ufisadi wa kutisha vipi ?

Unazuiya mikutano ya kisiasa ya hadhara halafu kutwa unatumia mikutano ya hadhara hiyo hiyo kushambuliya kila anaetofautiana nawe kimawazo vipi tena ?

Nchi ina manunguniko kila aina , badala ya kutafutwa suluhu unabeza na kudogosha mambo imekuwaje?

Tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 % lakini watu wanaachishwa kazi kila kukicha kwa ukata na bei za bidhaa zinapanda kuna nini ?

Tunachagizwa kuiombea mungu Tanzania yetu na rais wetu kila siku lakini mambo yanazidi kuwa magumu kunani ?

Unaahidi utawatendea haki watanzania wote lakini mbona kuna undumi la kuwili kwenye kutenda haki.

Unaahidi kushughulika na waliofoji vyeti unachukua hatua kwa baadhi lakini wengine wanaachwa kwa nini?

Unajisabu kusimamia sheria, sheria inavunjwa nyumbani mwako unanyamaza kimya na badala ya kuwashughulikia wavunja sheria, unawalinda na kushughulikia watetezi wa sheria kuna nini ?

Unataka kuijenga Tanzania ya viwanda, watu hawana maji, chakula na dawa, hawana afya wewe unajenga mji wa angani, wapi na wapi ?

MNASHANGAA NINI ?

Kwani hamjui kuwa kupanga ni kuchagua ? Kwani sisi tulipanga kweli? Hapana, leo hii mmesahau ?

Tulishakosea tokea awali, Tulikosea siku ile tulipoparaganyika kwa kushindwa kufanya maandalizi ya jemedari wetu. Wakati ulitusaliti tukafikiri kuwa yoyote anayetabasamu kuwa ni mwema, tulisahau kuwa kumbe ngoma ikivuma sana ndio hupasuka na tuliamini kuwa maneno ndio vitendo shangaeni tu.

Endeleeni kushangaa, shangaeni tu.

Ole wetu.

Iwafikie wote watu walio huru na GT pekee.

Kishada.
 
mtoa post andiko lako lingekuwa limeandikwa kwene magazet lingekuwa na mashko sana lkn humu waptiaj n wachache na hawa athar yoyote zaid ya maneno ya mihemko na upumbav2 unaotolewa na wanufaika na utawala huu!
 
Mnaleta utani kwenye mambo muhimu. Wewe unawahakikishia watu amani lakini ndio kwanza watu wanauawa na kupotezwa.

unasema hutawaangusha watu leo mwaka mmoja na nusu utafikiri bado tuko kwenye kampeni lakini uwaangushe vipi tena na fedha haionekani na biashara imebuma? . Vipi walau umeajiri ? au ndio tujiajiri wenyewe sote serikali haitaki tena waajiriwa?

Lete walau ufafanuzi wa kitaalamu kwa nini uchumi ukue lakini watu wanazidi kuachishwa kazi kwa ukata na biashara kukoma. mnaleta utani ?

Bibi yangu aliyemzaa Mama yangu mzazi"
ana umri wa miaka 86" Sikuzote hutuadithia maisha yake halisi na kusema...

Haijawahi hata siku moja' kuambulia pesa za serikali...! Hata nilipofikia hali ya uzee;
nilisikia tu kuwa kuna fungu la wazee" na
nilipofuatilia nikaambiwa pesa zilishaletwa
zipo huko huko kwenu..chamsingi nenda
serikali za mitaa...nikienda serikali za mitaa; naambiwa niende wilayani; nikienda wilayani naambiwa nenda mahakamani;
nikienda mahakamani; naambiwa njoo na Cheti cha kuzaliwa au cheti cha ndoa au passport 'hati ya kusafiria' alafu niende na
mshtakiwa• ndipo watanisaidi..! vinginevyo...nitoke nje nikaliangalie jua'
kama linaanza kuzama...*niwahi haraka nyumbani" nisije nikaliwa na simba.••

Lakini awamu hii ya 5" nashukulu sana
kwa maana serilkali inajua thamani yetu'
Pia imetushauri tufungue vikoba ili kujiendeleza kimaisha. Humaliza kwa
kusema....wajukuu zangu.." jitidini
kutofautisha Uchama na Utendaji kazi• ni
vitu viwili tofauti......

By:Tooth Brush@ chini ya uzamini wa
Hapa Kazi Tu....
 
Hii ndio Tanzania yetu. Tanzania isiyokishwa kila aina ya maajabu. Na yumkini hayatakwisha kwa sababu ndio majaliwa yetu. Watu wanashangaa sana mimi nawashangaa hao wanaoshangaa hii Tanzania yetu ya awamu ya tano kwani mlitarajia nini ?

Kwamba unasema hutaki misaada ya masharti baadae unakubali imekuwaje ?

Makusanyo ya kodi yamepanda lakini utekelezaji wa bajeti za maendeleo haufiki hata asilimia 40% vipi tena . Huko halmashauri kumelalala fofofo vipi badala ya kuinuka na kuamka.

Unaunda mahakama ya mafisadi na kutumbuwa wanaoitwa mafisadi halafu mahakama inakosa mtu wa kushtakiwa punde ripoti ya CAG inaonesha ufisadi wa kutisha vipi ?

Unazuiya mikutano ya kisiasa ya hadhara halafu kutwa unatumia mikutano ya hadhara hiyo hiyo kushambuliya kila anaetofautiana nawe kimawazo vipi tena ?

Nchi ina manunguniko kila aina , badala ya kutafutwa suluhu unabeza na kudogosha mambo imekuwaje?

Tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 % lakini watu wanaachishwa kazi kila kukicha kwa ukata na bei za bidhaa zinapanda kuna nini ?

Tunachagizwa kuiombea mungu Tanzania yetu na rais wetu kila siku lakini mambo yanazidi kuwa magumu kunani ?

Unaahidi utawatendea haki watanzania wote lakini mbona kuna undumi la kuwili kwenye kutenda haki.

Unaahidi kushughulika na waliofoji vyeti unachukua hatua kwa baadhi lakini wengine wanaachwa kwa nini?

Unajisabu kusimamia sheria, sheria inavunjwa nyumbani mwako unanyamaza kimya na badala ya kuwashughulikia wavunja sheria, unawalinda na kushughulikia watetezi wa sheria kuna nini ?

Unataka kuijenga Tanzania ya viwanda, watu hawana maji, chakula na dawa, hawana afya wewe unajenga mji wa angani, wapi na wapi ?

MNASHANGAA NINI ?

Kwani hamjui kuwa kupanga ni kuchagua ? Kwani sisi tulipanga kweli? Hapana, leo hii mmesahau ?

Tulishakosea tokea awali, Tulikosea siku ile tulipoparaganyika kwa kushindwa kufanya maandalizi ya jemedari wetu. Wakati ulitusaliti tukafikiri kuwa yoyote anayetabasamu kuwa ni mwema, tulisahau kuwa kumbe ngoma ikivuma sana ndio hupasuka na tuliamini kuwa maneno ndio vitendo shangaeni tu.

Endeleeni kushangaa, shangaeni tu.

Ole wetu.

Iwafikie wote watu walio huru na GT pekee.

Kishada.
KISHADA,mimi nimekuelewa vizuri sana,mimi binafsi wala sishangai niliyatarajia hayo.
 
endelea kupotezea mada na kushangaa. Hutaelewa

Vigezo na masaharti kuzingatiwa

Nimeeleweshwa' nimeelewa' na sasa ni zamu yangu kuwaelewesha wengine..."
kwamba NGADA, MIRUNGI, BANGI, USHOGA, UFISADI na RUSHWA...! ni hatari katika taifa letu
 
Si rahisi kama unavyodhani , hebu muulize Waziri wa kazi kama aliwahi hata kusuka ukili na kuuza kabla ya kuajiriwa .

Sasa kwani wewe ni waziri wa kazi? Mi naongea na wewe uliyesoma halafu unasubiri kuajiriwa tu. Sijui ambao hawajasoma wasemeje sasa [emoji849][emoji849]
 
Sasa kwani wewe ni waziri wa kazi? Mi naongea na wewe uliyesoma halafu unasubiri kuajiriwa tu. Sijui ambao hawajasoma wasemeje sasa [emoji849][emoji849]
Mimi ni mfanyabiashara tajiri niliyetoa ajira kwa zaidi ya watanzania 300 , huwa tunaleta hoja humu ili kutetea hawa masikini wa nchi hii na kuikumbusha serikali kuhusu wajibu wake .

Sina , sijawahi na sitegemei kuwa na njaa ya kunishawishi kuomba ajira kwenye serikali ya Tanzania .
 
Kama ni hivyo safi sana ila usiendelee kuwashawishi wasomi kutafuta ajira na badala yake washawishi wawe kama wewe (watengeneze ajira) za kutosha ili wasio soma waajiriwe pia.
 
Back
Top Bottom