Hii ndio Ndege Tupolev Tu-160, hatari ya kivita inayoumiza vichwa maadui

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Dec 20, 2012
195
537
tu160_2.jpg


Nami Josephat Keraryo Nyambeya.

Kama nilivyoahidi juzi baada ya kutoa uchambuzi kiduchu juu ya bomber (B-2) ya Marekani nilisema nitakuja na uchambuzi kiduchu juu ya Tu-160 kutoka Urusi ili kuleta balansi juu ya ushindani uliopo kati ya hawa mabwana .Leo ningependa kuendelea na ule uandishi wangu kiduchu juu ya masuala mbalimbali kama ilivyo kawaida yangu siku zote.

Leo ninapenda kujikita kwenye ndege vita aina ya Bombers lakini leo nitakuwa ninaijadili ndege vita hatari sana kutoka Urusi ambayo inaumiza watu vichwa haswa upande wa Magharibi (USA+NATO) kwa jinsi ilivyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, japo wafuatiliaji na wachambuzi wa mambo ya Kijeshi na Teknolojia za ndege wanadai kuwa ile Bomber (B-2 niliyoijadili juzi ndio hatari zaidi duniani).

Tu-160 (Tupolev Tu-160) ikijulikana kama Blackjack kwa wanachama wa NATO ilianza kutengezwa kipindi cha vita baridi. Ndege hii ilitengenezwa na Tupolev and Kazan Aircraft Production Associatio Bomber hii hatari ya kivita ilitengenezwa kwa lengo moja kuu la kuweza kuzivamia na kuzishambulia sehemu muhimu za Marekani.

Ikiwa inafanana sawa sawa na B-1B ya Marekani, hii ndio ndege vita (Bomber) nzito kuliko zote duniani ikiwa na uzito wa tani 275. Ndege hii inaweza kubeba silaha za kivita (Mabomu, Vichwa vya Nyuklia, Makombora ya kushambulia) yenye uzito wa Tani 40.

Naomba ifahamike kuwa hakuna ndege vita aina ya Bomber kwa upande wa Marekani yenye kuweza kubeba silaha nzito namna hiyo kwa sasa labda kama ipo kiwandani ikitengenezwa (kwa Marekani B-1Bndio inabeba silaha za uzito wa tani 34) na kama nilivyotangulia kusema ni kuwa Tu-160 ilitengenezwa kuja kushindana na B-1B ya Marekani.

Inaaminika kuwa jumla ya ndege vita hizi 39 zilitengenezwa lakini kutokana na gharama kubwa za uendeshaji na matunzo Jeshi la Wanahewa la Urusi linasadikika kuwa na jumla ya ndege hizi 16 tu kwa sasa. Na zipo aina nane za ndege hii.

Tu-160 ilipaa kwa mara ya kwanza mwaka 1981 na baada ya kuona haijakidhi matakwa kama walivyotarajia wahandisi wa ndege hii waliingiza tena kwenye sevisi mwaka 1987. Tu-160 inaweza kufanya kazi katika hali yoyote ya hewa, mchana, usiku na ina operate katika latitude zote za Kijografia. Ina mfumo wa kuijaza mafuta ikiwa angani na pia ina injini nne za Turbofan. Inakimbia kwa mwendokasi wa kilomita 2220 kwa saa.

Tu-160 ina mfumo wa kubeba makombora ya masafa marefu ya kushambulia aina ya Kh-55 na Kh-15. Pamoja na mambo mazuri iliyona nayo ndege hii hatari ya kivita bado ina mfumo hafifu wa rada. Hivyo kuwapa uwezekano maadui wa kuiona kwenye rada zao.

Tu-160 kumi na tisa zilibaki nchi Ukraine baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisoviet (USSR) mwaka 1991, Urusi ilijitahidi kuzirudisha kwa makubaliano na Urusi hatimae ndege hizi 8 kati ya 19 zilirudishwa nchini Urusi mwaka 1999, na zingine zilizobaki zilifanywa Skrepa kwa makubaliano yaliyoongozwa na Marekani (Udhaifu huu).

Kuanzia mwaka 2014 ndege hizi zinafanyiwa matengenezo na marekebisho ikiwemo kurekebisha mfumo wake wa radar , inategemewa kufikia 2020 ndege zote zitakuwa zimekamilika .Pia pamoja na marekebebisho hayo Urusi pia imeamua kutengeneza version mpya ya ndege hizi itakayojulikana kama Tu-160M2 ambayo itakuwa imara na ya kisasa zaidi ya hii iliyopo,

project hii inaendelea kwa sasa na inatarajiwa kukamilika baada ya miaka michache tokea sasa. Marekani iliutumia udhaifu wa kuvunjika kwa Muungano wa Kisoviet kumrubuni mshirika wake Ukraine na kuzinyaka ndege tatu za Tu-160 na kuzigeuza kuwa Tu-16SK kwa ajili ya space vehicle launching.

Sifa zingine ilizonazo ndege hii ni kuwa inaweza kupaa angani kwa masaa 15 mfululizo bila kujazwa mafuta kama itakuwa inakimbia kwa kwa kasi ya kilomita 850 kwa saa, pia ina uwezo wa kujazwa mafuta tani 130 kwa mara moja. Inapaa umbali wa futi 30,003 sawa na mita 9145.

Udhaifu wake mkubwa ni kuwa inaonekana kwenye RADA na kupaa umbali mfupi tofauti na B-2 ya Marekani ambayo haionekani kwenye rada na inapaa zaidi ya futi 50,000 juu. Mwaka 2010 ndege mbili za Tu-160 zilivunja rekodi ya kufanya Patrol ya masaa 23 mfululizo bila kutua ardhini.

Ifahamike kuwa kwa sasa Marekani wanaiboresha ndege yao (Bomber0 hatari ya B-2 na wanataka kuja na B-21 kama mbadala wa B-2 huku Urusi nao wakilenga kuja na Tu-160M2 kama mbadala wa Tu-160. Wenzetu hawalali, wanaumiza vichwa kutengeneza vitu vya kuvunja rekodi, sisi Tanzania na Afrika tunavunja rekodi ya kumezeshana Madesa tusiyoyatumia mara baada ya kuhitimu Elimu zetu, hivyo kujikuta tunabakia kuwa watumwa wa watu haswa wanasiasa badala ya kuwa sisi ndio dira yao, wanasiasa wanageuka kuwa Dira ya wataalamu kiduchu tulionao.

Unaweza wasiliana nami kupitia +255653737353 (WhatsApp) au nyambeya@yahoo.com
 
hiyo ndege si ya kitoto,inakaua sawa na B-2 japo yenyewe sio stealthbomber,na haihitaji kuwa stealth kwani inauwezo wa kurusha cruiser missili toka umbali wa km 7000 na ikahiti target bila hata kuingia katika
 
Hebu tupatie maelezo ya ndege mpya ya China iliyozinduliwa mwezi Octoba 2016 ambayo imeelezwa ndio ndege bora zaidi ya kivita Duniani.
 
Sisi bado tunabana matumizi na kukagua kama kuna ndege hewa.
 
Mikwara hii ya kila siku
Wanamtengenezea nani!!
Wanatengeneza kabla yakutumika
Inakuwa haifai !!
 
Nakubaliana na uchambuzi wako lakini T-160 Black jack sidhani km inabeba Tani kuliko B-52 bomber ya Us....
 
Back
Top Bottom