Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Hii ndio Familia ya Agustino Mahiga

Kama walivyo 95% ya mabalozi na maofisa wa ngazi za juu wa serikali ya Tanzania huyu hajui shida ni nini na watu wenye shida wanaishi vipi .................................

Mkewe ni Mbunge Janeth Mbene, Watoto wake wamesoma shule za International schools na hawajui Kiswahili vizuri), mtoto wake mwingine wa kufikia ndio PR director wa NSSF.

Huyu anajua zaidi mitaa ya Upper East side of Newyork kuliko Kariakoo, Ruvu, Kigoma, Tabora, Mwambani na Visiga

Huyu anajua zaidi tena kwa kichwa North Delegates Lounge bar kuliko Kwa Macheni auBreak Point (sidhani hataka anazijua)

Cliques zake tanzania ndio hao hao ma diplomats wenzake waliozaliwa na silver spoon kuliko hao wenyeviti wa serikali za mitaa.

Ukimuuliza bei ya nyanya tanzania hajui lakini anaspend close to $700 kununua tai moja ..................

Mahiga anaweza kuwa ana uwezo wa kuongea na hao madiplomats na hao watu wa matawi ya juu wenzake lakini sidhani kama yeye na familia yake na marafiki zake na mnaompigia debe humu Jamii Forums mnaweza kutushawishi kuwa ni mtu ambaye yuko IN TOUCH na watazanaia waliopo on the ground

Nina wasi wasi kama aliwahi kufika ofisi za CCM kariakoo na ukimuuliza klabu gani ilishinda Upingwa wa ligi kuu mwaka jana sidhani kama anajua.

Ila ingekuwa yule binti yake mlokole ( MODESTA) anagombea tungemfikiria lakini kwanza aanze na level ya udiwani kumpima lakini si baba mtu ambaye najua fika kuwa mjumbe wa nyumba 10 hawezi kupita.

Tazama Video za Watoto wake.

NImepata raha kidogo na hasa baada ya kuangalia ombi lake la kutaka kuwa Rais, nikaona ni mzee anaelekea 70s lakini nywele imepigwa rangi nyeusi ku-disguise, mara moja nikajua hakuna kitu hapo. Ni mtu anayejua aliyoyasoma lakini siyo presidential material.

Inaonekana pia watoto wamejazwa hisia za matawi ya juu maana naona New York wanaitaja kwa bold fonts kuliko Dar es Salaam. Nahisi ukiwatania kuwa wao ni New Yorkers watafurahi sana kuliko kuwa Wahehe wa Iringa. Shame!

Lakini kwa watu kama hawa wanashindwa kuelewa kwamba wao ni Waafrika. hawawezi hata siku moja kuwa american wenye thamani. Wanaweza kuwa black American lakini itawasaidia nini kama hao walioingizwa kwa utumwa bado ni bullet targets ya polisi wa kimarekani? Kwa nini utamani kuwa citizen wa daraja la pili ugenini kuliko kuwa citizen wa nchi yako?

Tunawasubiri tu tuone vituko maana ukiona mama anabaki TZ bila watoto wake, na watoto anawasukuma New York waishi na baba! hiyo siyo familia kama ulivyoiita.
 
Nafikiri Mahiga achambuliwe si kwa sababu ya uwezo wa kimaisha alionao bali kimaadili na mustakabali wa kitaifa. Kama mtoa mada unataka kuihusisha familia yake tupe taarifa ni vipi ametumia madaraka yake vibaya kujineemesha yeye na familia yake ikiwa ni pamoja na kucheza dili zinazotugharimu hivi leo.

Je ametumia mamlaka yake vibaya kuwapigia debe watoto wake wapewe ulaji popote walipo leo au juhudi zao zinawabeba? Je wapo hapo walipo by merits au kwa kubebwa? Nafikiri tuache kudandia hoja na badala yake tufanye tafiti juu ya wagombea zitakazo tusaidia kutupeleka mbele badala ya kupakana matope.

Hivi mjasiriamali asiwe tajiri kutokana na juhudi zake kisa watanzania ni masikini? Hebu tufanye kautafiti kidogo, toka unaamka saa 11 asubuhi mpaka unalala saa 5 usiku ni asilimia ngapi ya muda umeutumia kwa mambo ambayo ni productive na ngapi kwa mambo ya kipuuzi? Jamani juhudi zinalipa na watu wapo serious.

Mahiga alishakuwa Muhitimu wa Ph.D akiwa na miaka 30 na sasa anaelekea miaka 70. Ametumia vema elimu yake ikamfikisha hapo alipo yeye na familia yake, unataka aishi kama Matonya? Kama akili ya kitanzania ndivyo ilivyo basi tusubiri miaka 50 mingine kuendelea hata atawale malaika

Tungepata watanzania milion 1 wenye akili kama yako, I swear within 5 years tungewazidi hadi South Korea kwa uchumi na maendeleo.
Hilo ndo tatizo la tanzania ambalo ndo lililonifanya hata mimi niamue kumuunga mkono Prof Muhongo kwa sababu ndo aliyeligundua na ndo labda akikaa pale juu atabadirisha hizi mindset za kijinga za watanzania wenzetu.
Narudia tena tatizo kuu la watanzania ni kuendekeza siasa kwenye kila kitu,porojo porojo, uvivu na kuendekeza fitna, chuki na wivu bila kusahau ushabiki usio na maono na kulalamika. Niliposoma post ya mtoa mada hadi nikaona aibu kwa kweli.
Jamani watanzania tubadirike, tuwe watu wa kujituma na kufanya kazi. tuwe watu wa facts na sio siasa siasa tu na maneno mengi na chuki na wivu.
Hivi kweli kwa mtu mwqenye akili an ayefikiri si angejiuliza tuu mahiga amehudumu kwenye nafasi gani duniani hadi alipofikia hapa? Si angejiuliza tu kwenye hizo nafasi alikuwa anapata posho za namna gani na mshahara wake ulikuwaje? Si angejiuliza tu kwa position alizoshika nje ya nchi familia yake ilikuwa inahudumiwa na nani???? Alafu unajiuliza tu kabla ye kwenda huko nje ya nchi alilitumikia taifa lake kwenye nafasi gani?????

Yaani kama hamuwezi ulizeni jamani. Hii forum ina heshima sana sio kuleta vitu vya ajabu ili mradi tu mchafue watu. Kweli Tanzania we have a very long way to go.
T
 
Ila huyu Mahiga nae sijui ametokea wapi na haya mambo ya Urais, saa nyingine nahisi ukiwa mwanaccm unahitaji kuwa na akili mbovu kidogo. Heshima na kazi alizozifanya kwa taifa hili kwakweli sikutegemea kumsikia anaingia kwenye mambo ya siasa za CCM na CHADEMA, hajifunzi kutoka kwa watu kama kina Salim Ahmed Salim mtu wa kaliba kama yake akaja kuvamia siasa za bongo wakamvuruga mpaka hana hamu. Ila simshangai sana kwani naona na Mzee wangu Hass Kitine nae kajitosa sasa sijui ni nini hii??
 
Ndiyo maana nikasema habari za Mahiga na Janeth siwezi kuziongelea. Isipokuwa watoto wanaoogopwa hapa, wamesomeshwa na Janeth na muda mrefu amekuwa single mother.

Sasa ikiwa huyu mgombea uenyekiti wa ccm hawezi hata kuwa declare, au labda hajui kama nao ni watoto wake, au anao wengi ameamua kufanya wastani, maana (tunasikia mwingine yuko Iringa nasikia na mama yake alishafariki, na binti yule alikuwa na akili sana darasani ila hakuwa na msaada kaaishia form 5) lakini ni masuala binafsi tuyaache.

Tukijadili mahusiano yake ya kimapenzi, tutakuwa hatumtendei haki, kwa kuwa si Mkapa, Mwinyi wala Jk wenye sifa za kuwa models kwenye suala la mahusiano na wanaosemekana ni wapenzi wao. yako mengi kwenye carpet lakini hayasemwi kwa kuwa hayana maslahi kwa taifa.

Aangaliwe yeye kama yeye na watoto wa Janeth waachwe. Wamepitia mengi sana hadi hapo walipo. Tujikite kwenye mada. Dr. Mahiga, anasifa za kuwa raisi wa ccm?
Sifa hana,
Sababu hayajui vizuri matatizo ya Watanzania.
 
Nimesema, tatizo ni WIVU!. Sasa badala ya kuelekeza mashambulizi kwa Ccm iliyowanyima elimu nzuri wao wakawa katika hali walizonazo, wanaelekeza mishare kwa waliofanikiwa? Hii ni wapi na wapi

Nimewaambia, adui yao ni Ccm na wao wenyewe kuweka madarakani kiongozi asiyejua thamani ya elimu. Waipige mawe ccm lakini si watoto waliofanikiwa kufapata elimu safi kwa juhudi za wazazi wao!. Kama wanaona Janeth kafanikiwa sana kwa watoto, na mafanikio hayo wanayatamani, wasingekubali upuuzi wa Div. 5 na BRN!, ikiwa ni pmaoja ua uchakachuaji wa matokeo ya shule unaofanywa na serikali ya ccm.

Lakin pia waliakiwa walazimishe serikali iache kufanya maamuzi ajizi katiak suala la elimu ambalo ndilo uhai wa taifa!. Sasa matokeo yake mnaanza kuyaona hata kabla jua halijachanua!.

ILA KATIKA YOTE JANETH NA WATOTO WAKE WAACHWE SALAMA!. Hawakutunga sera za kuua elimu. Iulizwe serikali ya kisanii na kifisadi inayoanzisha shule za kata bila kuwa na mtazamo wa elimu bora!.

CHUKI GHADHABU NA HAMAKI ZOTE WAPELEK CCM WALIKOUA ELIMU NA SI KWA JANETH NA WATOTO WAKE!.

Pole kwa kushikwa pabaya mzee. . . . .Ila huwezi mshauri mtu aichukie CCM halafu awapende waliofaidika na mfumo huo kama unataka kuita spade ni spade basi kubali ichukiwe CCM na yatokanayo na mfumo mzima, tatizo nchii hii hata baadhi ya wazee kama wewe sasa hivi mnashindwa kuwa wakweli na wawazi na ndio maana tunakwama. . . . . . . . Unapoamua kuwa mkweli kuwa mkweli hata kama baadhi ya watu wako wataumia na ukweli husika!!!!!

Class based hatred huwezi iongea na kuiondoa kama unavyoiweka wewe. . . Mtu kazalia njiani kwa kukosa huduma labda na mtoto kapoteza uje umwambie muache X salama na umoende wakati huyo X hajui hata usafiri wa jumuia ukoje (labda) na huyi muathirika anajua wazi kuwa mfumo uliosababisha yeye kujifungulia njiani ndio huo uliosababisha X kujifungulia sehemu nzuri na kisomesha watoto. . . . . .,

kama kweli u mtu mzima basi ongea dhati ya moyo wako kwa ku adress source ya tatizo kuliko kuwa buffer na kuongea suoerficially. . . . . Nchi yetu wote watu wasipoona faida ya umoja basi chuki kama hizi za kwenye uzi huu huwezi ziondoa kwa kuhadithia historia ya mtu mmoja mmoja
 
Jamani mbona mimi naona binti anaongea kiswahili vizuri tu. Nilichobaini mimi ni kuwa binti anazimudu lugha zote mbili (Kiswahili na English) vizuri tu bila ya kuwa na zile chenga chenga za (izi na ze) tulizozizoe kwenye kile 'chingereza' chetu cha kizungu🙂

Hebu tazama video nilizoambatanisha hapo chini:

==========

UZURI NI SEHEMU YA MAFANIKIO YA MODESTA MAHIGA

https://www.youtube.com/watch?v=klcBtaJBeoE

Modesta Mahiga Speaks to the Women in Uganda

https://www.youtube.com/watch?v=pXTXDGMcLeg
 
Umehoji vizuri Mkuu. Kwa kuwa hili suala ni la ccm na si lakitaifa, ccm wanapaswa ku stick kwenye standards na katiba yao inasemaje. Si Mkapa, Mwinyi wala Kikwete wangepitishwa kugombea kama ccm wangalikuwa na kigezo cha kuangalia undani wa mahusiano ya wagombea na hao wanawake wanaopigaga nao picha, au tabia zao za kimapenzi. Hakuna hata mmoja wao angevuka chujio, wote wamejaa scandals.

Wawapime kwa vigezo vyao kama walivyojiwekea kwa mujibu wa katiba yao bila hila wala unafiki. Ninajua hawa wote wanaishia kuwa wenyekiti wa ccm taifa na hakuna raisi atatoka ccm.

Lakini wakiwaleta kwetu sis waTanzania, tutawasasambua kwa vigezo vya tiba ya mateso yetu!. Mateso yetu ni mengi na hatuwezi kuyaorodhesha. Na hapo ndipo ninasema ccm haina uwezo wa kuleta mtu kwetu eti tumpigie kura. Itakuwa ni kuwadhalilisha makada wao.


You might be having a good point. . . . . hivi haki za mgombea zinaanzia wapi mpaka wapi na za mpiga kura zinaanzia wapi mpaka wapi??!!!
 
mahiga who? the kids are trying to find life under tanzania sun.... really?
 
hao vijanaatanzania hivimbona kama cyo watanzzania hivi mbona hiyolugha wanaongea ciielewi:sad::sad:
 
Sijaona point hapo...nilidhani ni fisadi...kwani ni kosa kuwa na maisha mazuri? ...nadhani wote tuna struggle watoto zetu wawe na best life...angechekesha kwanza watoto wake wangekuwa na msoto akati ameshika position kubwa kubwa....
 
Umehoji vizuri Mkuu. Kwa kuwa hili suala ni la ccm na si lakitaifa, ccm wanapaswa ku stick kwenye standards na katiba yao inasemaje. Si Mkapa, Mwinyi wala Kikwete wangepitishwa kugombea kama ccm wangalikuwa na kigezo cha kuangalia undani wa mahusiano ya wagombea na hao wanawake wanaopigaga nao picha, au tabia zao za kimapenzi. Hakuna hata mmoja wao angevuka chujio, wote wamejaa scandals.

Wawapime kwa vigezo vyao kama walivyojiwekea kwa mujibu wa katiba yao bila hila wala unafiki. Ninajua hawa wote wanaishia kuwa wenyekiti wa ccm taifa na hakuna raisi atatoka ccm.

Lakini wakiwaleta kwetu sis waTanzania, tutawasasambua kwa vigezo vya tiba ya mateso yetu!. Mateso yetu ni mengi na hatuwezi kuyaorodhesha. Na hapo ndipo ninasema ccm haina uwezo wa kuleta mtu kwetu eti tumpigie kura. Itakuwa ni kuwadhalilisha makada wao.

Labda unachosema ndicho ila. . . . .Raia ana haki ya kujua taarifa za anayetazamiwa kuwa kiongozi wake kwa njia ya kura ili aamue akiwa na taarifa sahihi. .
 
Hao ulioishi nao wakikuongoza kwa miaka 30 iliyopita ndio Hao wamekuacha katika hali mbaya uliyonayo sasa hivi.

Unategemea miujiza?uwezo wa kiongozi haujalishi anafanya Kazi sehemu gani,huyo mahiga ni insider kuliko Hao ma-insider wa baraza La mawaziri,kwa hiyo shimbo akirudi utamuita outsider kwa kuwa kawa balozi nje ya tz?
Na akili zetu fupi tunadhania kuijua Tanzania ni kuzurula nchi nzima.nasubiri vichaa waliochukua fomu kurudi na kutuambia wametafuta wadhimini nchi nzima,sasa wanaijua Tanzania vizuri na waajua matatizoya watanzania kwa kuwa wametembeaikoa tote.
Sound policies hazijitaji kuwepo Ngara au lushoto kuzi-implement.

Swami La mwisho,unafahamu Kazi za mabalozi zetu nje ya nchi?hasa wale UN?ukilijibu hili hautauliza tena maswali obvious kama "kipofu anaonaje?"

Mkuu Kimweri,siimanishi kwamba ni lazima tuwachague waliotuongoza for the last 30 yrs.ni kwamba kwenye hao viongozi ambao wamekuwepo kuna wanaofaa na wasiofaa.ndani ya ccm na vyama vya upinzani kuna viongozi wanaofaa na wasiofaa.tunawajua vizuri kabisa kutokana na uwepo wao miongoni mwetu kwa kipindi kirefu cha nyuma.kwamba atleast tunaelewa ufanisi na uadilifu wao.tofauti na Dr mahiga ambaye tumeanza kumsikia juzi.kwamba tumchague kwasababu alikuwa UN?Migiro na Tibaijuka nao walikuwa UN..hivyo nao pia wanastahili kupewa uraisi kwa kigezo cha kuwa UN?Kitine nae alikuwa usalama nae tumpe uraisi??
Shimbo huwezi kumfananisha na Mahiga Mkuu.shimbo amekuwa Tanzania muda mrefu sana na kabla ya kuteuliwa kuwa balozi nje ya nchi..china amekwenda miaka miwili au mitatu iliyopita..
Ndio mkuu kimweri,nazielewa kazi za mabalozi wetu nje ya nchi..be blessed!
 
Sijaona point hapo...nilidhani ni fisadi...kwani ni kosa kuwa na maisha mazuri? ...nadhani wote tuna struggle watoto zetu wawe na best life...angechekesha kwanza watoto wake wangekuwa na msoto akati ameshika position kubwa kubwa....
Inategemea na perspective yako na class unayoishi. . . . . .. Tujaribu kuelewa kuwa maisha na maana yake haiko sawa kwa kila anayepumua chini ya jua. . . . .. Ninachojifunza katika uzi huu ni kuwa sasa candidates sio tu wanaagaliwa objectively ila mwaka huu subjectivity na personal inclinations zitasumbua sana!!
 
Nilipata wasaa wa kuongea na balozi Mahiga alivyokuwa anatuwakilisha Umoja wa Mataifa kwa weledi na uadilifu mpaka Tanzania tukapewa kiti katika baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa.

Katika maongezi yetu, tukagusia masuala ya security. Wakati huo "War on Terror" ya George Bush ikikuwa imeshika hatamu.

Balozi Mahiga alinifungua macho na kunieleza kwamba, ingawa kukabiliana na ugaidi ni kipaumbele, lakini kuna watu wanakufa kila siku Afrika huko kwa sababu ya "food security". Kwa hivyo, alipigania habari za vitu kama food security zipewe kipaumbele sawa na kupigana na ugaidi.

Mtu kama huyu aliyejenga ushawishi na kukubalika mpaka Tanzania ikapewa kiti katika baraza la usalama la UN na kutetea maslahi ya nchi masikini humo, leo hii unakuja kusema kirahisi tu kwamba hawezi kuelewa matatizo yenu,bila hata kumjua na kujua kafanya nini, katoka wapi, kafikaje hapo alipo etc, unakuwa humtendei haki na unavunja moyo watendaji wengine wanaojitoa kufanya utumishi wa umma kwa dhati.

Mahiga alivyokuwa UN alikuwa anategemewa kusafisha mambo mara kibao watu kama kina Membe walivyokuwa wanaharibu kwa kukosa weledi hapo nyumbani.

Leo shukurani ya punda mateke.

Bado sijaelewa kwa nini Mahiga ameamua kuingia kwenye Mud pit that is our political scene nyumbani. Kutakuwa na kitu kimemsukuma, au kuna mambo yameharibika kuzidi repair nyumbani. He is a canon in a knives fight. hawa kina Membe Lowasa, sijui Makamba,Mwigulu wanajua hawaingii hata robo, ndio maana wame-unleash their dogs to attack the heavy weight.

Yani Nyumbani kumejaa wababaishaji imefikia wakati akija mtu mwenye weledi anawekewa zengwe. hali hii ilikuwepo pia kwenye taasisi za umma. Akija staff msomi, basi vikongwe wa ile sehemu watafanya kila hila kumkatisha tamaa aondoke ili waendeleze mediocre leagues zao.
 
mtoa mada naona ana stress zake, na labda hasa ana WIVU juu ya watoto wa mahiga hasa hawa wawili ambao wanaonekana sana kwenye media. Haiwezekani mgombea awe baba yao yeye alete video za watoto, inahuu?
Haya some corrections:
1. Hivi mtu anaitwaje 'posh boy' wakati historia yake inaonyesha alizaliwa katika umaskini uliokithiri kiasi cha kushindwa ku-afford michango ya mablanketi sijui na makorokoro gani huko enzi za mwalimu na akasomeshwa kwa michango ya kanisa? Huyu ni wale watu typical ambao walikuwa wanataniwa 'wanasomeshwa na kijiji'! Leo hii mtoa mada anasema huyu naye ni silver spooner? Hizi ni chuki tu.

2. Mke wake ni huyu hapa kama alivyokuja naye kuchukua form na sio Janet Mbene.
IMG_6943.JPG


3. Wabongo sijui kwa nini wanachukia watu wenye mafanikio bila sababu. Utadhani Mahiga huko UN alikuwa anafanya dili zake na sio za serikali. ARRRRRGh!
 
Mkuu Kimweri,siimanishi kwamba ni lazima tuwachague waliotuongoza for the last 30 yrs.ni kwamba kwenye hao viongozi ambao wamekuwepo kuna wanaofaa na wasiofaa.ndani ya ccm na vyama vya upinzani kuna viongozi wanaofaa na wasiofaa.tunawajua vizuri kabisa kutokana na uwepo wao miongoni mwetu kwa kipindi kirefu cha nyuma.kwamba atleast tunaelewa ufanisi na uadilifu wao.

Acha porojo wewe, UPINZANI hakuna mtu mwenye calibre ya MAHIGA, they will need at-least 30 years to build that resume. CCM kwenyewe wenye resume nzito kama ya jamaa hawazidi wa-5 and none is below 65 years old.

Wanasiasa wa Tanzania ni sampuli za kina Mbowe na Slaa, wanaopiga kelele serikali iache matumizi mabaya halafu wao wanapewa ripoti chafu na CAG,au kina Slaa wanaoropoka kuhusu vitu wasivyo na uhakika navyo, au kina Tundu Lisu, wanaomkebehi baba wa taifa bungeni halafu kesho yake wanaenda kuzuru kaburi lake kutaka baraka zake. Hao ni wanasiasa njaa, ambao mtu yeyote asiyekuwa influenced na tumbo hawezi kuwachagua kuwa raisi wa nchi.

Ukija CCM hao mnaojua ufanisi wao ndio hao kina lowassa kutwa kugawa fedha makanisani na misikitini, akiulizwa vision yake anasema safari ya matumaini, DJ weka mziki. Au hao Kina Makamba, ambao wanaleta story telling kwenye vision,na ahadi amazo hawajui hata watazitekeleza vipi, au kina wasira wanaotamba kuleta mapinduzi ya kilimo in 5 years wakati wamepewa wizara toka mwaka 73, hakuna walilofanya.Watanzania mmezoea kudanganywa, kugeuzwa majuha na kufanywa mabwege. ENDELEEENI kuchagua HOVYO, ila mie nitakuwa mbaya wa wengi humu 2016, maana sitavumilia ulalamishi juu ya serikali ambayo mnaipigia debe humu ndani ichaguliwe. Msitegemee mchague hovyo halafu muongozwe vizuri. Huo ni UJUHA.

tofauti na Dr mahiga ambaye tumeanza kumsikia juzi.kwamba tumchague kwasababu alikuwa UN?Migiro na Tibaijuka nao walikuwa UN..hivyo nao pia wanastahili kupewa uraisi kwa kigezo cha kuwa UN?Kitine nae alikuwa usalama nae tumpe uraisi??
Shimbo huwezi kumfananisha na Mahiga Mkuu.shimbo amekuwa Tanzania muda mrefu sana na kabla ya kuteuliwa kuwa balozi nje ya nchi..china amekwenda miaka miwili au mitatu iliyopita..
Ndio mkuu kimweri,nazielewa kazi za mabalozi wetu nje ya nchi..be blessed!

Umeanza kumsikia juzi kwa kuwa umezaliwa JUZI. hebu jenga busara hata za kuazima. Tibaijuka unamfananisha na Mahiga?halafu you expect me to take you serious?sio kila muajiriwa wa UN ana weight inayofanana, au hujui hata hapo nyumbani kuna stafa lukuki wa UN?

Nimekupa mfano wa Shimbo kwa kuwa ninaamini ndio unaujua wewe uliyezaliwa juzi. Shimbo hata akikaa Huko china kwa miaka 20, anabakia kuijua Tanzania VIZURI kuliko wewe uliyekuwepo hapo Dar tokea unazaliwa.Unanielewa lakini?

Kuijua nchi kunategemea na aina ya majukumu ambayo mtu husika amewahi kuwa nayo. Hutakiwi kumchagua kwa kuwa alikuwa UN,Mchague kwa kuwa kwa kipindi Kirefu amekuwa one of Tanzania's very best diplomat if not the best. Anafaa kwa kuwa he has deep understanding of Tanzania through his positions over the years. Because he is capable, because he is by far the cleanest, together with Makongoro when it comes to UADILIFU.
 
Back
Top Bottom