Hii ndio Tanzania yetu. Tanzania isiyokishwa kila aina ya maajabu. Na yumkini hayatakwisha kwa sababu ndio majaliwa yetu. Watu wanashangaa sana mimi nawashangaa hao wanaoshangaa hii Tanzania yetu ya awamu ya tano kwani mlitarajia nini ?
Kwamba unasema hutaki misaada ya masharti baadae unakubali imekuwaje ?
Makusanyo ya kodi yamepanda lakini utekelezaji wa bajeti za maendeleo haufiki hata asilimia 40% vipi tena . Huko halmashauri kumelalala fofofo vipi badala ya kuinuka na kuamka.
Unaunda mahakama ya mafisadi na kutumbuwa wanaoitwa mafisadi halafu mahakama inakosa mtu wa kushtakiwa punde ripoti ya CAG inaonesha ufisadi wa kutisha vipi ?
Unazuiya mikutano ya kisiasa ya hadhara halafu kutwa unatumia mikutano ya hadhara hiyo hiyo kushambuliya kila anaetofautiana nawe kimawazo vipi tena ?
Nchi ina manunguniko kila aina , badala ya kutafutwa suluhu unabeza na kudogosha mambo imekuwaje?
Tunaambiwa uchumi unakuwa kwa asilimia 7 % lakini watu wanaachishwa kazi kila kukicha kwa ukata na bei za bidhaa zinapanda kuna nini ?
Tunachagizwa kuiombea mungu Tanzania yetu na rais wetu kila siku lakini mambo yanazidi kuwa magumu kunani ?
Unaahidi utawatendea haki watanzania wote lakini mbona kuna undumi la kuwili kwenye kutenda haki.
Unaahidi kushughulika na waliofoji vyeti unachukua hatua kwa baadhi lakini wengine wanaachwa kwa nini?
Unajisabu kusimamia sheria, sheria inavunjwa nyumbani mwako unanyamaza kimya na badala ya kuwashughulikia wavunja sheria, unawalinda na kushughulikia watetezi wa sheria kuna nini ?
Unataka kuijenga Tanzania ya viwanda, watu hawana maji, chakula na dawa, hawana afya wewe unajenga mji wa angani, wapi na wapi ?
MNASHANGAA NINI ?
Kwani hamjui kuwa kupanga ni kuchagua ? Kwani sisi tulipanga kweli? Hapana, leo hii mmesahau ?
Tulishakosea tokea awali, Tulikosea siku ile tulipoparaganyika kwa kushindwa kufanya maandalizi ya jemedari wetu. Wakati ulitusaliti tukafikiri kuwa yoyote anayetabasamu kuwa ni mwema, tulisahau kuwa kumbe ngoma ikivuma sana ndio hupasuka na tuliamini kuwa maneno ndio vitendo shangaeni tu.
Endeleeni kushangaa, shangaeni tu.
Ole wetu.
Iwafikie wote watu walio huru na GT pekee.
Kishada.