econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 24,160
- 37,888
Tahadhari huu Uzi Una Ukakasi kwa baadhi ya watu :
Hii habari nimeipata baada ya Kuangalia KTN Television inchini Kenya ni habari ya kichunguzi katika nyumba za ibada.
Hawa ni Manabii WA kizazi hiki na majina Yao makubwa makubwa mara Mtume mkuu,Nabii na kadhalika,jinsi wanavyofanya utapeli kuwahadaa kondoo wao kuendelea kuwapiga mahela.
Ziligundulika mbinu zifuatazo:
Mosi, kuwapanga watu watoe shuhuda mbali mbali ikiwemo kuugua ukimwi na maradhi mengine mbali mbali na kisha baadae kusema wamepona,na wengine hurekodiwa na kurushwa katika Redio kana kwamba wako live wanapiga simu lkn kumbe walicheza Hilo picha kitambo Tu.
Kutolewa vitu mwilini kwa Miujiza lakini ni uwongo mtupu,mfano walionekana watu wanaweka miguu katika mabeseni na kuoshwa miguu na maji kuwa mekundu, kumbe kuna kemikali moja wachungaji wanapaka katika mikono Yao halafu baada ya mda mfupi wakiwa wanasugua miguu ya kondoo wao inayeyuka na maji yanakuwa mekundu. Hapo inasemwa umetolewa uchawi na mabalaa kumbe ni upigaji Tu.
Wanapangwa vilema wa uongo ambao wanafundishwa namna ya.kucheza na viungo vyao na kweli ukiwaona utadhani ni vilema kweli lakini kumbe ni sarakasi za 5G!
Sasa kubwa kuliko yote ambayo watu wengi hawajui ni kuwepo na watu special ambao kazi yao ni kuwatambua kondoo wapya katika kanisa lao. Hawa wakisha kulenga basi watakuja ulipo kaa na kuzungumza na wewe mawili matatu na mwisho wa siku utatoa changamoto zako.
Sasa anakuwa makini kusikiliza halafu anaenda kwenye daftar na kuandika jina lako na changamoto zako mbalimbali, halafu zile data anapewa Nabii au Mtume whatever the case, huenda zikapita siku tatu au nne au hata wiki.
Unashangaa siku Nabii anakuita wewe fulani au wewe mama mwenye kitenge fulani njoo hapa madhabauni kuna kitu nimeona, anaanza kutaja changamoto zako na ukicheki ni kweli. Kwa ubwege wako ushasahau kuwa kuna siku uliuza faili lako lote kwa kondoo wenzako.
Basi utaona daah umekutana na bonge la Nabii kumbe upuuzi mtupu, hapo unaaza kupigwa mahela mwanzo mwisho.
Hilo nimelidhibitisha kwa mtu wangu wa karibu hapa Tanzania, alienda Kanisa fulani yeye ni Muislamu, akaenda Kanisa fulani, akaambiwa wewe si umeolewa mke wa pili, kuna changamoto moja mbili tatu na kweli Nabii anagusa mule mule. Lakini alishasahau kuna kipindi alikutana na mdada mwenzake kanisani na kuuza faili lake, haya mambo yapo sana.
Na wengine utasikia huyu Nabii yaani anaona sana, yaani ana maono hatari kumbe wanapiga ramli au wanashirikiana na wapiga ramli, unamuona ana maono kumbe mshirikina tu.
Unaweza ingia YouTube na kusechi hii clip na ukajionea mambo kibao, nimekupa kwa uchache Tu.
Kutoka kwangu ETUGRUL BEY
Ni hayo tu!
Aisee anaitwa pastor Kanyari tapeli namba moja. Cha kushangaza mpaka leo watu wanamfuata.