Hii ndio miujiza inayowachanganya watu

Hii ndio miujiza inayowachanganya watu

Yule mwandisha Mohammed Ali wa Kenya aliwahi kulifanyia uchunguzi hili kwa kweli ilikuwa ni bonge la noma, hapa bongo hatujapata waandishi wa namna hii.. ile topic iliitwa makri ya injili kama sikosei
Alimchunguza dr.kanyari jamaa tapeli sana anajiita nabii, .......huku bongo useme ufanye hivyo utakoromewa mbaya na wafia dini
 
Ushaingiza udini tayari hapo!

Ikitandazwa hoja mezani, tuwe tunaijadili hiyo hiyo bila kuruka fensi.

Ukisharuka uzio, akili yako inadumaa na kubweteka kushindwa kuwaza nje ya box, ninamaanisha habari hata ikiletwa wewe ukaiona ni ya mrengo fulani ama ni ya kipumbafu, jikite kuangazia context yake tu.

Tujiepushe kuegemea udini, uchama na ukanda vinavyoweza kutubungua na kutupukutisha nafsi zetu.
Asante mkuu

Itoshe kusema Tu kuwa hii comment iwekewe lamination chap
 
Alichokisema ni ukweli mtupu,Ukristo unatumika sana kutapeli watu kwa shuhuda za uongo,
Unaweza kuthibitisha hili ?
Nilikuwa mbagala nikaona masheikh wanawapa watu Kinga za majini ule sio utapeli.
Waislam wengi waganga na waganga wengi n watu hatari Mana Ni wachawi wale wale, Je sio utapeli ?
 
Kuna mchungungaji juzi naee kacheza mchezo Kama huo.kaja ukumbini kwake mapema asubuhi nawaumini wake kaawambia wawahi wakafanya hivyo.sasa wakati anaendelea kuombea namikelele yake ghafla ikaja gari imejaza watu ndani ikasimama nje yaukumbi.dereva akatoka akaingia ndani yaukumbi akatoka namchungaji mchungaji alivyofungua mlango akawa anafoka kwakuomba kumbe wale watu wanadai yule anae ombewa nimsukule walisha mzika miaka kumi ilio pita ila walivyo kuja kuombewa na kuchukua mafuta wakaenda kumwaga nyumbani ndio huo msukule ukatoka.kwahio wakasema wamekuja kutoa ushuhuda.msukule ukawekwa pembeni yaukumbi mchungaji akawambia waumini wainuke wakashuhudie muujiza alio ufanya.nasisi tukapata fursa yakuona.ulemsukule unatisha kwakweli unatema maudendatu mikucha inarangi nyeusi minywele Kama yamzungu inarangi nyeusi tiii.ukiangalia maramoja hutamani kurudia.baada yakufanya hivyo sasa hivi anawaumini balaa.
Tafuta mtu anaitwa Mussa chesaa kawauzia watumishi wa uongo wengi sana misukule alikuwa anakula nao dili
 
Tahadhari huu Uzi Una Ukakasi kwa baadhi ya watu :

Hii habari nimeipata baada ya Kuangalia KTN Television inchini Kenya ni habari ya kichunguzi katika nyumba za ibada.

Hawa ni Manabii WA kizazi hiki na majina Yao makubwa makubwa mara Mtume mkuu,Nabii na kadhalika,jinsi wanavyofanya utapeli kuwahadaa kondoo wao kuendelea kuwapiga mahela.

Ziligundulika mbinu zifuatazo:

Mosi, kuwapanga watu watoe shuhuda mbali mbali ikiwemo kuugua ukimwi na maradhi mengine mbali mbali na kisha baadae kusema wamepona,na wengine hurekodiwa na kurushwa katika Redio kana kwamba wako live wanapiga simu lkn kumbe walicheza Hilo picha kitambo Tu.

Kutolewa vitu mwilini kwa Miujiza lakini ni uwongo mtupu,mfano walionekana watu wanaweka miguu katika mabeseni na kuoshwa miguu na maji kuwa mekundu, kumbe kuna kemikali moja wachungaji wanapaka katika mikono Yao halafu baada ya mda mfupi wakiwa wanasugua miguu ya kondoo wao inayeyuka na maji yanakuwa mekundu. Hapo inasemwa umetolewa uchawi na mabalaa kumbe ni upigaji Tu.

Wanapangwa vilema wa uongo ambao wanafundishwa namna ya.kucheza na viungo vyao na kweli ukiwaona utadhani ni vilema kweli lakini kumbe ni sarakasi za 5G!

Sasa kubwa kuliko yote ambayo watu wengi hawajui ni kuwepo na watu special ambao kazi yao ni kuwatambua kondoo wapya katika kanisa lao. Hawa wakisha kulenga basi watakuja ulipo kaa na kuzungumza na wewe mawili matatu na mwisho wa siku utatoa changamoto zako.

Sasa anakuwa makini kusikiliza halafu anaenda kwenye daftar na kuandika jina lako na changamoto zako mbalimbali, halafu zile data anapewa Nabii au Mtume whatever the case, huenda zikapita siku tatu au nne au hata wiki.

Unashangaa siku Nabii anakuita wewe fulani au wewe mama mwenye kitenge fulani njoo hapa madhabauni kuna kitu nimeona, anaanza kutaja changamoto zako na ukicheki ni kweli. Kwa ubwege wako ushasahau kuwa kuna siku uliuza faili lako lote kwa kondoo wenzako.

Basi utaona daah umekutana na bonge la Nabii kumbe upuuzi mtupu, hapo unaaza kupigwa mahela mwanzo mwisho.

Hilo nimelidhibitisha kwa mtu wangu wa karibu hapa Tanzania, alienda Kanisa fulani yeye ni Muislamu, akaenda Kanisa fulani, akaambiwa wewe si umeolewa mke wa pili, kuna changamoto moja mbili tatu na kweli Nabii anagusa mule mule. Lakini alishasahau kuna kipindi alikutana na mdada mwenzake kanisani na kuuza faili lake, haya mambo yapo sana.

Na wengine utasikia huyu Nabii yaani anaona sana, yaani ana maono hatari kumbe wanapiga ramli au wanashirikiana na wapiga ramli, unamuona ana maono kumbe mshirikina tu.

Unaweza ingia YouTube na kusechi hii clip na ukajionea mambo kibao, nimekupa kwa uchache Tu.

Kutoka kwangu ETUGRUL BEY

Ni hayo tu!
🚮🚮 Umeandika stori za kijiwe cha wasio na elimu ya dini. Kwa nyomi kama ya mwamposa utakariri na kuwapanga wangapi sasa??
 
“kwa ubwege wako ushasahau kuwa kuna siku uliuza faili lako lote kwa kondoo wenzako"

Nimecheka sana hii sentence [emoji23][emoji23][emoji23]
 
🚮🚮 Umeandika stori za kijiwe cha wasio na elimu ya dini. Kwa nyomi kama ya mwamposa utakariri na kuwapanga wangapi sasa??

Mkuu usipagawe na nyomi hata kidogo kuna namna nyingi ya kuratibu mambo.

Kwa mfano wale ambao mara nyingi hukaa mbele pale baadhi Yao wameshapangwa,unakuta wametawanyika huku huku.

Ishu ya vilema iko hivi, Kwa mfano labda mwamba anatarajia kufanya ziara mbali mbali mikoani,basi Kwa kila mkoa huenda hata mwezi mzima au wiki mbili wanamwagwa vilema feki wanakuwa around hapo na kuonekana na baadhi ya watu na kuzoeleka then siku ya siku anakuja mwamba na mambo yake jamaa wanakuwa mbele hapo wanaitwa na kupokea Miujiza feki.

Kifupi hao jamaa wanajua wanachofanya ni juu yako kuamini au kutoamini.

Sijui kama umeangalia hiyo video JICHO PEVU, huko kuna Siri zao kubwa zimeanikwa.
 
Back
Top Bottom