Hii ndio miujiza inayowachanganya watu

Hii ndio miujiza inayowachanganya watu

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
13,644
Reaction score
27,537
Tahadhari huu Uzi Una Ukakasi kwa baadhi ya watu :

Hii habari nimeipata baada ya Kuangalia KTN Television nchini Kenya ni habari ya kichunguzi katika nyumba za ibada.

Hawa ni Manabii WA kizazi hiki na majina Yao makubwa makubwa mara Mtume mkuu,Nabii na kadhalika,jinsi wanavyofanya utapeli kuwahadaa kondoo wao kuendelea kuwapiga mahela.

Ziligundulika mbinu zifuatazo:

Mosi, kuwapanga watu watoe shuhuda mbali mbali ikiwemo kuugua ukimwi na maradhi mengine mbali mbali na kisha baadae kusema wamepona,na wengine hurekodiwa na kurushwa katika Redio kana kwamba wako live wanapiga simu lkn kumbe walicheza Hilo picha kitambo Tu.

Kutolewa vitu mwilini kwa Miujiza lakini ni uwongo mtupu,mfano walionekana watu wanaweka miguu katika mabeseni na kuoshwa miguu na maji kuwa mekundu, kumbe kuna kemikali moja wachungaji wanapaka katika mikono Yao halafu baada ya mda mfupi wakiwa wanasugua miguu ya kondoo wao inayeyuka na maji yanakuwa mekundu. Hapo inasemwa umetolewa uchawi na mabalaa kumbe ni upigaji Tu.

Wanapangwa vilema wa uongo ambao wanafundishwa namna ya.kucheza na viungo vyao na kweli ukiwaona utadhani ni vilema kweli lakini kumbe ni sarakasi za 5G!

Sasa kubwa kuliko yote ambayo watu wengi hawajui ni kuwepo na watu special ambao kazi yao ni kuwatambua kondoo wapya katika kanisa lao. Hawa wakisha kulenga basi watakuja ulipo kaa na kuzungumza na wewe mawili matatu na mwisho wa siku utatoa changamoto zako.

Sasa anakuwa makini kusikiliza halafu anaenda kwenye daftar na kuandika jina lako na changamoto zako mbalimbali, halafu zile data anapewa Nabii au Mtume whatever the case, huenda zikapita siku tatu au nne au hata wiki.

Unashangaa siku Nabii anakuita wewe fulani au wewe mama mwenye kitenge fulani njoo hapa madhabauni kuna kitu nimeona, anaanza kutaja changamoto zako na ukicheki ni kweli. Kwa ubwege wako ushasahau kuwa kuna siku uliuza faili lako lote kwa kondoo wenzako.

Basi utaona daah umekutana na bonge la Nabii kumbe upuuzi mtupu, hapo unaaza kupigwa mahela mwanzo mwisho.

Hilo nimelidhibitisha kwa mtu wangu wa karibu hapa Tanzania, alienda Kanisa fulani yeye ni Muislamu, akaenda Kanisa fulani, akaambiwa wewe si umeolewa mke wa pili, kuna changamoto moja mbili tatu na kweli Nabii anagusa mule mule. Lakini alishasahau kuna kipindi alikutana na mdada mwenzake kanisani na kuuza faili lake, haya mambo yapo sana.

Na wengine utasikia huyu Nabii yaani anaona sana, yaani ana maono hatari kumbe wanapiga ramli au wanashirikiana na wapiga ramli, unamuona ana maono kumbe mshirikina tu.

Unaweza ingia YouTube na kusechi hii clip na ukajionea mambo kibao, nimekupa kwa uchache Tu.

Kutoka kwangu ETUGRUL BEY

Ni hayo tu!
 
Juzi mu TV niliona watu Fulani wakitoa ushuhuda pale kwa mkapa usiku wa manane. Kuna jamaa wa Moro na mdada mmoja mpare, kwa kweli wale walipewa kidogo kitu na kutoa ushuhuda.
Kuna huyu mhuni wa Arusha, mkware mpenda wake za watu utadhani mkewe Hana K, huyu muhuni anayedai alikutana na Yesu Kristo LIVE lakini tarehe haikumbuki.(utokewe na Yesu halafu tarehe uisahau)
Sijajua namna ya kuwanasua wafuasi wake. Kuna huyu wa Dar anayewaambia waumini wampelekee nywele au kope au sharubu au ndevu au..mav.....

Mbombo ngafu
 
Yani ni hatar Sana mkuu,kiukweli kabisa hatusemi kwa ubaya lakini usanii ni mwingi Sana siku hizi
 
nachukulia habari hizi kwa tahadhari Bwana ERTUGUR BEY unajulikana we ni mrengo gani. habari cant be reliable, ingukua umeandika kuhusu masheck feki ningekuamini.
Nakuelewa mkuu ndio maana nikaona isiwe tabu watu waingie you tube wacheki wenyewe

Huwa napenda ukweli dawamu
 
Kila kukicha unahaha na dini za watu hiki ndio kitu mnafurahiaga wavaa kobazi na mnafana kwelikweli kwa kusumbukia dini za watu mkiamini ya kwenu ndio sahihi na salama. Upo gizani na mtumwa
 
Kuna mchungungaji juzi naee kacheza mchezo Kama huo.kaja ukumbini kwake mapema asubuhi nawaumini wake kaawambia wawahi wakafanya hivyo.sasa wakati anaendelea kuombea namikelele yake ghafla ikaja gari imejaza watu ndani ikasimama nje yaukumbi.dereva akatoka akaingia ndani yaukumbi akatoka namchungaji mchungaji alivyofungua mlango akawa anafoka kwakuomba kumbe wale watu wanadai yule anae ombewa nimsukule walisha mzika miaka kumi ilio pita ila walivyo kuja kuombewa na kuchukua mafuta wakaenda kumwaga nyumbani ndio huo msukule ukatoka.kwahio wakasema wamekuja kutoa ushuhuda.msukule ukawekwa pembeni yaukumbi mchungaji akawambia waumini wainuke wakashuhudie muujiza alio ufanya.nasisi tukapata fursa yakuona.ulemsukule unatisha kwakweli unatema maudendatu mikucha inarangi nyeusi minywele Kama yamzungu inarangi nyeusi tiii.ukiangalia maramoja hutamani kurudia.baada yakufanya hivyo sasa hivi anawaumini balaa.
 
Tahadhari huu Uzi Una Ukakasi kwa baadhi ya watu :

Hii habari nimeipata baada ya Kuangalia KTV Television inchini Kenya ni habari ya kichunguzi katika nyumba za ibada.

Hawa ni Manabii WA kizazi hiki na majina Yao makubwa makubwa mara Mtume mkuu,Nabii na kadhalika,jinsi wanavyofanya utapeli kuwahadaa kondoo wao kuendelea kuwapiga mahela.

Ziligundulika mbinu zifuatazo:

Mosi, kuwapanga watu watoe shuhuda mbali mbali ikiwemo kuugua ukimwi na maradhi mengine mbali mbali na kisha baadae kusema wamepona,na wengine hurekodiwa na kurushwa katika Redio kana kwamba wako live wanapiga simu lkn kumbe walicheza Hilo picha kitambo Tu.

Kutolewa vitu mwilini kwa Miujiza lakini ni uwongo mtupu,mfano walionekana watu wanaweka miguu katika mabeseni na kuoshwa miguu na maji kuwa mekundu, kumbe kuna kemikali moja wachungaji wanapaka katika mikono Yao halafu baada ya mda mfupi wakiwa wanasugua miguu ya kondoo wao inayeyuka na maji yanakuwa mekundu. Hapo inasemwa umetolewa uchawi na mabalaa kumbe ni upigaji Tu.

Wanapangwa vilema wa uongo ambao wanafundishwa namna ya.kucheza na viungo vyao na kweli ukiwaona utadhani ni vilema kweli lakini kumbe ni sarakasi za 5G!

Sasa kubwa kuliko yote ambayo watu wengi hawajui ni kuwepo na watu special ambao kazi yao ni kuwatambua kondoo wapya katika kanisa lao. Hawa wakisha kulenga basi watakuja ulipo kaa na kuzungumza na wewe mawili matatu na mwisho wa siku utatoa changamoto zako.

Sasa anakuwa makini kusikiliza halafu anaenda kwenye daftar na kuandika jina lako na changamoto zako mbalimbali, halafu zile data anapewa Nabii au Mtume whatever the case, huenda zikapita siku tatu au nne au hata wiki.

Unashangaa siku Nabii anakuita wewe fulani au wewe mama mwenye kitenge fulani njoo hapa madhabauni kuna kitu nimeona, anaanza kutaja changamoto zako na ukicheki ni kweli. Kwa ubwege wako ushasahau kuwa kuna siku uliuza faili lako lote kwa kondoo wenzako.

Basi utaona daah umekutana na bonge la Nabii kumbe upuuzi mtupu, hapo unaaza kupigwa mahela mwanzo mwisho.

Hilo nimelidhibitisha kwa mtu wangu wa karibu hapa Tanzania, alienda Kanisa fulani yeye ni Muislamu, akaenda Kanisa fulani, akaambiwa wewe si umeolewa mke wa pili, kuna changamoto moja mbili tatu na kweli Nabii anagusa mule mule. Lakini alishasahau kuna kipindi alikutana na mdada mwenzake kanisani na kuuza faili lake, haya mambo yapo sana.

Na wengine utasikia huyu Nabii yaani anaona sana, yaani ana maono hatari kumbe wanapiga ramli au wanashirikiana na wapiga ramli, unamuona ana maono kumbe mshirikina tu.

Unaweza ingia YouTube na kusechi hii clip na ukajionea mambo kibao, nimekupa kwa uchache Tu.

Kutoka kwangu ETUGRUL BEY

Ni hayo tu!
Clip inaitwaje, niisake kwa jina gani?
 
Back
Top Bottom