Ni mtu mjinga peke yake atakayekimbialia kuwashutumu wahitimu wa chuo akiwaacha maprofesa wao ambao njaa inawaongoza kuwa makatibu wakuu na mawaziri wakizikana thesis zao kwa kuwa wameshindwa kujiajiri.
YAHERI MUNGU, Mungu akupe akili. Kuanguka kwa ajira kunawaathiri hata hao waliojiajiri. Tumia akili yako ndugu yangu, bidhaa unayozalisha ikikosa wateja basi kujiajiri kwako kumeingia dosari. Na ikiwa inaaminika kuwa VIJANA WANAPASWA TU KUJIAJIRI, kuna haja gani ya kuwasumbua vijana hao miaka 7 + 4 + 2 + 3 halafu waje kulima matikiti na kufuga kuku wa kisasa? Mbona Tupele anafuga kuku na aliishia darasa la 7?
Serikali ikikosa majibu ya ukosefu wa ajira isikimbilie 'MJIAJIRI', kwa maana katika miaka 7 + 4 + 2 + 3 kuna mwaka wowote umetengwa kuwafunda watu juu ya ujasiriamali?
Mimi humtukana mtu yeyote mnafiki. Jihesabu nimeshakutukana, maana ndio lililoko moyoni mwangu.